
19/07/2025
KILA MTU ANAISHABIKIA* *CCM* *KWA STYLE YAKE*
Kitu muhimu wananchi wanachopaswa kufahamu ni kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi; kelele, mivutano na shutuma zisizo na maana ni sehemu ya maisha.
Hakika katika jicho la tatu; jicho la kutulia na kutumia akili nyingi - ni wazi Upizani dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umezidi kuzikwa.
Leo wapizani hawapigi tena kelele za No Reforms No Election, leo wapizani wameungana na kushangilia kelele za Balozi Kada wa CCM Ndugu Humphrey Polepole, anayelia na Chama chake Chama Cha Mapinduzi. Anacholilia yeye mwenyewe ndiye anayejua.
Ukimsiliza Ndg. Polepole halili ujenzi wa Taifa hili, haangazii miradi iliyokamilishwa na inayoendelea, haangazii uchumi na uboreshwaji wa miundombinu mbalimbali, hatuambii juu ya elimu bure na mikopo ya elimu ya juu kufika kwa wakati kwa wanafunzi.
Ndugu Polepole ameridhika na utendeji kazi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Jemedari Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ngazi za kitaifa, bila shaka hana kesi ya maendelo bali ana kesi ya yanayoendelea ndani ya chama chake.
Watu wa 'Reform' pasipo kujigundua wameingia kwenye mtego na kushangilia pale Ndugu Polepole anapolia kuimarisha siasa za ndani ya CCM, kuimarisha maadili ya CCM na yale yaliyo ndani ya CCM anayoona yanahitaji kurekebishwa. Pasipo kujitambua 'Reform' wanaungana kuijenga CCM; hii ndio nguvu ya CCM.
Kelele zote zimekufa za Mahakamani na 'Reform' kelele utakazozisikia sasa ni CCM. Hii pia ukiangalia kwa Ndugu Askofu Gwajima utaiona upepo wa kelele ni wa kichama na si kitaifa. Leo hii wote tunapambana na Katiba ya CCM, hakika Wahenga hawakukosea waliposema CCM BABA LAO, wamefanikiwa KUZIMA ZOTE NA KUWASHA MOSHI WAKIJANI masikio macho harakati zote zinaangazia CHAMA TAWALA WAKIELEKEA OKTOBA KUTIKI ✅.
The Diplomat_Tz 🇹🇿 .
🇹🇿
🧭
🔨