11/07/2025
Tanzania ilivyojidhatiti mapambano dhidi ya rushwa
DODOMA-Serikali imesema kuwa, marekebisho ya sheria yaliyofanyika hivi karibuni yameongeza nguvu zaidi kwa kutambua makosa ya rushwa yanayofanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo upande wa burudani, michezo,chaguzi na mengineyo.
Hayo yamebainishwa leo Julai 11,2025 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa George Simbachawene wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa barani Afrika.
Amesema, kupitia Sheria ya Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, Taasisi ya Kuzuia na Kupambaba na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imepewa mamlaka ya kuhakikisha kuwa rushwa inatokomezwa nchini.
Vilevile amesema,Serikali imeendelea kuipatia TAKUKURU rasilimali fedha, kibali cha kuajiri watumishi wapya na vitendea kazi na samani za ofisi ili kuongeza ufanisi wake wa kazi | https://www.diramakini.co.tz/2025/07/tanzania-yatembea-kifua-mbele-mapambano.html