02/09/2026
Biashara nyingi hazifi kwa kukosa mtaji, hufa kwa kukosa mwelekeo. Mwelekeo si kuwa na wazo tu, ni kujua unakwenda wapi, unamhudumia nani, na kwa nini wateja wachague wewe na si mwingine.
Bila mwelekeo, kila fursa inaonekana ni yako, unaanza kutawanyika; leo unauza nguo, kesho chakula. Mwelekeo unakupa nidhamu ya kusema HAPANA kwa vitu vizuri ili useme NDIO kwa kitu kimoja bora zaidi.
Hufunga rasilimali zako chache - muda, pesa, nguvu - mahali pamoja kuleta matokeo makubwa. Biashara yenye mwelekeo hujenga uaminifu na utaalamu. Ukiieleweka kwa jambo moja, wateja wanakukumbuka, wanakuamini na wanarudi. Huo ndio tofauti ya bidii na akili sokoni.
IkFied.com