31/12/2025
USIMUUZIE KILA MTU....
Ukijaribu kuuza kwa kila mtu, hutauza kwa mtu yeyote.
Muuza bora humjua mteja wake ni nani, na ni nani Si mteja wake.
Hili ndilo kosa kubwa ambalo watu wengi wanaoanza biashara na mauzo hulifanya.
Wanataka kila mtu anunue bidhaa yao.
Wanataka kila anayewaona, asikilize, apende na anunue.
Lakini ukweli ni huu👇
👉 Biashara hazikui kwa kujaribu kufurahisha kila mtu.
👉 Mauzo hayazaliwi kwa kelele nyingi, yanazaliwa kwa ujumbe sahihi kwa mtu sahihi.
Muuza bora hana shida kusema:
“Bidhaa hii si kwa kila mtu.”
Na kwa kushangaza, hapo ndipo mauzo huanza kuongezeka.
Kwa nini?
Kwa sababu anapozungumza, anayezungumza naye anajiona ndani ya ujumbe.
Anahisi: “Huyu ananiongelea mimi.”
Ukijua:
Nani hasa unamsaidia
Ana shida gani
Anaogopa nini
Anataka matokeo gani
Basi hauhitaji kushawishi sana.
Hauhitaji kupunguza bei kupita kiasi.
Hauhitaji kuomba watu wanunue.
Unachofanya ni kuweka ujumbe sahihi mbele ya mteja sahihi.
Kumbuka hili
❌ Ukilenga kila mtu → hakuna anayehisi ujumbe ni wake
✅ Ukimlenga mtu mmoja vizuri → wengi wanaofanana naye watanunua
Ndiyo maana wauzaji wakubwa huanza na swali moja muhimu sana:
“Huyu ninayemuuzia ni nani hasa hasa kuanzia jinsia, Hali, Umri na yote mpaka anapoishi?”
Ukishajua hilo,
mauzo hayawezi kuwa magumu —
yanakuwa ya asili.
📌 K**a unajifunza biashara, mauzo au ujenzi wa mfumo wa kipato mtandaoni, hili ni somo la msingi usiliruke.