BABU K TZ

BABU K TZ Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from BABU K TZ, Media/News Company, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msin...
01/03/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa LPG Terminal GBP Gas Mkoani Tanga tarehe 01 Machi, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga mar...
01/03/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga mara baada ya kukagua maboresho ya gati mbili mpya wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Tanga tarehe 01 Machi, 2025.

26/11/2024
TAMKO LA KUTANGAZA SIKU YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA SIKU YA MAPUMZIKO LA MWAKA 2024
24/11/2024

TAMKO LA KUTANGAZA SIKU YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA SIKU YA MAPUMZIKO LA MWAKA 2024

03/11/2024

UTIAJI SAINI UJENZI WA SOKO LA KISASA MWANGA NA SOKO LA SAMAKI KATONGA

WAFANYABIASHARA 6140 KIGOMA KUNUFAIKA NA UJENZI WA SOKO LA MWANGA NA  KATONGA Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMINaibu W...
03/11/2024

WAFANYABIASHARA 6140 KIGOMA KUNUFAIKA NA UJENZI WA SOKO LA MWANGA NA KATONGA

Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma wapatao 4140 watanufaika na ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na wengine 2000 watanufaika na ujenzi wa Soko la Samaki Katonga, ambayo yanajengwa kupitia mradi wa TACTIC unaosimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Mhe. Katimba amesema hayo wakati akizungumza na wananchi kwenye Viwanja vya Mwanga Kigoma Ujiji, wakati wa hafla ya utiaji saini wa ujenzi wa Soko Kuu la Mwanga na Soko la Samaki Katonga katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma.

Akizungumzia ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga, Mhe. Katimba amesema hapo awali Soko la Mwanga lilikuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 1246 lakini ujenzi wake utakapokamilika litakuwa ni soko la kisasa lenye uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 4140.

“Mara baada ya ujenzi wa soko hili kukamilika, litakuwa na vizimba 1000, maduka 3040, litachukua mamalishe 100 na litakuwa na kituo cha polisi tofauti na lilivyokuwa hapo awali, hivyo maboresho ya soko hili yataongeza mapato ya Manispaa ya Kigoma kwa mwaka kutoka milioni 450 hadi bilioni 1.42,” Mhe. Katimba amefafanua.

Aidha, Mhe. Katimba amesema kuwa, ujenzi wa Soko la Samaki Katonga ukikamilika wafanyabiashara 2000 watanufaika, tofauti na hapo awali ambapo lilikuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 270.

“Ujenzi wa Soko la Samaki Katonga ukikamilika litakuwa na vizimba 300, maduka 800 na vyumba vya kutunzia samaki (cold room) 10 hivyo mapato ya Manispaa ya Kigoma kwa mwaka yataongezeka kutoka milioni 31 iliyokuwa inakusanywa hapo awali hadi milioni 183.2,” Mhe. Katimba amesisitiza.

Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Humprey Kanyenye amesema kuwa, mikataba ya ujenzi wa masoko hayo ya Mwanga na Katonga yaliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji ina thamani ya shilingi bilioni 16.49.

Mkandarasi aliyepewa kandarasi ya ujenzi wa masoko hay

03/11/2024
03/11/2024

News # #
Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lippi, Mkurugenzi Wa Manispaa ya kigoma Ujiji, Kisena Mabuba, Mkandarasi ASABHI CONTRACTOR LIMITED na PIONEER BUILDERS LIMITED wakionyesha mikataba baada ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa soko la Mwanza na soko la samaki katonga tarehe 02.11.2024

KIGOMA # # # Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- TAMISEMI akipokea taarifa ya mkoa wa Kigom...
03/11/2024

KIGOMA # # # Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- TAMISEMI akipokea taarifa ya mkoa wa Kigoma kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo kwa ajili ya kushuhudia utiaji saini ujenzi wa soko la kisasa Mwanga na soko la kisasa la Samaki la Katonga katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji leo tarehe 02.11.2024.

31/10/2024

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BABU K TZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share