Muvi za kijanja

Muvi za kijanja Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Muvi za kijanja, Digital creator, Dar es Salaam.

👉Kwenye movie ya SHELTER mtaalam wetu JASON alikutana na hiki chuma Cha kazi,zikapigwa,zikapigwa tena...Ikabidi wote wap...
07/03/2026

👉Kwenye movie ya SHELTER mtaalam wetu JASON alikutana na hiki chuma Cha kazi,zikapigwa,zikapigwa tena...

Ikabidi wote wapumzike kila Mmoja akijipanga kwa round nyingine huku akijiuliza napigana na mtu au jini 😂😂

Pambano langu pendwa kwenye mzigo WA SHELTER...

SCOTT akiwa muuwaji na Mdunguaji Wa masafa marefu anaamua kuachana na kazi hiyo baada ya kumiss target na kumuuwa mtu as...
02/06/2025

SCOTT akiwa muuwaji na Mdunguaji Wa masafa marefu anaamua kuachana na kazi hiyo baada ya kumiss target na kumuuwa mtu asiye na hatia...hataki tena kupelekeshwa na maboss zake

Kiroho upande bibie TAMARA ambae ndio boss wake SCOTT anaridhia maamuzi ya kijana wake ...japo ina muuma maana si rahisi kupatikana Wa kuziba pengo lake..lakini sa atafanyaje

Hata partner na msoma ramani aliyekuwa akipiga matukio ya udunguaji na mission mbalimbali pamoja na SCOTT nae pia maamuzi ya mwamba yanamuumiza kuhisi atabaki mpweke kwa kuimiss kampan ya SCOTT

Basi SCOTT na yule partner wake Wa kazi wanakodiwa hotel moja safi ya gharama na huyo boss wao huku wakipewa starehe zote ikiwemo wanawake kwaajili ya kuenjoy nao usiku huo k**a kuwaaga rasmi kundini

Wao wakijua boss wao kawakarimu kumbe ana mpango Wa kishenzi dhidi yao...

SCOTT aliushtukia mchezo baada ya kuona mapazia yapo wazi haitoshi wahudumu wanaacha madirisha ya chumba Cha hotel waliyochukua wazi

Akiwa anahoji kulikoni ghafla risasi zikaanza kumiminwa eneo hilo walilofadhiliwa...mlengaji haijulikani anafanya yote hayo akiwa upande gani lakini ndani ya sekunde chache wahudumu na wanawake walioenda kutoa starehe walikuwa chali damu zikimwagika

Kumbe TAMARA baada ya kupokea taarifa za SCOTT kuasi kundi hakuridhia na kuamua kumpoteza kwa kutafuta Wadunguani wengine mahiri kumkomoa kwamba tumepata zaidi yenu

Shida ni namna ya kujikomboa kutoka hotelin hapo maana tayali Partner wake nae ameshatwanga risasi anaugulia..

Hata alipojaribu kuwasiliana na boss wake kuomba back up ndio akachoka kabisa baada ya boss wao kuthibitisha kwamba yote hayo anafanya yeye na kuwaambia hawatoki hapo wakiwa salama

Kwahiyo hapo nguvu na akili zao ndio zitakazowakomboa... Mzigo tayali tunao Whatsapp 0742932384 bei sh 1000 iliyo tafsiriwa pia ipo..link ya kutupata Whatsapp ipo sehemu ya coment..

👉mzigo unahusu kampuni Moja inayomilikiwa na nyamela mmoja kwa jina la Mr blutKampuni yake inaandamwa na skendo za mauwa...
02/10/2024

👉mzigo unahusu kampuni Moja inayomilikiwa na nyamela mmoja kwa jina la Mr blut

Kampuni yake inaandamwa na skendo za mauwaji ya wafanyakazi wake pindi wanapokaribia kustaafu,Lakini hamna ushahidi wa kumfunga

Hufanya mauwaji hayo ili kiinua mgongo Cha wafanyakazi hao kibaki mikononi mwake kwa maslahi yake mwenyewe

Kazi hii ya mauwaji na kupoteza ushahidi wa mauwaji ilikuwa ikifanywa na mtu wake Mzee Duncan almaarufu black kaiser

Baada ya Dancan kufanya kazi hiyo ya mauwaji kwa miaka mingi na yeye pia muda wake wa kustaafu ukawadia na yeye pia wakapanga kumletea Ile Ile michezo

Hapa ndipo unatimia ule msemo usemao ukiuwa kwa upanga na wewe utakufa kwa upanga

Zilipobaki siku 14 Ili astaafu alipewa mission ya mwisho,Wakiwa na dhumuni kwamba baada ya kufanya mission hiyo na yeye wamletee huo huo mchezo waliofanyiwa wafanyakazi wengine

Hivyo kikaagizwa kikosi kipya Cha wauwaji wachanga ili wakadeal na kumpoteza Mzee Duncan

