EXL Media

EXL Media Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from EXL Media, Media/News Company, Mbezi beach kwa Zena, Block K, Plot No 5, Dar es Salaam.

MKUU wa mkoa wa Geita, Martine Shigela amekemea tabia ya waajiri hususani maofisa utumishi wa ofisi za umma kukwamisha w...
04/05/2026

MKUU wa mkoa wa Geita, Martine Shigela amekemea tabia ya waajiri hususani maofisa utumishi wa ofisi za umma kukwamisha watumishi kubadilisha kada na kupandishwa madaraja.

Shigela ametoa kauli hiyo katika maazimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi, 2026) ambayo kimkoa yalifanyika katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro wilayani Geita.

Amesema kazi ya upandishaji madaraja ni endelevu na hivo maofisa utumishi mara kwa mara wanapaswa kupeleka taarifa za watumishi wanaohitaji kupandishwa madaraja kwa hatua zaidi.

“Nielekeze na kumkumbusha RAS (Katibu Tawala wa Mkoa) jambo hili tuendelee kulifuatilia kwa ukaribu, ili kila mfanyakazi anayestahili kupandishwa daraja aweze kupandishwa”, amesema.

Shigela amesema serikali haitakubali kuona watumishi wa umma waliojiendeleza na wana sifa za kubadili kada ama kupadishwa daraja wanakwamishwa kwa sababu za mtu binafsi.

“Nisisiitize waajiri, tuwape fursa wafanyakazi wetu, wabadilishe kada, kwani inawapa motisha ya kuongeza ari ya kazi na kujituma ili kuongeza juhudi za maendeleo kwenye mkoa wetu.

“Niwasihi na kuwatia moyo watumishi, wanaotamani kubadilisha kada, wajiendeleze kwenye kada ambayo wanataka Kwenda, na kuwasilisha maombi yao kwenye taasisi zinazohusika” amesema.

Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu imefanikiwa kuwapandisha madaraja watumishi 15,553 tangu ilipoingia madarakani mpaka kufikia Desemba mwaka 2025.

Amesema pia jumla ya wafanyakazi 1,194 wamebadilishiwa kada baada ya kujiendeleza kielimu na wengine kuomba kubadili kada ya utumishi kutokana na kukidhi matakwa ya kitaaluma.

MIRADI ya maendeleo 7 yenye thamani ya Sh bilioni 2 iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani inatarajiwa kupitiwa na Mwenge ...
04/05/2026

MIRADI ya maendeleo 7 yenye thamani ya Sh bilioni 2 iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru 2026.

Mwenge huo umepokelewa leo Mei 3, 2026 mkoani Mtwara katika viwanja vya Shule ya Msingi Mpapura kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ukitokea mkoani Lindi.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya amesema Mwenge ukiwa katika manispaa hiyo utaweka mawe ya msingi miradi miwili, utaona na kukagua miradi mitatu pamoja na kuzindua miradi miwili.

Miongoni mwa miradi ya maendeleo itakayopitiwa manispaa ikiwemo kikundi cha vijana cha uvuvi cha mikindani fishers, ujenzi wa kisima cha maji mtaa wa namayanga.

Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari shangani, ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa mji mwema, ufunguzi wa barabara ya mtaa-Namayanga -Naliendele ya kilometa 4.3 na mingine huku ukikimbizwa umbali wa kilometa 106.6.

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwango’nda amewaagiza wataalamu wa miradi wa manispaa hiyo kuwa vifaa vya kupimia miradi viwepo kwenye maeneo yote ya miradi ambayo Mwenge utapitia.

Chama Cha Wakaguzi wa Ndani (IIA Tanzania) kimesema miongoni mwa changamoto wanazokumbana katika ukaguzi ni viatarishi j...
04/05/2026

Chama Cha Wakaguzi wa Ndani (IIA Tanzania) kimesema miongoni mwa changamoto wanazokumbana katika ukaguzi ni viatarishi jambo linalopelekea kushuka kwa ufanisi katika taasisi wanapofanya ukaguzi.

