FreeVoice TV

FreeVoice TV Dickson Mush welcome to our official page for fun videos,movies,magic,music
(1)

Waziri Mkuu mstaafu Kassim Majaliwa ameonekana mapema leo asubuhi akiendesha baiskeli mitaa ya mbweni  Jijini  Dar es sa...
06/06/2026

Waziri Mkuu mstaafu Kassim Majaliwa ameonekana mapema leo asubuhi akiendesha baiskeli mitaa ya mbweni Jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kila siku wa kujenga afya na kuimarisha mwili.

Hatua hiyo imeendelea kutoa hamasa kwa Wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuboresha afya zao na kupunguza hatari ya magonjwa yasiyoambukiza.

Kwa mujibu wa Wataalamu wa Afya na Wadau wa Mazoezi, kuendesha baiskeli ni aina ya mazoezi ya mwili (cardio) ambayo husaidia kuimarisha moyo na mapafu, kuboresha mzunguko wa damu na kuongeza uwezo wa mwili kustahimili uchovu.

06/06/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Tanzania haiko chini ya vikwazo vyovyote, na kwamba serikali inaendelea kujipanga kuchochea maendeleo.

Rais Samia ameyasema hayo leo Juni 5, 2026 alipokuwa akihitimisha ziara yake ya Kitaifa katika Urusi, ambapo alihutubia Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na Urusi pamoja na Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF), lililowakutanisha viongozi, wataalamu, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, amewasihi watumishi wa sekta ya afya katika Wilaya ya Ilala kufanya kazi k...
05/06/2026

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, amewasihi watumishi wa sekta ya afya katika Wilaya ya Ilala kufanya kazi kwa ushirikiano, weledi na uwajibikaji ili kuendelea kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wananchi_.

Mhe. Mpogolo ametoa wito huo leo, Juni 2026, wakati wa kikao kazi cha utiaji sainie wa mikataba ya utendaji kazi kwa watumishi wa sekta ya afya kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa dhamira ya mikataba hiyo ni kuweka uwazi katika utekelezaji wa majukumu, kuimarisha uwajibikaji na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi, sambamba na kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza wajibu wake kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa.

“Mikataba hii ni nyenzo muhimu ya kupima utendaji kazi wetu. Niwahimize kufanya kazi kwa ushirikiano, kuheshimiana na kuweka mbele maslahi ya wananchi ili huduma zinazotolewa ziwe bora zaidi,” amesema Mhe. Mpogolo.

Pia Mhe. Mpogolo amewahakikishia watumishi hao kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kufikia malengo ya kuboresha huduma za afya katika wilaya hiyo.

Mhe. Mpogolo amewataka watumishi wa afya kuwahudumia wananchi kwa tabasamu, upendo na utu, akisisitiza kuwa huduma bora kwa wananchi ni miongoni mwa maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Sambamba na hilo, Mhe. Mpogolo amekipongeza Kituo cha Afya Chanika kwa kupata Cheti cha Ithibati, hatua ambayo imeonyesha juhudi na mafanikio ya kituo hicho katika kuzingatia viwango vya ubora wa huduma za afya.

Amesema mafanikio hayo yanapaswa kuwa chachu kwa vituo vingine vya afya kuendelea kuboresha huduma zao ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya zenye ubora, usalama na zinazokidhi viwango vinavyotakiwa.

01/06/2026

DIWANI KATA YA ZINGIZIWA AKEMEA WANAOKIUKA MAADILI.

Diwani wa kata ya Zingiziwa iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Mhe. Selemani Kaniki ametoa wito kwa Jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi kukemea na kukomesha vitendo vinavyopelekea mmonyoko wa maadili katika Jamii.

Mhe. Kaniki ametoa wito huo wakati wa mkutano wake na wananchi wa mtaa wa Nzasa ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana nao kila mwezi na kusikiliza kero zao.

Amesema Jamii haina budi kukemea vitendo hivyo ambavyo vinasababisha mmonyoko wa maadili huku akilisifu Jeshi la Polisi kwa kuendelea kuchukua hatua kwa watu wanaokiuka maadili na kuvunja Sheria katika Kata hiyo.

27/05/2026

‎Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa ufafanuzi kuhusu changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji iliyowakumba wakazi wa maeneo yanayohudumiwa na Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu kuwa ni matengenezo makubwa yaliyolenga kuboresha na kuimarisha huduma zaidi.

