sallytv

sallytv Your go-to source for Breaking news, in-depth analysis, & Exclusive interviews, Sports, Business, Politics, and Entertainment.
📧:[email protected]

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi zake za dhati kwa Mhe. Profesa A...
25/09/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi zake za dhati kwa Mhe. Profesa Arthur Peter Mutharika kwa ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa Malawi wa mwaka 2025.

Katika salamu zake, Rais Samia amesema anatarajia kushirikiana na Rais mteule Mutharika katika kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Malawi.

Aidha, Rais Samia amempongeza Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera, Chama cha Malawi Congress Party (MCP) pamoja na wananchi wa Malawi kwa kufanikisha uchaguzi wa amani na mchakato mzuri wa mpito wa madaraka.

“Mungu ibariki Afrika. Mungu ibariki Malawi,” ameongeza Rais Samia

Prof. Peter Mutharika aliwahi kuwa Rais wa nchi hiyo kati ya mwaka 2014 na 2020

  Sio mara ya kwanza sisi kinatokea kitu k**a hichi cha Kocha kuondoka, sisi ni professional na wachezaji wote Simba wap...
25/09/2025

Sio mara ya kwanza sisi kinatokea kitu k**a hichi cha Kocha kuondoka, sisi ni professional na wachezaji wote Simba wapo k**a professional hivyo kwetu sisi kimetokea lakini kimeshapita na tunafocus kupata ushindi kwenye mchezo wetu wa kwanza wa ligi kesho." - Seleman Matola Assistant Coach Simba Sports Club.

25/09/2025

Tiwa Savage, ameweka wazi chanzo cha video yake ya faragha iliyowahi kuvuja na kutikisa mitandao ya kijamii.

Akizungumza kwa mara ya kwanza kwa uwazi, Tiwa alisema:

“Mtu huyo alikuwa mpenzi wangu kwa wakati ule. Alisema alitaka ku-save video lakini akabonyeza send kwa bahati mbaya. Baadaye niligundua alikuwa amewekeana dau na marafiki zake.”

Kauli hii imewagusa mashabiki na kujiuliza kuhusu usalama wa faragha kwenye mahusiano.

📺: SnS

  Mtoto wa mstaafu Marehemu Ali Hassan Mwinyi, Abbas Mwinyi ambae ni Kaka wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la...
25/09/2025

Mtoto wa mstaafu Marehemu Ali Hassan Mwinyi, Abbas Mwinyi ambae ni Kaka wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi Leo Septemba 25 amefariki Dunia akiwa Hospitali ya Lumumba Mjini Unguja.

Abbas Mwinyi ni Mtoto wa Mstaafu Marehemu Mzee Mwinyi ambae kabla ya umauti wake alikua msemaji wa Familia mara baada ya kifo cha Baba yao.

Source: AyoTV

  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Bill Gates usiku kuamkia leo ambapo ameshiriki katika...
25/09/2025

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Bill Gates usiku kuamkia leo ambapo ameshiriki katika hafla ya “Goalkeepers” Jijini New York Marekani, iliyoandaliwa na Taasisi ya Bill Gates na kukutana na wadau mbalimbali.

Hafla hiyo ambayo ilihusu masuala ya Afya ya Watoto chini ya miaka mitano, ilikutanisha watu mashuhuri kutoka duniani kote.

Hafla hiyo ililenga kuendelea na uhamasishaji wa kuunga mkono uwekezaji katika Afya kwa ujumla na maendeleo endelevu.

  Picha mpya kutoka kwa msanii wa Bongo Fleva   ❤️🔥
25/09/2025

Picha mpya kutoka kwa msanii wa Bongo Fleva ❤️🔥

25/09/2025

  Kupitia Instagram Channel yake, mmiliki wa META, Mark Zuckerberg, ametoa shukrani kwa watumiaji wote wa mtandao wa Ins...
25/09/2025

Kupitia Instagram Channel yake, mmiliki wa META, Mark Zuckerberg, ametoa shukrani kwa watumiaji wote wa mtandao wa Instagram kwa mchango wao uliopelekea ukuaji mkubwa wa huduma hiyo.

Kwa sasa, Instagram imepiga hatua kubwa na kufikia mafanikio ya kuvutia. Inatumika na watumiaji bilioni 3 kwa mwezi, ikiwa ni mtandao wa tatu kwa ukubwa duniani nyuma ya Facebook na YouTube pekee. Thamani yake kwa sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 500, sawa na takribani trilioni 1,238 za Kitanzania.

Instagram imebadilika kutoka kuwa mtandao wa kushare picha pekee, na sasa imekuwa himaya ya kijamii na kiuchumiinayowakutanisha watu, biashara, wasanii na wabunifu wa maudhui duniani kote.

Hata hivyo, licha ya ukuaji huu na idadi kubwa ya wafuasi, bado watumiaji wengi wanatamani kuona faida moja kwa moja kupitia kipengele cha monetization, k**a ilivyo kwa YouTube.

  Mwimbaji maarufu duniani Rihanna, ametangaza rasmi ujio wa mtoto wake mpya kupitia ukurasa wake wa Instagram. Katika p...
24/09/2025

Mwimbaji maarufu duniani Rihanna, ametangaza rasmi ujio wa mtoto wake mpya kupitia ukurasa wake wa Instagram. Katika picha ya kupendeza aliyochapisha, Rihanna ameonekana akimkumbatia mtoto mchanga huku akifichua jina lake kuwa ni Rocki Irish Mayers, aliyezaliwa tarehe 13 Septemba 2025.

Hii inakuwa ni baraka nyingine kwa Rihanna na mpenzi wake, rapa A$AP Rocky, ambao tayari wana watoto wawili wakiume RZA Athelston Mayers, aliyezaliwa Mei 2022, na Riot Rose Mayers, aliyezaliwa Agosti 2023. Rocki Irish Mayers sasa anakuwa mtoto wao wa tatu, akiongeza furaha ndani ya familia hiyo maarufu.

24/09/2025

Mchambuzi wa mpira wa miguu anasema licha ya klabu ya Yanga SC kuibuka na ushindi mnono lakini Pamba Jiji FC wamapaswa wapewe sifa kutokana na ushindani wa hali ya juu kwenye mechi ya leo.

🎙️
📹

24/09/2025

Tambo za Mzee wa Utopolo baada ya kumkanda Pamba Jiji FC mabao matatu kwa sifuri katika dimba la Benjamin Mkapa.

🎙️
📹

24/09/2025

Moja ya shabiki wa Yanga SC anasema maingizo ya timu ni mazuri kilichobaki ni kwa kocha kutengeneza Chemistry nzuri baina ya wachezaji.

🎙️
📹

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when sallytv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share