Rais wa chama hicho, Jonathan Ngoma amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ufunguzi wa mwezi wa uhamasishaji wa ukaguzi wa ndani ambapo utadumu kwa mwezi huu mzima na kusema kuwa itakuwa ni kwa mikoa yote nchini.

Jonathani amesema miongoni mwa mambo wanayoyazingatia kwenye ukaguzi ni kuhakikisha viatarishi wanavizuia vyema ili kuweze kuwa na tija kwa taifa pamoja na jamii kwa ujumla.

“Sisi tunakuja kuangalia mpepewa ‘project’ hii sisi tunakuja kuangalia je mmefanya vitu vinavyotakiwa na miongozo inafatwa kwa hiyo kazi yetu kubwa ni kwenda kwa Bodi na kusema kwamba katika hizi project zizopangwa ni moja mbili Tatu vingapi vimefanyika vizuri kwa sababu tunaripoti vitu vizuri na vibaya ambavyo hujafika lakini tunatoa maoni.

‘Tunakaa pamoja Nini tuone turekebishe baada ya apo tunakaa na bodi tumeona hichi na tumekubaliana na management watafanya hivi hivyo watu wote tunategemeana katika utekelezaji majukumu,”amesema Jonathan.

WAZIRI wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amewaagiza watumishi wa afya nchini kuwa bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27 inatakiwa ...
04/05/2026

WAZIRI wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amewaagiza watumishi wa afya nchini kuwa bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27 inatakiwa kuonyesha mwelekeo wa taifa utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.

Mchengerwa amesema hayo leo Mei 3, 2026 wakati wa uzinduzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya jijini Mwanza.

“Katika bajeti ya 2026/2027, vipaumbele vyetu lazima vionyeshe mwelekeo wa Taifa. Kwanza, lazima tujiandae kikamilifu kwa utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote. Hili si suala la kadi pekee; ni suala la uwezo wa mfumo. Lazima miundombinu iwe tayari,” amesema Mchengerwa.

Amesema ni lazima mifumo ya TEHAMA iwe imara pia dawa zipatikane na rasilimali watu wawepo pamoja na vifaa vya kufanyia kazi. Ameagiza mkazo katika uzalishaji wa ndani wa bidhaa za afya.

“Taifa lisilojenga uwezo wa kuzalisha dawa na vifaa tiba vyake, daima litakuwa mateka wa bei, usafirishaji na misukosuko ya dunia. Kwa hiyo, ununuzi kupitia MSD na mifumo yetu ya manunuzi lazima uanze kutoa msukumo wa kimkakati kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini, bila kushusha ubora,” ameongeza.

Alisema katika mwaka wa fedha 2025/2026, wamefanikiwa kupiga hatua muhimu ikiwemo kuongeza upatikanaji wa dawa muhimu kufikia wastani wa asilimia 73 kwa mwezi Februari, 2026.

“Tumeendelea kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kupitia uwekezaji katika vituo vya afya, hospitali za wilaya, vifaa tiba na rasilimali watu. Haya ni mafanikio ya pamoja. ” amesema.

Ametoa wito kwa kila mtumishi, kuanzia Makao Makuu hadi hospitali za rufaa, kutoka idara hadi kituo cha afya, kuhakikisha wanatoa huduma kwa weledi na huruma.

“Hatutavumilia ucheleweshaji wa huduma usio na sababu. Hatutavumilia upendeleo unaodhalilisha haki ya mwananchi.