‎Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Bi. Everlasting Lyaro, amesema kukosekana kwa huduma hiyo tangu Machi 26,2026 kulitokana na utekelezaji wa kazi muhimu tatu katika mtambo huo, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa uzalishaji na usambazaji wa maji kwa wananchi.

18/05/2026

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza hatua ya kwanza ya utekelezaji wa mkakati wa miaka mitano wa kupunguza upotevu wa maji unaotekea katika eneo la huduma ya mamlaka hiyo, kwa kuanza marekebisho katika maeneo yenye mivujo inayoonekana.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire amesema kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Ewura inaonesha upotevu wa maji umekuwa mkubwa kwa wastani wa asilimia 35 kwa nchi kwa ujumla, hivyo endapo kiwango hicho kitaweza kusimamiwa vizuri huduma ya maji itaboreka na kuwafikia wananchi kwa ukubwa kwa kupunguza kiwango cha maji yanayopotea.

16/05/2026

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Malori ya Masafa marefu Tanzania (TLDTA), Hassan Dede amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi inayoonekana katika sekta mbalimbali ikiwemo ya uchukuzi, kupitia waziri wake Profesa Makame Mbarawa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Dede amesema imekua ni mara ya kwanza kwa chama cha maderava kupata mwaliko wa kuhudhuria vikao vya bunge katika uwasilishaji wa bajeti ya wizara ya uchukuzi, ambapo Mbunge Rashidi Shangazi aliibua hoja iliyochangiwa na wabunge mbalimbali kuhusu maslahi ya madereva wa masafa marefu ikiwemo mikataba.

Amesema kuwa hatua ya madereva kualikwa bungeni kwa mara ya kwanza inatoa matumaini ya kuwa changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakiziwasilisha serikalini na wabunge zimeanza kutazamwa ama kufanyiwa kazi, huku wakitoa matarajio makubwa kwa Rais Samia kufanya mambo makubwa zaidi katika uongozi wake.

15/05/2026

Serikali imeziomba kampuni binfasi zonazohusika na uzalishaji au usambazaji wa huduma pamoja na vifaa vya Afya kujitolea kusaidia kwenye vituo vya Afya ili kupunguza changamoto zilizopo na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma bora za Afya nchini.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Leo Mei 15,2026 wakati anapokea ya taulo za k**e na za watoto 8000 zilizotolewa Hospitali ya Amana kwa ajili ya wanawake na watoto zitakazogaiwa bure kwa kipindi cha miezi mitatu.

13/05/2026

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kupata kichwa cha aliyekua mwanafunzi wa IFM, James Temba, ambaye hivi karibuni mwili wake ulikutwa ukielea kwenye maji ya Mto Msimbazi nakuzikwa Mkoani Kilimanjaro.

Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 13, 2026 jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Aidha, amesema kuwa baada ya upelelezi wa kina kufanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya uchunguzi wa kisayansi, sehemu ya kichwa hicho imepatikana eneo la Kitunda Kibeberu, Wilaya ya Ilala, kikiwa kimefukiwa ardhini.

“Hadi sasa watu watano wamekamatwa, akiwemo mganga wa kienyeji anayejulikana kwa jina la Saidi Ally (Side) Mzigua (31),” amesema SACP Muliro.
Na kuongeza kuwa, “Taratibu za kisheria zinakamilishwa ili watuhumiwa wafikishwe kwenye mamlaka za kisheria.”

Aidha, amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwashukuru wananchi na mamlaka nyingine za uchunguzi wa kisayansi katika kufanikisha zoezi la upatikanaji wa kichwa hicho.

“Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuacha kutoa taarifa za upotoshaji wakati uchunguzi wa matukio ya kihalifu, ikiwemo mauaji, unaendelea.”

Hata hivyo, Jeshi hilo linaendelea kulaani watuhumiwa waliotekeleza mauaji hayo na kwamba litaendelea kufuatilia jalada la kesi hiyo ili watuhumiwa wapate adhabu wanayostahili. Part 3

13/05/2026

Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dkt. Lazaro Mambosasa, amewataka wananchi kupuuza tangazo la uzushi linalosambazwa mtandaoni na kwamba wanaohusika kuandaa au kutengeneza tangazo hilo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Address


Telephone

+255768161054

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when FreeVoice TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share