Chuo cha Mawazo ya Biashara

Chuo cha Mawazo ya Biashara MIFANO YA MITAJI YA BIASHARA:
🌟 KIPAJI 💡 UJUZI
🎓 ELIMU 🤝 UAMINIFU

Ni Kitu Gani Ambacho Kilikuingiza Hasara na Hutakuja Kukisahau Kamwe? 🤣🤣
27/02/2026

Ni Kitu Gani Ambacho Kilikuingiza Hasara na Hutakuja Kukisahau Kamwe? 🤣🤣

Hi Ni Moja ya Biashara Ambayo Unaweza Ingiza Pesa Nyingi Kwa Mwezi Kuliko Mwaajiriwa wa Serikali🤣
18/02/2026

Hi Ni Moja ya Biashara Ambayo Unaweza Ingiza Pesa Nyingi Kwa Mwezi Kuliko Mwaajiriwa wa Serikali🤣

Ona Jinsi Bajaji ya Gesi Inavyoweza Kukuletea Utajiri wa Haraka Ndani ya Muda MfupiUkijaza gesi ya TZS 6,000 unaendesha ...
21/01/2026

Ona Jinsi Bajaji ya Gesi Inavyoweza Kukuletea Utajiri wa Haraka Ndani ya Muda Mfupi

Ukijaza gesi ya TZS 6,000 unaendesha km 180.
Nauli ya Mwenge mpaka Mbezi ni km 18, TZS 2,000 kwa abiria.

Kwa abiria wanne unapata TZS 8,000 kwa trip moja.
Mpaka gesi iishe utaendesha trip 10.
Hivyo kwa siku unaweza kupata TZS 80,000.
Kwa mwezi mapato yanafikia takribani TZS 2,400,000.
Kwa mwaka mapato yanaweza kufikia takribani TZS 28,800,000, kulingana na upatikanaji wa abiria na uendeshaji wa kila siku.

Nilianza na nyanya za shilingi 10,000, leo hii nasafirisha mzigo wa milioni 10! Nilianza na nyanya za shilingi 10,000, l...
19/01/2026

Nilianza na nyanya za shilingi 10,000, leo hii nasafirisha mzigo wa milioni 10!

Nilianza na nyanya za shilingi 10,000, leo hii nasafirisha mzigo wa milioni 10!
​Wengi wanajua mimi ni Daktari Nasra, lakini wachache wanajua safari yangu ya mtaani baada ya kuhitimu mwaka 2014. Baada ya kituo nilichokuwa nafanya kazi kufungwa, nilirudi kuwa "mzigo" kwa shangazi yangu mpaka akataka kunirudisha kijijini Manyara.

​Ili nibaki mjini, ilibidi nitumie akili ya ziada! Siku moja nikiwa sokoni, niliona fursa kwenye tenga la nyanya. Nikaacha kuwaza "Degree" yangu ya Udaktari, nikapiga mahesabu ya biashara.

​Wakati huo nilikua nimebakiwa na TZS 50,000 tu baada ya kutumia Millioni 1 yote niliyo kuwa nasave wakati nafanya kazi.
Katika hiyo elfu 50 nilichukua elfu 10 nikajumua nyanya alafu elfu 10 nikatengeneza meza nzuri ya kupangia nyanya. Nikabakiwa na elfu 30 ya matumizi. Nikaanza biashara.

Safari haikuwa rahisi hata kidogo. Kulikuwa na siku nyanya zilioza, siku mauzo yalikuwa hafifu, na siku nililala njaa nikijiuliza k**a nilikuwa nafanya maamuzi sahihi. Wapo waliocheka, wapo waliodharau, lakini sikuacha.

Nilijifunza taratibu, nikasikiliza soko, nikajifunza kwa makosa. Faida ndogo ndogo nikazirudisha kwenye biashara. Meza moja ikawa mbili, mbili zikawa nyingi zaidi.

Leo hii ninasafirisha nyanya kutoka mikoani kwenda masokoni na kwa wateja wakubwa.

ATM ya Maji ya Kunywa ni Biashara Inayoweza Kukutajirisha Ukiwa UmelalaATM ya maji ni biashara inayojiendesha yenyewe, a...
14/01/2026

ATM ya Maji ya Kunywa ni Biashara Inayoweza Kukutajirisha Ukiwa Umelala

ATM ya maji ni biashara inayojiendesha yenyewe, ambapo wateja wanajihudumia wenyewe. Kwa maneno mengine, baada ya kuweka mashine kwenye eneo lenye wateja, huna haja ya kusimamia kila wakati wateja huja, hutoa pesa au skana kadi/QR code, na kuchukua maji safi wenyewe.

