Swahili Forums

  • Home
  • Swahili Forums

Swahili Forums Chombo cha habari kinachorusha maudhui yake mtandaoni | E-Mail:[email protected] |0766081920

18/10/2023

‎Follow the SwahiliForums channel on WhatsApp:

Unamjua huyu😂😂😂? Angusha jina lake kwenye komenti🤩
03/10/2023

Unamjua huyu😂😂😂? Angusha jina lake kwenye komenti🤩

  Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia kwa mwezi Septemba. Ronaldo ame...
03/10/2023

Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia kwa mwezi Septemba. Ronaldo ametwaa tuzo hiyo baada ya kufunga magoli matano na kutoa pasi 3 za usaidizi wa goli (assist) kwenye mwezi huo.

Hii ni tuzo ya pili mfululizo kwa Ronaldo baada ya kutwaa tuzo ya mwezi Agosti kwenye Saudi Pro League baada ya kufunga magoli matano na assist mbili kwa mwezi Agosti.

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

  Hivi karibuni K**a ulipita kwenye page ya timu ya Yanga Princess utakuwa umemuona mwanadada wa kizungu kutoka Marekani...
03/10/2023

Hivi karibuni K**a ulipita kwenye page ya timu ya Yanga Princess utakuwa umemuona mwanadada wa kizungu kutoka Marekani “Kaeda Wilson” akifanya mazoezi na timu hiyo.

Yanga wameamua kuweka kiingilio cha Tsh. 1000 siku ya kesho mashabiki wanaotaka kwenda kuangalia Mazoezi ya Mwanadada huyo wa kizungu raia wa Marekani.

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

 :Mfanyabiasha wa kimataifa, Rostam Azizi amesikitishwa na uwepo wa matapeli wa mitandao ya kijamii wanaosambaza taarifa...
02/10/2023

:Mfanyabiasha wa kimataifa, Rostam Azizi amesikitishwa na uwepo wa matapeli wa mitandao ya kijamii wanaosambaza taarifa za uongo zinazomhusisha na kuwekeza hisa katika Klabu ya Soka ya Yanga.

Rostam ametoa taarifa hiyo ya kusikitishwa na utapeli huo leo Oktoba 2, 2023 jijini Dar es Salaam huku hakisisitiza kuwa hajakutana na uongozi wa Yanga k**a ilivyoelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya matapeli hao ambayo imemsababishia usumbufu mkubwa, Rostam mbaye pia ni Mwenyekiti wa kundi la makampuni ya Taifa (Taifa Group Ltd) anadaiwa kukutana na viongozi wa Yanga na kufikia nao makubaliano ya yeye kuwa tayari kuwekeza kiasi cha Sh bilioni 30 k**a sehemu ya asilimia 49 ya hisa za mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.

Mbali na hilo, matapeli hao wa mtandaoni walikwenda mbele zaidi na kueleza kwamba, Rostam alikuwa amefikia makubaliano na Yanga kwa kuutaka uongozi wa klabu hiyo kutafuta wawekezaji wengine wawili zaidi ambao nao wangetoa kiasi cha Sh bilioni 20 kwa pamoja ili kukamilisha nakisi ya hisa asilimia 49.

“Katika hili, napenda kuwahakikishia wanachama na wapenzi wa timu ya Yanga na wapenda soka kwa ujumla ambao wamekuwa pia na dukuduku kubwa baada ya kusoma taarifa hizo potofu kuwa sijakutana na uongozi wa timu ya Yanga wakati wowote hivi karibuni kwani niko nje ya nchi kwa shughuli mahususi ya kifamilia kwa muda mrefu sasa.

“Hivyo napenda kuufahamisha umma wa Watanzania kutambua kuwa, kila wakati ninapokuwa na jambo linalogusa maslahi mapana ya nchi au uwekezaji nimekuwa nikijitokeza hadharani mimi mwenyewe au kwa kutoa taarifa rasmi inayotoka ofisini kwangu moja kwa moja.

“Kwa sababu hiyo basi, natoa wito kwa Watanzania kuwa makini na matapeli wa aina hiyo mitandaoni ikiwa ni pamoja na kuzipuuza taarifa za namna hiyo na natoa onyo kali kwa matepeli hao wa mitandaoni kukoma kutumia majina ya watu isivyopaswa,” ameeleza Rostam kupitia taarifa hiyo.

