Sports Online

Sports Online Karibu kwenye ulimwengu wa burudani ya michezo! Tunakuletea habari, matokeo, na matukio moto kutoka ndani na nje ya uwanja. Usipitwe na chochote!

17/01/2026

Awesu akirudi kiwango chake atabaki Simba Sc

🔔 Taarifa kutoka AFCON 2025Mwamuzi kutoka Mali, Boubou Traoré, anaripotiwa kuondolewa kwenye mashindano yote yaliyobaki ...
13/01/2026

🔔 Taarifa kutoka AFCON 2025

Mwamuzi kutoka Mali, Boubou Traoré, anaripotiwa kuondolewa kwenye mashindano yote yaliyobaki ya AFCON 2025, hivyo hatachezesha mechi nyingine yoyote.

Pia, mwamuzi wa Cameroon, Abdou Abdel Mefire, inaelezwa kuwa hatatumika tena kwenye AFCON 2025.
Haya ni maamuzi makubwa yaliyofanywa nyuma ya pazia, huku CAF ikiendelea kupitia na kuchunguza viwango vya uamuzi (refereeing standards) kwenye mashindano hayo.

Kwa ufupi waamuzi hao wameondolewa kwa sababu ya utendaji/maamuzi yao, na CAF inafanya marekebisho ili kuboresha haki ya mechi.

Ujumbe wa Diarra"Ndugu zangu raia wa Mali 🇲🇱mashabiki wapendwa, wafuasi,ndugu na dada wa bara la Afrika,Kwa hisia nyingi...
11/01/2026

Ujumbe wa Diarra

"Ndugu zangu raia wa Mali 🇲🇱
mashabiki wapendwa, wafuasi,
ndugu na dada wa bara la Afrika,
Kwa hisia nyingi na uwajibikaji mkubwa nachukua nafasi hii kuzungumza baada ya kushindwa kwetu dhidi ya Senegal katika michezo ya kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Morocco 2025.

Kwa niaba ya wachezaji wenzangu na kwa jina langu binafsi, napenda kutoa pole za dhati kwa maumivu na masikitiko yaliyosikika. Tunajua jinsi mchezo huu ulivyokuwa na umuhimu mkubwa kwa wananchi wa Mali na kwa wote wanaoamini timu hii.

Lakini zaidi ya matokeo, napenda kusema asante.
Asante kwa wananchi wa Mali kwa sapoti yenu isiyoyumba, ujumbe wenu wa motisha, ujasiri na faraja.
Asante kwa mashabiki wetu na wafuasi waliokuwepo viwanjani, mbele ya skrini na kwenye mitandao ya kijamii.

Asante pia kwa bara zima la Afrika kwa heshima, mshikamano na moyo wa michezo mliouonyesha.
Sapoti yenu ni heshima kwetu na pia ni jukumu. Inatupa nguvu ya kusimama tena, kujifunza kutokana na jaribio hili na kuendelea kufanya kazi kwa unyenyekevu, dhamira na fahari kutetea rangi zetu.

AFCON Morocco 2025 inaendelea, na soka la Afrika linaendelea kukua. Kwa upande wetu, tutaendelea kuwa na mshikamano, umoja na kuangalia mbele.
Mungu aibariki Mali 🇲🇱
Asanteni kwa imani yenu 🤍."

Djigui Diarra
Mchezaji wa Kimataifa wa Mali 🇲🇱

11/01/2026

Tayari Okello ni mwananchi, Hersi said hana utani

11/01/2026

Wachambuzi wanavyogombania kuichambua Simba Sc kipindi hiki 😕

10/01/2026

Huyu Barjaber hata Namungo haanzi kwa kiwango chake.

10/01/2026

Hii timu wanayoandaa Yanga ni balaa mjini

10/01/2026

Simba wanazidiwa mikakati na Rais wa Yanga

10/01/2026

Bacca kawa maarufu dunia nzima kwa kumkaba Osimen

10/01/2026

Mimi tayari ni Mtanzania, nipo hapa miaka mitatu

09/01/2026

Sikiliza mpaka mwisho tatizo la Simba lilipo

09/01/2026

Wachezaji hawaumii na matokeo ya Simba Sc

Address

Mazinde
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sports Online posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Sports Online:

Share