Dree Football

Dree Football We love football

NEGREILA CASE (KESI YA 'NEGREILA') ni nini?Maelezo yote kuhusu KESI YA 'NEGREIRA'Huu ni mkasa maarufu sana nchini Uhispa...
10/01/2025

NEGREILA CASE (KESI YA 'NEGREILA') ni nini?
Maelezo yote kuhusu KESI YA 'NEGREIRA'

Huu ni mkasa maarufu sana nchini Uhispania, Ulaya kwa ujumla na katika ulimwengu wa michezo unaohusisha team ya FC Barcelona na aliyewahi kuwa makamu wa raisi wa umoja wa marefa wa soka la kulipwa pale Spain.

NEGREILA ni nani?
• Jina lake kamili anaitwa José María Enríquez Negreira, amezaliwa September 1945 huko jijini Barcelona nchini Uhispania

• Amewahi kuwa mwamuzi wa soka la kulipwa katika ligi kuu ya soka nchini Uhispania (LaLiga) kuanzia msimu wa 1979/80 mpaka mwaka mwaka 1992

• Mwaka 1994 alichaguliwa kuwa makamu wa raisi wa Technical Committee of Referees (CTA) chini ya Royal Spanish Football Federation (RFEF) ambayo hii RFEF ndio taasisi inayosimamia maswala ya soka pale Spain na alifanya kazi hio mpaka mwaka 2018

• Kesi hii imeitwa kwa jina la huyu mwamba kwa sababu yeye ndio mhusika mkuu kwenye hii kesi ambapo iliyohuaiana na yanayodaiwa kuwa ni malipo ya fedha kutoka Barcelona kwenda kwa kampuni za huyu Negreira ili jamaa awafanyie mchakato wakiwa uwanjani waamuzi wawe wanawapendelea kidogo...

Vuguvugu lilipoanzia...

• February 15 mwaka 2023, kituo kimoja cha redio kwa jina la Cadena SER kilitangaza kwamba kuna fununu za timu ya Barcelona kuingia hatiani kwa kosa la rushwa ambapo huyu Negreira alitajwa k**a mpokeaji wa hio 'hongo'

• Siku mbili baadae, yaani tarehe 17, kuna barua ilipatikana ambayo ni barua iliyoandikwa na Negreira kwenda kwa uongozi wa Barcelona ambapo ndani ya barua hio, Negreira anautishia uongozi wa Barcelona ya kwamba ataweka hadharani maovu ya timu hio endapo uhusiano wake na timu hio hautarudi k**a zamani.

Mpaka hapa inaonekana wazi kwamba kabla ya kutumwa kwa barua hio, kulikuwa na uhusiano kati ya Negreira na Barcelona.

Uhusiano huo ni upi?

• Barcelona walikuwa wakilipa kiasi cha fedha kwa kampuni inayomilikiwa na huyu mwamba inayoitwa DASNIL 95 kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2018 ambapo ndio aliachia nafasi ya umakamu wa raisi aliyokuwa nayo.

• Inasemekana jumla ya Euro milioni 6.65 zililipwa na Barcelona kwa kipindi chote hiko kuanzia mwaka 2001 ambapo raisi wa timu hio alikuwa Joan Gaspert na ulipaji uliendelea kwa kila raisi aliyeingia madarakani na wengine hata kuongeza kiwango kila mwaka.

• February 22 mwaka 2023, timu mbali mbalimbali za soka nchini Spain k**a Atletico Madrid, Cadiz, Tenerife, Huesca, Alaves na zingine zilielezea wasiwasi wao mkubwa kutokana na taarifa zilizochapishwa.

• Jumatano hio hio ya tarehe 22 February 2023, FC Barcelona walitoa tamko kuhusu swala hilo na walisema ya kwamba malipo hayo ilikuwa sehemu ya makubaliano yao na yeye Negreira mwenyewe ili awe msaidizi au tunaweza kusema mshauri wao wa nje katika maswala ya uamuzi wa kitaalamu na ni kitu ambacho kilikuwa ni kawaida na kinachokubaliwa kati soka

Itaendelea...







Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dree Football posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share