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

 :Serikali imeruhusu mabasi ya abiria kufanya usafirishaji kwa saa 24 kuanzia Oktoba 1,2023, baada ya kuweka zuio kwa ta...
30/09/2023

:Serikali imeruhusu mabasi ya abiria kufanya usafirishaji kwa saa 24 kuanzia Oktoba 1,2023, baada ya kuweka zuio kwa takriban miaka 29.

Zuio hilo liliwekwa mwaka 1994 la kuzuia mabasi kusafiri usiku, lililosababishwa na matukio ya utekaji wa mabasi uliohusisha uporaji na udhalilishaji wa abiria, ajali mbaya za mabasi zilizogharimu maisha ya watu na wengine kupata ulemavu wa kudumu.

Akiongea na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini amesema, Serikali imefikia uamuzi huo baada kuboresha miundombinu ya usafiri husuan barabara kuu na barabara za mikoa, na hivyo kuifanya nchi kuwa moja ya nchi zenye usafiri wa barabara unaoaminika na bora.

Aidha, amesema wafanyabiashara wanaomiliki mabasi hayo ambao wako tayari kufanya safari kwa saa 24 ni muhimu wakazingatia Sheria, Kanuni na Miongozo kuhusu usafiri na usafiri wa abiria.

“ Katika kutekeleza uamuzi huo wenye nia njema madereva wa mabasi wanapaswa kuthibitishwa na LATRA kwa mujibu wa miongozo iliyopo. LATRA inapaswa kutoa ratiba za safari za saa 24 kwa kushirikisha watoa huduma, na kuhakikisha Mfumo wa VTS na kituo cha mawasiliano vinafanya kazi wakati wote.” amesema Sagini.

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

Tuambia umemtambua nani kwenye hii picha ?
30/09/2023

Tuambia umemtambua nani kwenye hii picha ?

 :Mchezaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema kuwa wakati anajiunga na Azam FC alikuwa chibonge, lakini kwa sasa amepambana...
29/09/2023

:Mchezaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema kuwa wakati anajiunga na Azam FC alikuwa chibonge, lakini kwa sasa amepambana hadi kukata zaidi ya kilo sita na kujiona mwepesi hivyo kurejesha makali aliyokuwa nayo akiwa Yanga.

Amesema alipojiunga Azam FC alikuwa na uzito wa kilo 75, lakini kwa sasa amebaki na kilo 69 baada ya mazoezi makali kutoka kwa mkufunzi maalum.

“..nilikaa nje karibu miezi minne bila kucheza na kwa bahati nimepunguza uzito na sasa nimeanza kurejea katika makali niliyokuwa nayo Yanga,” alisema Fei Toto akifanya mahojiano na Mwanaspoti.

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

 :Jeshi la Polisi Jimbo la Lagos kupitia K**anda wake ,SP Benjamin Hundeyin wamethibitisha kumk**ata Sam Larry ambaye ni...
29/09/2023

:Jeshi la Polisi Jimbo la Lagos kupitia K**anda wake ,SP Benjamin Hundeyin wamethibitisha kumk**ata Sam Larry ambaye ni rafiki wa Karibu wa Naira Marley kwasababu ya uchunguzi unaoendelea kubaini chanzo cha kifo cha Msanii .

Hundeyin kupitia taarifa hiyo amesema ,

"Ndiyo, Balogun Eletu almaarufu k**a Sam Larry sasa yuko chini ya ulinzi wetu. Kwa sasa anasaidia uchunguzi unaoendelea.”

Inadaiwa sababu ya Kuk**atwa kwa Sam Larry ni pamoja na Kuwahi kushtakiwa na Mohbad kwa kumpiga na Kumtisha kifo ambapo mara kadhaa pia alikuwa chanzo cha kumkosesha Amani msanii huyo.

Aidha sababu nyingine ya kuk**atwa kwake ni kudaiwa pia kuwa baba halali wa Mtoto wa Mohbad.

Sam Larry anaungana na Muuguzi aliyemchoma sindano Mohbad huku watuhumiwa wengine wanaosubiriwa kuk**atwa ni pamoja na Naira Marley aliyesema hivi karibuni anampango wa kurudi Nchini humo kwa ajili ya kulisaidia jeshi la Polisi kuchunguza kifo cha msanii huyo ,Mke wa Mohbad pamoja na watu wa karibu waliokuwepo wakati wa Kifo cha Mohbad.

Mohbad, 27, alifariki tarehe 12 Septemba na kuzikwa siku iliyofuata huko Ikorodu, Jimbo la Lagos.