Faida za ATM ya Maji
Biashara Inayofanya Kazi 24/7: Hutoa maji kwa wateja wakati wowote, hata ukiwa huna pale.
Gharama Ndogo ya Usimamizi: Kwa kuwa wateja wanajihudumia wenyewe, unahitaji mfanyakazi mdogo au hakuna kabisa.
Maji Safi na Salama: Mashine nyingi zinatumia teknolojia ya RO, UV, na filtration ya kaboni.
Faida Inayokua: Kwa kiwango cha wastani, unaweza kupata mapato ya kila siku bila kuwekeza tena kwa wateja.
Biashara Rahisi Kuanzisha: Mashine zinaweza kuwekwa kwenye maeneo yenye watu wengi k**a vituo vya mabasi, shule, au hospitali.
ATM ya maji si tu suluhisho la kijamii, bali pia ni fursa halisi ya kifedha, ambapo unaweza kupata faida huku wateja wakipata maji safi kila wakati.

Angalia Jinsi Laki Mbili Inavyoweza Kufungua Biashara ya Uwakala na Fresh Juice 😋Kuanza biashara ya uwakala ni njia nzur...
13/01/2026

Angalia Jinsi Laki Mbili Inavyoweza Kufungua Biashara ya Uwakala na Fresh Juice 😋

Kuanza biashara ya uwakala ni njia nzuri ya kujiajiri na kupata mapato ya haraka. Kiasi cha mtaji unachohitaji kinategemea ukubwa wa biashara unayotaka kuanzisha. Hapa kuna mwongozo wa makadirio ya mtaji kulingana na viwango tofauti vya biashara:
(2) Mtaji Unaohitajika
1. Mtaji Mdogo (TZS 200,000 – 1,000,000)
Kibanda kidogo au sehemu ya kupangisha ndani ya duka
Float ya kuanzia: TZS 200,000 – 700,000
Bango la matangazo: Wakala wa Simu Zote
2. Mtaji wa Kati (TZS 1,500,000 – 3,000,000)
Kioski chako au sehemu ya uhakika ya kupangisha
Float: TZS 1,000,000 – 2,000,000
Vifaa muhimu: mashine ya POS, meza, kiti, na simu ya uwakala
Mabango ya matangazo na kadi za huduma
3. Mtaji Mkubwa (TZS 3,500,000 – 10,000,000)
Duka kubwa lenye uwakala wa mitandao yote
Float: TZS 2,000,000 – 7,000,000
Vifaa vya usalama: CCTV Camera
Huduma za ziada: kuuza vocha, simu, na vifaa vya simu

Hivyo kuanza biashara ya uwakala ni rahisi na yenye faida. Unaweza kuanza na mtaji mdogo au mkubwa, kulingana na malengo yako. Ili kuongeza mvuto kwa wateja na kuongeza mapato, unaweza pia kuhusisha brand ya biashara yako na Fresh Juice, ambapo pesa inayopatikana kwenye juice unaweza kuiingiza kwenye uwakala, na faida ya uwakala pia inaweza kuingizwa kwenye juice. Hii ni njia nzuri ya kuvutia wateja wengi zaidi na kuongeza biashara yako kwa kiwango cha juu.
BusinessTips SideHustle CashFlow Viral Motivation Success MoneyMaking

Ni mradi gani unafanya au unapanga kufanya kati ya hii?
09/01/2026

Ni mradi gani unafanya au unapanga kufanya kati ya hii?

Eti huyo dogo afanye nini ili aweze kuuza? 🤣🤣🤣
07/01/2026

Eti huyo dogo afanye nini ili aweze kuuza? 🤣🤣🤣

Ng'ombe wa Maziwa dhidi ya Bajaji: Chaguo Gani ni Bora?Ng'ombe mmoja wa maziwa unayegharimu TZS 2,000,000 anaweza kukupa...
07/01/2026

Ng'ombe wa Maziwa dhidi ya Bajaji: Chaguo Gani ni Bora?

Ng'ombe mmoja wa maziwa unayegharimu TZS 2,000,000 anaweza kukupa lita 20 za maziwa kila siku, lita 10 asubuhi na lita 10 jioni.

Ukiuza maziwa hayo mjini kwa bei ya TZS 2,000 kwa lita, utapata mapato ya TZS 40,000 kila siku.

Sii hivyo tu, ng'ombe huyu ana uwezo wa kuzaliana. Baada ya muda, idadi ya ng'ombe wako itaongezeka, na hivyo mapato yako pia yataongezeka.

Kwa upande mwingine, Bajaji yenye thamani ya TZS 12,000,000, ukimpa dereva aendeshe mjini, anaweza kukuletea hesabu ya TZS 20,000 tu kwa siku.

Kumbuka pia:
Ng'ombe anakula majani (gharama ndogo)
Bajaji inakula mafuta (gharama kubwa za kila siku)

Thamani kwa Muda Mrefu:
Ng'ombe: Thamani yake inaongezeka kwa sababu anazaliana, na unaweza kuuza wazao wake kwa bei ya juu zaidi
Bajaji: Thamani yake inapungua kadri siku zinavyopita

Kwa hiyo maisha ni kuchagua. Wewe chaguo lako ni lipi?

