
25/07/2025
Billnass na Nandy sio tu wanandoa na wasanii wakubwa, bali pia ni wazazi wa mtoto wao wa k**e, Naya. Kwa sasa, jina la binti yao limegeuka kuwa sehemu ya ubunifu wa sanaa yao. Kwenye wimbo mpya wa Billnass How Come, anasikika akisema “Baba Naya, usiniguse” – kauli inayotafsiriwa k**a ujumbe wa kujiamini, kuwatahadhalisha watu kujiweka mbali na yeye, na kusonga mbele bila kuyumbishwa.
Nandy naye amejumuisha kauli ya “Mama Naya, usiniguse” kwenye wimbo wake mpya Tonge Nyama, akionyesha kuwa jina la Naya limekuwa nembo mpya katika muziki wake.
Ubunifu huu umeleta utambulisho wa kifamilia kwenye kazi zao, ukionyesha namna wanavyotumia maisha yao binafsi kuwaburudisha mashabiki kwa njia ya muziki.