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

Umewaona wanyama wangapi?
28/09/2023

Umewaona wanyama wangapi?

 :WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa madhehebu ya mbalimbali ya dini nchini waendelee kushirikiana na Ser...
28/09/2023

:WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa madhehebu ya mbalimbali ya dini nchini waendelee kushirikiana na Serikali katika kupiga vita biashara na matumizi ya dawa za kulevya .

"Tushirikiane kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya ambayo yameathiri zaidi vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa."

Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 28, 2023), alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Baraza la Maulid lililofanyika Kitaifa jijini Dodoma kwenye kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete.

“Matumizi ya dawa za kulevya yana madhara mengi kwa Taifa yakiwemo ya kiuchumi, kiafya na kimazingira pamoja na kuathiri uwezo wa mtu kufikiri”

Pia, Waziri Mkuu ametoa rai kwa viongozi wa dini waendelee kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili katika jamii na wawahamasishe waumini kushiriki katika shughuli zitakazowaongezea kipato.

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

 : Kundi la Wanasarakasi la Ramadhani Brothers kutoka Tanzania wamemaliza katika nafasi ya tano kwenye shindano maarufu ...
28/09/2023

: Kundi la Wanasarakasi la Ramadhani Brothers kutoka Tanzania wamemaliza katika nafasi ya tano kwenye shindano maarufu la Kusaka Vipaji la 'America's Got Talent' lililofanyika nchini Marekani.

Ramadhani walionesha Sanaa yao ya kushangaza mbele ya majaji wanne akiwemo Simon Cowell, Sofia Vergara, Heidi Klum na Howie Mandel ambapo Adrian Stoica ndiye aliyeibuka mshindi.

Kupitia ukurasa wao wa mitandao ya kijamii Ramadhani Brothers wameandika "Hatujapata kura za kutosha, tumekuwa watano katika shindano, na tunashukuru AGT kwa nafasi hii na watu wote waliotupigia kura, mapambano yanaendelea"

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

 :Mpenzi wa muigizaji na aliyewahi kushinda Taji la Miss Tanzania  , Whozu ameeleza kuwa anamshukuru Mungu kwenye maisha...
28/09/2023

:Mpenzi wa muigizaji na aliyewahi kushinda Taji la Miss Tanzania , Whozu ameeleza kuwa anamshukuru Mungu kwenye maisha yake kumpa mpenzi wake huyo moyo wake na anapendwa na kila mtu.

Ikiwa ni kumbukizi ya kuzaliwa kwa Wema Sepetu, ameandika

"K**a kuna kitu ambacho Namshukuru Mungu nimefanya vizuri kwenye Maisha yangu ni mimi kukupea Moyo wangu.

Your so special Wema na hata sio mimi tu Nakupenda Unapendwa na kila mtu Roho Yangu..🥰 I wish Everyday should be Your birthday.

Ufahamu tu Nakupenda sana Mpenzi wangu.. usishangae kesho Nikakupenda mara kumi ya leo coz najua lazima itakua ivyo tu.Sitoacha Kukupenda HAPPY BIRTHDAY ROHO YANGU I LOVE YOU SO MUCH
❤️

Kwa mapenzi Naombeni Mumwish Shunu Wangu Mzuri Mzuri happy birthday plz🥰🎂🎂🎂

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

DODOMA: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 28, 2023 amemuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Baraza la Mauli...
28/09/2023

DODOMA: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 28, 2023 amemuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Baraza la Maulid Kitaifa linalofanyika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

 : Naira Akijibu Kuhusu Video Ya Marehemu Mohbad Aliyorekodi Akisema Kwamba K**a Akifa Basi Yeye Na Watu Wa Label Yake (...
28/09/2023

: Naira Akijibu Kuhusu Video Ya Marehemu Mohbad Aliyorekodi Akisema Kwamba K**a Akifa Basi Yeye Na Watu Wa Label Yake (Marlian) Wak**atwe

“Unajua Mi Mwenyewe Sielewi, Nilihitaji Kumpa Msaada, Halafu Kwanza Sikuwepo Kabisa Nchini (Nigeria) Wakati Anarekodi Ile Video ….”