Alisema kuna malalamiko katika sehemu mbalimbali kuhusu matumizi mabaya ya madaraka, vitisho, unyanyasaji na tabia za
kuwadhalilisha watumishi wa ngazi za chini.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dk James Mataragio ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Mkondo...
22/04/2026

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dk James Mataragio ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa kusimamia kwa mafanikio utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa visima vya gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay, mkoani Mtwara.
Dr Mataragio ametoa pongezi hizo leo Jumanne, Aprili 21, 2026, mara baada ya kupokea maelezo ya utekelezaji wa mradi huo alipotembelea banda la PURA katika Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.
Akitoa taarifa kwa Mataragio, Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau kutoka PURA, Charles Nyangi alieleza kuwa tayari kisima kimoja kati ya vitatu kimeshachimbwa na uchimbaji wa kisima cha pili unaendelea.
“Kupitia usimamizi wa PURA, uchimbaji wa kisima cha kwanza (MB5) umekamilika kwa wakati na mafanikio. Kisima hicho kimeshafanyiwa majaribio na kuingizwa katika uzalishaji ambapo kina uwezo wa kuzalisha wastani wa futi za ujazo milioni 40 kwa siku,”aliongeza.
Kwa mujibu wa katibu mkuu, kiasi hicho kimeongeza uzalishaji wa gesi asilia kutoka Kitalu cha Mnazi Bay kutoka wastani wa futi za ujazo milioni 90 kwa siku hadi kufikia wastani wa futi za ujazo milioni 130 kwa siku.
Alielezea pia kuwa PURA imeendelea na usimamizi wa uchimbaji wa kisima cha pili (MS-2) ambapo kazi inaendelea vizuri ambapo hadi kufikia Aprili 20, 2026, zaidi ya mita 1400 zilikuwa zimeshachimwa.
Kwa upande mwingine Dk Mataragio alieleza kuridhishwa na utendaji wa mamkala hiyo kwa usimalizi na udhibiti makini wa miradi ya utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia ikiwemo mradi wa uchimbaji wa gesi asilia unaoendelea Mnazi Bay.

Amesema kuwa PURA imeandika historia mpya katika uzalishaji wa gesi asilia nchini ambapo baada ya miaka 10 nchi imeshuhudia uchimbaji wa visima vipya vya gesi asilia.

Wanasheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wanapatiwa mafunzo maalumu ya usuluhishi yaliyoan...
22/04/2026

Wanasheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wanapatiwa mafunzo maalumu ya usuluhishi yaliyoandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa lengo la kuwajengea uwezo, kuwapatia mbinu na maarifa ya kushughulikia migogoro na malalamiko ya wateja yanayowasilishwa katika mamlaka hiyo ikiwa ni njia mbadala ya utatuzi wa migogoro.

Mafunzo hayo ya wiki moja yameanza leo April 20, 2026 Chuoni Lushoto na yamefunguliwa na Mkurugenzi wa Mafunzo ya Kimahakama na Elimu Endelevu IJA, Dk. Patricia Kisinda kwa niaba ya Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Dk Paul F. Kihwelo.

Akizungumza wakati wa ufunguz, Dk. Kisinda amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea washiriki uwezo, maarifa na mbinu za kutatua migogoro na malalamiko kwa njia mbadala za utatuzi wa migogoro, hususani usuluhishi ili kupunguza utegemezi wa mashauri Mahakamani ambayo mara nyingi huchukua muda mrefu na kuathiri shughuli za kiuchumi.

Dk Kisinda amebainisha kuwa IJA ina jukumu la msingi la kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya haki kupitia mafunzo endelevu yanayoendana na mahitaji ya sasa ya mfumo wa haki.

Katika kuhakikisha waathirika wa ukatili wa kingono wanakuwa na mazingira rafiki wakati wa uendeshwaji wa mashauri Mahak...
22/04/2026

Katika kuhakikisha waathirika wa ukatili wa kingono wanakuwa na mazingira rafiki wakati wa uendeshwaji wa mashauri Mahakamani, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Irish Rule of Law International (IRLI) kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania kimeendesha mafunzo maalumu kwa Mahakimu, Waendesha Mashtaka na Maafisa Ustawi kwa lengo la kuwajengea uwezo na mbinu bora za kushughulikia mashauri hayo.

Mafunzo hayo, ambayo ni awamu ya sita na yanatarajiwa kuchukua siku tatu, yameanza leo April 20, 2026 na yanafanyika katika wilaya ya Bukoba na Sumbawangu huku washiriki wakitokea mikoa ya Kagera, Geita, Rukwa na Katavi.

