21/09/2025
Mgombea ubunge wa Arusha Mjini kupitia (CCM) Paul Makonda, amekiri kuwahi kulishwa sumu hali iliyomsababishia kulazwa hospitalini na kutoonekana hadharani.
Makonda amesema hayo leo Jumapili, Septemba 21, 2025, wakati wa ibada katika Kanisa la Mbingu Duniani lililopo Njiro - Arusha, akisema si mara yake ya kwanza kulishwa sumu na kwamba amenusurika kifo mara kadhaa.