27/10/2025
Dr. Nandipha : Ndege Mjanja hunaswa na tundu bovu-3
Nandipha alikuwa kwenye penzi zito na Thabo Bester. Historia ya Thabo Bester haiko wazi sana. Ambacho kiko wazi ni kwamba Bester alikuwa binadamu. Alizaliwa na mwanamke. Mama yake anaitwa Maria Mabaso. Alizaliwa huko Soweto. Mama yake hakuwa na maisha mazuri alikuwa anafanya vibarua vya kulima. Bester hakuwa na hata cheti cha kuzaliwa. Makuzi yake hayako wazi sana. Lakini mara kadhaa Bester alikumbwa na shutuma za ulaghai na udanganyifu katika umri mdogo. Bester alikuwa tapeli. Akiwa na miaka 19 Bester alifungwa miaka miwili gerezani kutokana na makosa ya ulaghai.
Ukweli ni kwamba, malezi ya Nandipha na Bester yalikuwa ardhi na mbingu. Wakati mwingine watoto waliolelewa vizuri k**a Nandipha huwa wanakosa kuzijua kanuni za kitaa. Hawa ni rahisi kudanganyika kwa sababu wanafikiri kwamba duniani watu wote ni wema k**a walivyokuwa wazazi wao. Mitaa ina kanuni zake. Kanuni zake hazifundishwi chuo Kikuu. Nandipha hakuyajua haya.
Bester kwake mtaa ndio ulikuwa nyumbani kwake. Yeye toka anazaliwa alijua aishi namna gani aweze kusurvive mtaani. Bester alikuwa anajifanya wakala na anawasaidia wanawake ambao walikuwa wana ndoto ya kufanya kazi ya urembo kutimiza ndoto zao. Bester alikuwa anawaaminisha kwamba yeye alikuwa anazijua njia za kuwafanya wafike wanapotaka kufika. Wanawake walimwamini. Kila walipokuwa wanakutana nae, Bester aliwabaka na kisha kuwaibia simu la laptop na kuwatishia kisu.
Bester hakuishikia kuwabaka tu, mwaka 2011 Bester alimuua kikatili aliyekuwa mpenzi wake Nomfundo Tyhulu. Nomfundo alikuwa bado mdogo sana. Wakati anafariki alikuwa na umri wa miaka 27.
Nomfundo na Bester walikuwa wamejuana miezi 8 tu. Walikuwa hawaishi pamoja. Nomfundo alikuwa anaishi Johannesburg wakati Bester Durban. Siku moja Nomfundo akampigia simu Bester, akamwambia amepata ajira mpya. Bester akamdanganya kwamba anataka apige picha. Wakaenda Capetown. Hiyo ilikuwa tarehe 19 September 2011. Wakafikia hotel inaitwa One&Only. Hii ni hotel ya Nyota 5 ambayo gharama ya chumba si chini ya Shilingi Milioni 1.5. Wakaa hapo siku 2.
Siku ya tatu wakahamia hotel nyingine. Nomfundo akagundua kwamba..!
Itaendelea... Ijumaa !
Dr. Nandipha : Ndege Mjanja hunaswa na tundu bovu-4
Siku ya tatu wakahamia hotel nyingine. Nomfundo akagundua kwamba kumbe Bester bado alikuwa na mahusiano na mpenzi wake wa zamani. Tena walikuwa wanapasha kiporo k**a kawaida. Hii ilimuumiza Nomfundo ambaye alikuwa ana amini Bester ni wake tu. Siku nzima walikuwa wanazozana. Baada ya kuzozama wakaenda kulala. Hiyo ilikuwa ni tarehe 21 September mwaka 2011.
Tarehe 22 September 2011.
Saa 8 usiku Nomfundo anashtuka usingizini. Anakuta Bester akiwa amesima huku amemnyooshea kisu. “Lete simu na lap yako hapo”. Bester anaamrisha. Maskini wakati Nomfundo hajajua afanye nini, Bester anashusha kisu na kumdunga Nomfundo kifuani. Nomfundo anapapatika huku damu zikiruka mithili ya kuku wa Krismasi. Bester akamfunga Nomfundo mikono nyuma kwa kutumia t-shirt, kisha akamwamuru atoe password ya laptop. Masaa matano baadae Bester akaondoka na kumwacha. Bester akamwambia mhudumu wa guest kwamba, Nomfundo alikuwa amelala, asimsumbue labda atamwamsha kuanzia saa 8 mchana. Kumbe Nomfundo alikuwa tayari amekufa.
Ilipofika saa 3 usiku wahudumu wakaenda kumgongea Nomfundo. Maskini Nomfundo wa watu alikuwa amekufa tayari. Damu zilikuwa zimetapakaa karibu chumba kizima.
Ilikuwa ngumu kumk**ata Bester. Kwa sababu Facebook alikuwa na zaidi ya akaunti 13 huku akitumia majina tofauti. Hii ndio sababu aliitwa Mbakaji wa Facebook. Siku anak**atwa alikutwa na line za simu 100. Baada ya kuk**atwa. Bester akikiri kwa kinywa chake ni yeye ndie aliyemuua Nomfundo. Bester akahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Akiwa gerezani, Bester akaanzisha mahusiano na Dr. Nandipha Magudumana...
Itaendelea...