Akifungua mafunzo hayo mjini Bukoba, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda hiyo ya Bukoba. Immaculata Banzi amewasihi washiriki kuwa makini wanapokuwa wanashughulikia mashauri ya ukatili wa kingono kwa kuwa ukatili huo huacha majeraha makubwa ya kihisia na kisaikolojia.

“Unyanyasaji wa kingono na ukatili wa kijinsia huacha majeraha makubwa ya kihisia na kisaikolojia kwa waathirika,” alisema Banzi.

Ameongeza: “Tusipokuwa waangalifu, mchakato wa kisheria wenyewe unaweza kuwaongezea maumivu manusura wa ukatili wa kingono. Hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha wanajisikia vizuri, wanasikilizwa na kuheshimiwa.”

Kwa upande wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Frederick Kapela Manyanda amesema kuwa manusura wa ukatili wa kingono wanaweza kuumizwa tena wanapokabiliwa na maswali yasiyo na staha, mazingira yasioyo salama wakati wa mashauri Mahakamani.

Hivyo, amewaambia washiriki kuwa wana nafasi muhimu katika kulinda utu na ustawi wa manusura kabla ya kesi, wakati wa kutoa ushahidi Mahakamani na baada ya kesi.

Pia ametoa wito kwa washiriki kwenda kufanyia kazi yale watakayofundishwa ndani ya siku hizo tatu za mafunzo.

Wataalamu wa afya kutoka vituo mbalimbali nchini wanatarajiwa kunufaika na mafunzo maalumu yatakayofanyika kwa wiki moja...
22/04/2026

Wataalamu wa afya kutoka vituo mbalimbali nchini wanatarajiwa kunufaika na mafunzo maalumu yatakayofanyika kwa wiki moja jijini Dar es Salaam, yakilenga kuboresha uwezo wa kufanya maoteo sahihi ya dawa na hivyo kupunguza changamoto ya upungufu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Hatua hiyo imekuja kufuatia utafiti wa utekelezaji wa ugawaji wa dawa ulioonesha kuwepo kwa mapungufu katika mchakato wa maoteo, hali inayochangia kukosekana kwa dawa muhimu kwa wakati katika baadhi ya maeneo.

Akizungumza leo Aprili 20, katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Elimu Endelevu na Mafunzo ya Kitaaluma kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Profesa Raphael Sangeda amesema lengo kuwawezesha wataalamu hao kuongeza ufanisi na usahihi katika kupanga mahitaji ya dawa kulingana na matumizi halisi.

Amesema kupitia mafunzo hayo, washiriki watapatiwa mbinu bora za kitaalamu zitakazosaidia kuboresha mifumo ya ugavi wa dawa, kupunguza upotevu na kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa wananchi bila kukwama kutokana na ukosefu wa dawa.

“Mwisho wa mafunzo haya wataalamu wataondoka wakiwa wamesheheni elimu ambayo itaenda kuwasaidia kuboresha huduma katika sehemu mbalimbali wanazofanyia kazi,” amesema Prof Sangeda.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na uongozi wa Benki ya Ecobank, u...
16/04/2026

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na uongozi wa Benki ya Ecobank, ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Biashara na Uwekezaji kutoka makao makuu ya benki hiyo nchini Togo, Bw. Michael Larbie, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank Tanzania, Ndugu Charles Asiedu.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 15 Aprili 2026, Ikulu Zanzibar, ambapo pande zote mbili zimejadili masuala ya ushirikiano wa kiuchumi na fursa za uwekezaji. Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi ameishukuru Ecobank kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kiuchumi.

Aidha, ameihakikishia benki hiyo ushirikiano endelevu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, huku akibainisha fursa mbalimbali za uwekezaji zikiwemo bandari, miundombinu ya barabara na uchumi wa buluu.Kwa upande wake,Michael Larbie amesema Ecobank itaendelea kushirikiana na Zanzibar na kuimarisha ushirikiano wa kifedha na kibiashara barani Afrika kupitia mpango wake wa Pan African Partnership

WASHINDI wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu wametangazwa katika hafla ya nne ya utoaji wa tuzo hizo ...
16/04/2026

WASHINDI wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu wametangazwa katika hafla ya nne ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika Aprili 13, 2026 katika Ukumbi wa The Super Dome, jijini Dar es Salaam.