Bila kujua kwamba kakwepa mishale mingi kipindi cha ujana wake mpaka kufikia umri huo wa kustaafu,hivyo ana mafunzo na mbinu nyingi za kudeal na hao watoto walioanza kazi majuzi

Hapo ndipo alienda kuwaonyesha yeye ni mafia zaidi yao,uzee wake si kizuizi Cha yeye kushindwa kuwapelekea moto na kuwachezesha sindimba.✍️

Ni single movie,ipo iliyo tafsiriwa na ambayo haijatafsiriwa,Bei sh 1000 tunatuma Whatsapp na telegram 0742932384,pia tuna group la movie na season telegram, link ipo sehem ya comment.👇

Michael Dudikoff alipitia njia fupi na thabiti kutoka kuwa mtu asiyejulikana hadi kuwa nyota wa filamu za mapigano. Akiw...
19/09/2024

Michael Dudikoff alipitia njia fupi na thabiti kutoka kuwa mtu asiyejulikana hadi kuwa nyota wa filamu za mapigano. Akiwa anafanya kazi ya kuhudumia wateja kwenye mgahawa, aligunduliwa na mhariri wa jarida la mitindo la Esquire, Max Evans, ambaye alimshauri kujaribu kuwa mwanamitindo.

Maonesho ya mitindo ya mavazi yalimpeleka kwenye matangazo ya picha, ambayo hatimaye yalifungua mlango wa uigizaji kupitia matangazo ya kibiashara kwa wateja wakubwa k**a Coppertone na Stridex.

Hatua iliyofuata ilikuwa uigizaji kwenye televisheni; alionekana kwenye kipindi cha vichekesho kiitwacho Happy Days.

Baada ya kucheza nafasi ndogo kwenye vipindi vya televisheni (k**a vichekesho vya NBC Gimme a Break!) na filamu (k**a filamu ya kisayansi ya TRON), Dudikoff alipata nafasi ya kuwa mhusika mkuu ambayo anajulikana zaidi, Pvt. Joe Armstrong, katika filamu ya American Ninja.

Mbali hili tambala alitamba na filamu k**a Avenging Force, Platoon Leader na River of Death.

Dudikoff amemuoa Belle Dudikoff, na wanandoa hawa wana watoto wawili pamoja. Licha ya umaarufu wake, Dudikoff ameweza kudumisha maisha ya familia yenye usawa na anabaki kujitolea kwao.

Baada ya kuwa na kazi zenye mafanikio katika tasnia ya burudani, Dudikoff alitangaza kustaafu kutoka kwenye uigizaji.

Hivi Bado mnaamini bongo movie inazinguwa vijana wadogo Sasa wanaibeba hivyo ,hivyo inabidi tumsahau kanumba maisha ya b...
19/09/2024

Hivi Bado mnaamini bongo movie inazinguwa vijana wadogo Sasa wanaibeba hivyo ,hivyo inabidi tumsahau kanumba maisha ya bongo movie yasonge RK Mzee wa wrong house na huku sasa anaichanganya sukari ndani ya SIRI YA HUBA🔥🔥

14/09/2024

👉Katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 75 Mzee Charles Abernathy aliwaita watoto wake wote wanne ili ajumuike nao katika siku yake hiyo muhimu

Wanae wote waliitikia mualiko na kufika katika jengo la baba yao la kifahari aliyekuwa kajaaliwa Kuwa na utajiri mkubwa,Lakini miongoni mwa kijana wake kwa jina la Grew alifika na mkewe Hannah

Jambo la Mwanae kufika na mkewe halikuwafurahisha baadhi ya ndugu maana mualiko ulikuwa unawahusu watoto tu,maana Baba yao alikuwa na agenda ya sili dhidi Yao

Baada ya muda kidogo baba yao aliwaambia kwamba kawaita nyumbani kwake siku hiyo kwa sababu usiku huo anapaswa kuuwawa,hivyo basi alimpa bibie Hannah nafasi ya kuondoka ili msala huo wakabiliane nao ndugu tu,Lakini bibie akagoma🤔

Hivyo basi lengo la wito huo kwa wanae ni kuhakikiaha kwamba usiku huo anapaswa kuuwawa hivyo wanapaswa wafanye juu chini wazuie baba yao asiuwawe 😱

Watoto walidhani masihara,baadae akawaambia kwamba wakifanikiwa kumlinda dhidi ya watu wanaotaka kumuuwa usiku huo basi atawalithisha mali zake zote😍

Na iwapo wakishindwa kumlinda baba yao dhidi ya kifo basi utajiri wake wote utagawiwa katika vituo vya misaada ikiwemo vituo vya watoto yatima

kuonyesha kwamba haleti masihara alimuamuru mtu wake wa karibu afunge milango yote kwa nje Kisha wasubiri kizaa zaa kitakachokuja usiku

