13/09/2024
Leo siku ya tarehe 13 september ni kumbukumbu ya kifo cha mwanamuziki wa kufoka foka kutoka nchini marekani, tupac shakur,kilichotokea mwaka 1996 baada ya nyota huyo kushambuliwa kwa risasi akiwa kwenye gari na bosi wake.
Tukio la kushambuliwa kwa tupac, lilitokea mnamo tarehe 7 september 1996 huko jijini las vegas nchini marekani, wakati tupac akiwa ndani ya gari nyeusi aina ya BMW, yeye na boss wake suge knights. Wawili hao walikuwa wametoka kwenye pambano la ngumi la mike Tyson lililofanyika katika ukumbi wa MGM Grand.
Wakiwa katika mataa, gari nyeupe aina ya Cadillac ilisimama pembeni yao, upande ambao tupac alikuwa amekaa katika siti ya abiria, ghafla mtu kutoka kwenye gari hiyo alianza kufyatua risasi, ambazo zilimpata Tupac sehemu kadhaa za mwili.
Tupac alipelekwa hospitali ambako madaktari walijaribu kuokoa uhai wake kwa siku sita. Lakini hatimae siku ya tarehe 13 september 1996, tupac alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 25 tu.
Kifo cha tupac kiliacha maswali mengi na nadharia za mbalimbali huku baadhi wakidai nyota huyo hakufa, bali alighushi kifo chake, na ya kwamba yuko hai mafichoni na siku moja atarudi, lakini mpaka leo, miaka 28 imepita Tupac hajawahi kurudi, lakini jina na kazi zake, bado zinaishi.