“Mohbad alirekodi ile Video akisema Kwamba K**a Akifa Basi Mimi Na Marlians Tuk**atwe!!. Na Niliporudi Nigeria Nilikutana Nae Na Kuongea Nae, Ambapo Nilimuuliza (Shida Ni Nini?) lakini Alijibu Kuwa Haelewi Chochote Na Kuniomba Msamaha” -

Lakini Pia Naira Marley Amesema Kwamba Mohbad alimuomba Msamaha Na Ushahidi Wa Mazungumzo Anao

“Nina Video Zinazoonesha Nikizungumza Na Mohbad, Wakati Nipo Marekani Mke Wake Alinipigia Simu Na Kuniambia Niongee Na Mohbad Chochote kile Kwasababu alikuwa anataka Kujiua, Kwahiyo Baada Ya Hapo Nilimpigia Na Nikawa Narekodi Mazungumzo Hayo Nikimuuliza Kwanini Anataka Ajiuwe Kwasababu Familia Yake haikuwa Sawa Kabisa (Walikuwa Stress), Nikamwambia Walau (Upate muda kidogo na Usijiue!Kwasababu ukijiua Saizi Unataka Watu Waseme Nini ?, Ikiwa Umerekodi Video Ukisema Kwamba K**a Ukifa Basi Watu Wote Wa Naira Marley Wak**atwe)

“Hivyo Kwasababu alikuwa anataka Kujiua, Nikampigia Ili Nijue Namsaidiaje, lakini alisema Kuwa mama na baba Yake Ndio Wanaelewa Shida Yake, Kwahiyo Nikamwambia Acha Nizungumze na Wazazi Wako K**a Hawatojali, Nilizungumza Nao Nikawaambia K**a Kuna Tatizo Basi akapatiwe matibabu Ila Mi sina Shida Nae Yoyote, Na Mwacheni Atulie, Asisumbuliwe na Kelele Wala Chochote kile” (SWIPE)

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

 :Baraza la Wawakilishi Nigeria limeitaka Tume ya Hakimiliki ya Nigeria (NCC) kubuni mbinu za kulinda haki za muziki za ...
27/09/2023

:Baraza la Wawakilishi Nigeria limeitaka Tume ya Hakimiliki ya Nigeria (NCC) kubuni mbinu za kulinda haki za muziki za marehemu Mohbad.

Azimio ambalo lilikuwa mwendelezo wa hoja ya muhimu na haraka kwa umma iliyowasilishwa na Babajimi Benson (APC, Lagos),
Bw Benson alisema wananchi wa Nigeria bado wanahamu kujua chanzo cha kifo cha nyota huyo.
Alieleza kuwa,Wawakilishi hao wanatakiwa kufuatilia uchunguzi unaoendelea kwa karibu ili kulinda haki za marehemu nyota huyo wa muziki kutoka Nigeria .

Ikumbukwe kwamba Staa wa Muziki kutoka Nchini Nigeria Naira Marley mapema jana alitoa tamko kukanusha kashfa za kuhusika na kifo cha aliekuwa Msanii wake Marehemu Mohbad .

Marley alisema hivi karibuni anampango wa kurudi Nchini humo kwa ajili ya kulisaidia jeshi la Polisi kuchunguza kifo cha msanii huyo.

Mohbad, 27, alifariki tarehe 12 Septemba na kuzikwa siku iliyofuata huko Ikorodu, Jimbo la Lagos.

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa   tunaungana na Waislamu duniani kote kwenye kusheherekea sikukuu ya Maulid.
27/09/2023

Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa tunaungana na Waislamu duniani kote kwenye kusheherekea sikukuu ya Maulid.

  Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameuomba Mfuko wa Maendeleo wa Sweden (SWEDFUND) kuweka kipaumbele cha ku...
27/09/2023

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameuomba Mfuko wa Maendeleo wa Sweden (SWEDFUND) kuweka kipaumbele cha kuisaidia Tanzania kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji ili kukuza ajira na uchumi wa nchi ikiwa ni kutekeleza dhamira ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa haraka.

Dkt. Mwigulu ametoa rai hiyo mjini Stockholm, Sweden, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Miradi wa SWEDFUND, Stefan Falk, ambapo walijadili masuala mtambuka ya ushirikiano kati ya Tanzania na mfuko huo.

Alisema kuwa sekta za uzalishaji ikiwemo kilimo, mifugo, uvuvi, utalii na sekta ya madini, zinaajiri watanzania wengi hususan vijana ambapo serikali imeamua kuelekeza rasilimali kubwa kupitia bajeti na program mbalimbali kukuza sekta hizo.

TANGAZA BIASHARA YAKO NA SWAHILIFORUMS: TUCHEKI WHATSAPP 0712 058 619 AU 0766 081 920.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Swahili Forums posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Swahili Forums:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share