Katika matokeo hayo, Hamisi Kibari ameibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha tamthiliya, huku Bishop Hiluka akishika nafasi ya kwanza katika kipengele cha riwaya. Aidha, Abdalla Ngereza ameshinda katika kipengele cha ushairi, wakati Amina Mohamed aliibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha hadithi za watoto.

Tuzo hizo zinalenga kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili na kuendeleza fasihi nchini kupitia tanzu kuu nne ambazo ni riwaya, ushairi, tamthiliya na hadithi za watoto.

LICHA ya Yanga SC kuwa na baadhi ya wachezaji majeruhi, ila mchambuzi maarufu wa michezo, Ansibert Rafael ‘Hans Rafael’ ...
16/04/2026

LICHA ya Yanga SC kuwa na baadhi ya wachezaji majeruhi, ila mchambuzi maarufu wa michezo, Ansibert Rafael ‘Hans Rafael’ anaamini utendaji wa timu haujaathirika kwani kocha msaidizi Abdihamid Moalin amerejesha chachu benchi la ufundi.

Mshambuliaji, Laurindo Depu na Clement Mzie ni majeruhi, beki Dickson Job majeruhi, pia Prince Dube alikosekana kwa wiki kadhaa na kurejea mchezo dhidi ya TMA Stars kombe la CRDB.

Akizungumza na HabariLeo mapema leo Aprili 15, 2026, Hans Rafael amesema kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji, Yanga SC walionesha mabadiliko makubwa ya kimbinu kwa kucheza na viungo wanne na kubadilisha wachezaji maeneo tofauti.

“Wachezaji wa Yanga SC wamekuwa na uchu wa mafanikio, na hii imeanza kwa uongozi wa Injia Hersi Said, amekuwa chachu kubwa sana amekuwa akibeba maono ya klabu,” amesema Hans Rafael.

Aidha, Hans Rafael alimtaja Allan Okello na Mohammed Hussein kuwa ndio usajili mpya ambao una uhakika wa kuanza ndani ya Yanga SC.

“Wengine wamekuwa wachezaji wa kikosi, pia wengi walisajiliwa Julai mwaka jana hawapo msimu huu, hivyo hakuna usajili uliobadili mfumo wa Yanga SC,” amesema Hans Rafael.

Pia Hans aliwasifu wachezaji hao kuwa wameonesha ubora mkubwa kwa wachezaji wapya, hasa katika kutengeneza nafasi za mabao na kufunga pia.

“Allan Okello ameonesha ubora wake akicheza nyuma ya mshambuliaji anakuwa hatari zaidi kuliko akicheza winga ya kulia,” amesema Hans Rafael.

Hans Rafael pia amewasifu Yanga SC kwa kuwa na kikosi kipana chenye ubora kwani wapo wachezaji ambao wanaaminiwa na kucheza kwa ubora.

“Aziz Andambwile ana uwezo wa kuanza Simba SC, leo Mudathir Yahya, Shandrack Boka wana uwezo wa kuanza Simba SC, Mshery ni mjadala dhidi ya Kassali,” ameongeza Hans.

Kwa upande mwingine, Hans Rafael amezungumzia nafasi za makocha wazawa na kigeni, akidai kuwa bila kujali hilo, makocha wote wanapaswa kupewa nafasi.

Amesema changamoto ya wazawa hawana uzoefu wa soka la nje ya Tanzania, pia wengi wao wameridhika na kuwa makocha wa timu za ligi kuu.

“Hawachukui changamoto kutoka nje ya mipaka ya Tanzania, inaleta shida kwa sababu ligi ya Tanzania ina wachezaji wengi wageni hawajui jinsi ya kuwamudu,” amesema Hans Rafael.

Address

Mbezi Beach Kwa Zena, Block K, Plot No 5
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when EXL Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share