16/03/2025
Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi wa Oktoba.
*Zanzibar kumoto juu ya madai ya Chama kikuu cha upinzani cha ACT Wazalendo kutaka usawa na haki pamoja na kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi Zanzibar (ZEC). Suala la kupiga kura siku mbili lapingwa vikali sana na ACT Wazalendo kwa madai kuwa baadhi ya wafanyakazi wa serikalini na vikosi vya SMZ wanatumiwa kuwapigia kura CCM kwa kulazimishwa. Nao CCM Zanzibar wanasema upigaji kura siku mbili ndivyo katiba na sheria ndivyo inavyosema na ilitungwa kihalali ndani ya Baraza la Wawakilishi, katiba na sheria hiyo iheshimiwe. Nini kitatokea huko Zanzibar? Wagombea urais wa Zanzibar majina yameshatangazwa, CCM imemtangaza Mhe. Hussein Ali Mwinyi na ACT Wazalendo imemtangaza Mhe. Othman Masoud Othman.
*Tanzania Bara, Mwenyekiti wa Chama Cha CHADEMA, Tundu Lissu amekuja na kauli mbiu ya "No reform no election". Yaliyotokea mwaka 2020 bado yanawaliza sana CHADEMA, wanasema uchaguzi wa mwaka wa 2020 haukuwa huru wala haukuwa na haki, matokeo halisi ya kura hayakutangazwa vituoni, matokeo yaliyoyatangazwa ni yaliyopangwa na makamishna wakuu wa halmashauri wakishirikiana na jeshi la polisi kwa kutii amri kutoka juu. CHADEMA inasisitiza bila ya kuwepo tume huru na ya haki ya uchaguzi kutakuwepo uchaguzi, na wananchi ndiyo watakaoamua hivyo.
Nini kitaendelea?
Ukurasa wako wa Hahama Media upo kukujuza mengi kuhusu uchaguzi wa Tanzania na Zanzibar 2025. Tuombe uhai na uzima.