Dr. Nandipha : Ndege Mjanja hunaswa na tundu bovu-5
Simu ya mume wa Nandipha ilikuwa inaita. Kuangalia ni namba mpya. Akapokea.
“Habari shemeji,” kumbe ni kaka yake Nandipha alikuwa amepiga.
“Salama” mume wa Nandipha akajibu
“Shemeji Nandipha amek**atwa”
“Nandipha ndio nani” mume wa Nandipha akauliza k**a ndio kwanza analisikia jina hilo kwa mara yako.
“Nandipha Magudumana, mkeo, mama wa watoto wako humjui shemeji” kaka yake akajibu.
“Huyo mtu mimi simjui wala sijawahi hata kumsikia. Utakuwa umekosea namba”, mume wa Nandipha akakata simu kabisa.
Pengine ningekuwa hata mimi ningemkana mchana kweupe. Mwanamke umemuoa, ukazaa nae. Leo anaondoka na kwenda kutangatanga kisha ndugu zake wanakupigia simu. K**a sio kumkana basi ningekemea pepo. Pepo tokaaa.
Haiko wazi sana Nandipha na Bester walijuanaje. Lakini mahusiano yao yanapamba moto kuanzia mwaka 2017. Lakini walikutanaje?
Inadaiwa kwamba, Nandipha na Bester walijuana toka mwaka 2006 katika chuo Kikuu cha Witwatersrand. Inaamika Bester alikuwa akiendesha matamasha ya mambo ya urembo na mitindo. Nandipha alikuwa mmojawapo wa mabinti waliokuwa wakishiriki katika matamasha hayo. Miaka ikaenda wakiwa wanawasilina. Ilipofika mwaka 2011 wakapotezana. Baada ya hapo Nandipha akaolewa na kupata watoto.
Mwaka 2016 Nandipha na Bester wakaanza kuwasiliana tena. Nandipha akaanza kumtembelea gerezani mara kwa mara. Penzi likakolea. Nandipha akawa haambiliki tena. Nandipha akawa anafanya anachoambiwa na Bester. Mwaka 2020, Nandipha akawasilisha nyaraka kwamba alikuwa amechumbiwa na Bester. Hii ilikuwa k**a mkosi kwake kwani mwaka 2021 Nandipha akafungiwa kutibu..!
Itaendelea...!
Dr. Nandipha: Ndege Mjanja hunaswa na tundu bovu-6
7 April 2023, Arusha Tanzania
Sasa haikuwa siri tena kwamba Bester hakufa gerezani. Ilikuwa wazi Nandipha ndie aliyemsaidia Bester kutoroka gerezani. Habari hizi zilikuwa wazi kwa kila mtu. Bester na Nandipha walijua kwamba walikuwa wanatafutwa. Sasa wakae Afrika Kusini wanafanya nini. Uamuzi ulikuwa mmoja tu. Kutoroka.!?
Polisi walishtuka kwamba tayari Nandipha na Bester walikuwa hawako tena Afrika Kusini. Gari waliyotumia ilikutwa imetelekezwa kwenye mpaka wa Msumbiji na Afrika Kusini. Tayari Bester na Nandipha walikuwa Dar es Salaam Tanzania. Huko Nandipha alikuwa anavaa juba na kujifunika gubi gubi. Bester nae alikuwa anavaa nguo za kuficha uso. Hata hivyo Dar es Salaam ilikuwa ni njia ya mpito tu.
Tarehe 7, April Saa 11 alfajiri polisi wa Tanzania, wakiwa na polisi wa Interpol walikuwa wameizunguka Hotel moja maarufu jijini Arusha. “Tunamtaka mteja aliyelala chumba namba 44”. Hayo yalikuwa ni maneno ya polisi kwa mhudumu wa hotel hiyo. “Wameondoka k**a dakika 10 zilizopita”, mhudumu akawajibu na kuwaacha polisi wanaangaliana. Sasa watakuwa wanakwenda wapi. Nairobi ndio kituo kilichokuwa kinafuata.
Polisi wakajiongeza. Mbio mbio mpaka kwenye kizuizi cha barabarani kuelekea mpaka wa Namanga. Ikapita gari ya kwanza, ikapita gari ya pili. Hatimaye ikasimamishwa gari moja iliyokuwa spidi. Shusha vioo. Polisi mmoja akaita kwa kujiamini. Bester umekwisha. Bester akashukta. Wamenijuaje. “Mko chini ya Ulinzi”. Hapo wakak**atwa Bester akiwa na Dr. Nandipha pamoja na mtu mwingine raia wa Msumbiji.
Afrika Kusini ikapigwa na butwaa, imevichukua vyombo vya nchi hiyo miezi 11 kubaini Bester katoroka, lakini imewachukua siku 2 tu polisi wa Tanzania kumk**ata Bester na washirika wake. Huo ndio ukweli. Bester alikuwa tayari amek**atwa. Hiyo ilikuwa ni siku ya Ijumaa. Kifuatacho. Warudishwe Afrika Kusini kujibu mashtaka yaliyokuwa yanawakabili.
Siku 6 baadae,Bester na Nandipha walikuwa Afrika Kusini na kisha kusomewa mashtaka. Nandipha na Bester bado wako gerezani huko Afrika Kusini. Kesi yao itaanza kusikilizwa mwezi Novemba. Kwa sasa kuna habari kwamba huko gerezani Nandipha ana mimba ya miezi 5..!
Mwisho