Eeh bhana kumbe utajiri wote aliokuwa nao Mzee aliupata kwa njia za haramu za kishirikina(k**a freemason) na wanae hawakujua na mkataba wake na mashetani ilikuwa kwamba akifikisha miaka 75 basi ndio siku yake ya mwisho😔

kwahiyo Mzee akaona si mbaya kizaa zaa hicho kikimkuta yeye na wanae usiku huo wa birthday yake maana wote wamekula huo utajiri haramu🤣oyaah ni bonge Moja la horror muvi,humo ndani Kuna kizaa zaa Cha maana bibie Hannah alijuta kuingilia mambo ya kifamilia🤣

Mzigo ninao Whatsapp na telegram 0742932384, iliyo tafsiriwa na ambayo haijatafsiriwa Bei sh 1000.✍️

Digital creator

14/09/2024

👉Chuoni na mashuleni huwa Kuna Ile pisi kali ambayo Kila mwanaume rijali anatamani Kuwa nayo,hichi ndicho kilichomkuta mwamba Nick baada ya kumuelewa mwanachuo mwenzie bibie Christina

Shida ni kwamba bibie Christina Yupo matawi ya juu hapo chuoni kuanzia swaga,pia ni mtoto wa kishua na pesa ipo,Lakini mtaalam wetu Nick yeye swaga ziro kuanzia tembea yake,ongea yake pia kutupia code kali hajui

Hivyo basi hali hiyo ilimnyima ujasiri Nick na wanachuo wengine wa kiume wenye swaga ziro kushusha nyavu kwa bibie

Kuna siku bibie Christina alichukua gari ya mama yake aliyekuwa kasafiri na kwenda kupiga nayo misele hadi maeneo ya chuoni kwao,bahati mbaya alipata ajali,hivyo Ili kuuwa Soo pindi mama yake atakaporudi alitaka kufix hitilafu iliyojitikeza katika gari hiyo

Hivyo ikabidi atafute mafundi chuoni hapo maana kulikuwa na kitengo Cha ufundi magari,bad News akaambiwa gari lake ili liwe sawa matengenezo yatagharimu muda wa wiki mbili,wakati bibie anataka zoezi hilo likamilike kwa muda wa siku chache maana mama yake karibu anarudi

Good news kwenye kitengo hicho Cha garage alikuwepo pia kijana asiye na swaga Nick ,akaona hiyo ndio fursa ya Kuwa karibu na bibie,hivyo akamwambia bibie gari lake atalitengeneza kabla ya hizo wiki mbili,lakini kwa sharti Moja tu,waigize k**a Wapenzi chuoni hapo kwa muda wa wiki mbili

Bibie akaona fresh tu,Si kuigiza tu bila kurusha roho hamna Shida, ila kutokana na muonekano wa Nick kuanzia uvaaji,mtindo wa nywele na ongea yake bibie aliona jamaa anamuaibisha chuoni hapo

Hivyo akaanza kumbadirisha kuanzia kwa kumtafutia pamba kali,kuchange mtindo wa nywele n.k,Ili wafanane,eeh bhana baada ya bibie kumgharamia mshkaji nyota kali na uhandsome wa jamaa uliofichika awali ukaanza kuonekana chuoni hapo

Ghafla akawa staa kuliko bibie,madem wa chuoni hapo waliomuona k**a rofa wakawa wanang'ang'ania Kuwa nae,too bad hata bibie Christina alijikuta tayari moyo wake umeangukia kwa Nick ambaye hivi Sasa Kawa staa kuliko bibie,na hana habari tena na bibie Christina

Bibie akawa hazingatiwi tena too bad Nick akaanza kutoka na pisi nyingine akiwemo rafiki wa karibu wa christine wakati huo bibie Christina alikuwa ameanza kumpenda Nick kikweli kweli si maigizo tena🤔mapenzi hayajaribiwi🤣

Ni single movie, tunayo Whatsapp na telegram 0742932384, ipo iliyo tafsiriwa na ambayo haijatafsiriwa Bei sh 1000.✍️

Digital creator

Movie inaañza nchini india mwana anaenjoy maisha ya kijijini ya amani na familia yake yani mama yake pamoja na mkewe lak...
13/09/2024

Movie inaañza nchini india mwana anaenjoy maisha ya kijijini ya amani na familia yake yani mama yake pamoja na mkewe lakini ataingia tamaa kwenda kutafuta maisha nje ya india na kudondokea nchini saudia ili akafanye kazi na pesa atume nyumbani sasa movie ndo inaanza je atafanikiwa kufika saudia ?

NB Wale wanao penda kuangalia movie uku wanafuta machozi😂 ndio kazi yenu moja ya movie kali za drama za asia za mwaka2024🔥

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Muvi za kijanja posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share