
15/12/2024
NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz sambamba na Dystinct wa Morocco anayejulikana kwa miondoko ya R&B, Afrobeat na muziki wa Kiarabu, ni miongoni mwa wasanii watakao tumbuiza katika tuzo za CAF za 2024.
Makocha na wachezaji waliofanya vyema msimu uliopita wanatarajiwa kutangazwa na kukabidhiwa tuzo za mwaka 2024 katika hafla itakayofanyika kesho Jumatatu pale Palais des Congrès, mjini Marrakech, Morocco kuanzia saa 3:00 usiku kwa ukanda wa Afrika Mashariki.