The Long File Tv

The Long File Tv Je Umewahi kuteseka kufuatilia Mambo Mbalimbali kwa Lugha ya Kigeni? Kama ndio usiteseke tena LIKE - Karibu kwenye The LONG FILE TV

19/07/2025

MBEYA - CHUNYA - MAKONGOLOSI BARABARA ILIYO KATIKA MWINUKO WA JUU ZAIDI TANZANIA

Barabara ya Mbeya-Chunya Makongoros takriban kilomita 111 kutoka katikati mwa jiji la Mbeya.

Alama hii iko kwenye mwinuko wa mita 2,457 sawa na (futi 8,061) juu ya usawa wa bahari.

Eneo hili linatoa mandhari ya kuvutia ya Bonde la Ufa, ikijumuisha Ziwa Magadi na tambarare za Usangu.

Uendeshaji hadi hatua hii ni wa kupendeza, na barabara zenye vilima na miinuko mikali.

KARIBU THE LONG FILE TV YOUTUBE UPATE KUFAHAMU MENGI

https://youtu.be/f1eG8jD-U70?si=9hUKC1dVoz_01ajp

19/07/2025

MCHAKATO WA WATIA NIA CCM KUFAHAMIKA JULAI 28 MWAKA HUU

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa kikao cha K**ati Kuu kwa ajili ya kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu uteuzi wa watia nia wa ubunge na udiwani kitafanyika Julai 28, 2025.

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 19, 2025, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi, Amos Makala, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

18/07/2025
18/07/2025

UKIMYA WA FREEMAN MBOWE WAIBUKIA DODOMA , AELEZA HAYA KUHUSU DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

17/07/2025

HUMFREY HERSON POLEPOLE NI NANI KATIKA UWANJA WA SIASA ZA TANZANIA

Ndoto yake ilikuwa ni kuwa rubani, lakini bahati mbaya uwezo wa familia yake ukuweza kumudu gharama za masomo hayo hali iliyochangia kubadilisha ndoto hiyo.

Harakati za utetezi ndani ya jamii hususani vijana ndizo zilizomkuza Polepole na kumfikisha katika hatua kubwa za kisiasa ndani na nje ya nchi.

Je nyota yake ilianza kung”ara wakati gani? https://youtu.be/A9FqpbieDBQ?si=9Yo58KQtNn4hKZlu

17/07/2025

MAAJABU YA NCHI AMBAZO JUA HALIZAMI ,LINAWAKA MPAKA USIKU WA MANANE/ NINI SABABU FUATILIA.

Utaratibu wetu wa maisha unazunguka saa 24 kwa siku, na saa 12 za jua, na saa zingine zilizobakia ni wakati wa usiku.

Lakini, je! Ulijua kwamba kuna maeneo ulimwenguni ambapo jua halizami kwa kwa zaidi ya siku 70?

Endelea kufuatilia ..https://youtu.be/BZ6i-FSEHmU?si=xlWY8uZ_DwrKEWhf

16/07/2025

SEHEMU PEKEE ILIYOKARIBU NA MWEZI DUNIANI /IKO NCHINI ECUADOR BARA LA AMERIKA KUSINI

MLIMA Chimborazo ulioko katika nchi ya ECUADOR ndiyo sehemu pekee duniani iliyo karibu zaidi na mwezi kwa sababu ya dunia kupanuka kidogo kwenye ikweta, ambayo inaitwa kitaalamu inaitwa "oblate spheroid".

Kuvimba huku kunamaanisha ya kuwa watu wanaosimama kwenye ikweta wako karibu na anga ya juu kuliko watu waliosimama mahali pengine duniani

Tofauti na hapo ili kufikia Mwezi utalazimika kuzipita wastani wa maili 238,855 sawa na (kilomita 384,400).

16/07/2025

KIMONDO VIPANDE VYA MIAMBA VINAVYOANGUKA KUTOKA ANGA LA JUU HADI KWENYE USO WA DUNIA

Mwanzo wa Kimondo: Kimondo huanzia katika anga-nje k**a sehemu ya asteroidi au nyotamkia. Asteroidi ni miamba mikubwa inayozunguka Jua, wakati nyotamkia ni vitu vya barafu na vumbi vinavyosafiri kwenye obiti zao.

Uvunjikaji: Wakati asteroidi inapoathirika na mgongano mwingine au nguvu za graviti, inaweza kuvunjika na kutoa vipande vidogo. Vipande hivi vidogo vinaweza kuwa vimondo.… See more

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Long File Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share