💸🔥 HIZI NDIO BIASHARA ZA KUANZA NA MTAJI MDOGO LAKINI MBILI 🔥💸(Usisome peke yako, mshirikishe rafiki 🙌)Watu wengi wanadh...
02/01/2026

💸🔥 HIZI NDIO BIASHARA ZA KUANZA NA MTAJI MDOGO LAKINI MBILI 🔥💸

(Usisome peke yako, mshirikishe rafiki 🙌)

Watu wengi wanadhani lazima uwe na pesa nyingi ili uanze biashara 🤦‍♂️
👉 UKWELI NI HUO SI LAZIMA!

👇 Angalia biashara hizi 5 zinazolipa hata k**a una mtaji mdogo sana:

1️⃣ Biashara ya Vitu vya Mtumba
👕👖 (Nguo, Viatu, Mikoba)
✔️ Zinauzika haraka
✔️ Wateja wengi kila siku

2️⃣ Biashara ya Sabuni za Maji na Vifaa vya Usafi 🧼
✔️ Mahitaji ya kila siku
✔️ Faida nzuri na haraka

3️⃣ Kuandaa na Kuuza Vyakula vya Haraka (Fast Food) 🍟🍔
✔️ Chips, maandazi, mayai, sambusa
✔️ Faida kila siku

4️⃣ Biashara ya Mapambo ya Nywele & Vifaa vya Saluni 💇‍♀️✨
✔️ Weaves, beads, mafuta, vifaa
✔️ Wanawake ndio soko kubwa

5️⃣ Uuzaji wa Matunda na Juisi Asilia 🍍🍉🥤
✔️ Afya kwanza
✔️ Mahitaji yanaongezeka kila siku

🚀 KUMBUKA:
Si mtaji unaokuchelewesha…
👉 Ni uamuzi wako!

💬 ONGEZA NYINGINE KWENYE COMMENT
👇👇
Ni biashara ipi umejaribu au ungependa kuanza?

❤️ Like | 🔁 Share | 💬 Comment
Post hii inaweza kumbadilisha mtu maisha!

✨ Biashara 5 Zenye Faida Mwaka 2026 Unazoweza Kuanzisha kwa Mtaji wa Laki 3! ✨Unataka kuanza mwaka mpya kwa faida na bia...
01/01/2026

✨ Biashara 5 Zenye Faida Mwaka 2026 Unazoweza Kuanzisha kwa Mtaji wa Laki 3! ✨
Unataka kuanza mwaka mpya kwa faida na biashara ndogo? Hapa kuna biashara 5 unazoweza kuanzisha ukiwa na mtaji mdogo wa Tsh 300,000:
💰 1. Kuuza mitumba
🧹 2. Biashara ya usafi
🌾 3. Kuuza nafaka na vyakula
🌱 4. Kilimo
📱 5. Duka la kutengeneza simu
💡 Tip: Anza ndogo, pandisha hatua kwa hatua, na weka nidhamu ya kifedha. Mtaji mdogo leo unaweza kuwa biashara yenye faida kubwa kesho!

✨ Fanya haya mambo 10 ili ufanikiwe sana mwaka 2026! ✨Mwaka mpya ni fursa ya kuanza upya kifedha. Jitathmini, weka malen...
01/01/2026

✨ Fanya haya mambo 10 ili ufanikiwe sana mwaka 2026! ✨
Mwaka mpya ni fursa ya kuanza upya kifedha. Jitathmini, weka malengo wazi, panga matumizi yako, jenga akiba, na fuata nidhamu kila siku. Mafanikio si tu kipato kikubwa, bali ni maamuzi sahihi na mazoezi thabiti.
📌 Hapa kuna mambo 10 muhimu:
1️⃣ Jitathmini kifedha bila kujilaumu
2️⃣ Weka malengo ya fedha yaliyo wazi na yanayopimika
3️⃣ Panga matumizi kabla ya kutumia
4️⃣ Jenga akiba ya dharura (hata kidogo)
5️⃣ Dhibiti matumizi kuliko kutegemea kipato kikubwa
6️⃣ Tenganisha mahitaji na tamaa
7️⃣ Epuka mikopo isiyo ya lazima, tumia mikopo kwa busara
8️⃣ Fuata matumizi yako kila siku/mwezi
9️⃣ Ishi chini ya uwezo wako
🔟 Pitia na rekebisha malengo yako mara kwa mara
💡 Kumbuka: Mafanikio ya kifedha hayaanzi na kipato kikubwa, yanaanza na nidhamu, mpangilio, na maamuzi bora.

Address

Mwenge
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chuo cha Mawazo ya Biashara posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share