
26/08/2025
Alikuwa akitoka nyumbani huku akiacha wosia mmoja kwa mkewe: alisema
“Mke wangu iwapo nitapatwa na jambo, au nikichelewa, na mkihitaji kitu…baasi piga simu namba hii.”
Mkewe akamuuliza: “Namba ya nani hii?”
Akasema kwa utulivu: “Namba ya ndugu yangu.”
Akaona ajabu; maana anamfahamu vyema mume wake kuwa hana ndugu, lakini akatikisa kichwa na akaendelea kimya na mume akaondoka.
Siku zikapita. Mume akatoweka wiki nzima, jambo lisilo desturi yake.
Vitu vya nyumbani vikaanza kuisha kidogo kidogo, hadi makabati yakawa matupu.
Mama akachoka na hofu ikamzidia. Watoto wakawa wanalia kwa njaa kali, naye hakuwa na chochote cha kuwatuliza nacho watoto.
Alijaribu kumpigia mumewe mara nyingi. Simu ilikuwa imezimwa au haipatikani.
Na mambo yalipozidi kuwa mabaya, alikumbuka wasia wa mume wake.
Akachukua simu na kupiga namba ile.
Akapokea mwanaume kwa sauti yenye ya kuchoshwa, kana kwamba alikuwa na tatizo kazini:
Akasema,
“Ni nani anayepiga?”
Yule mke akasema huku akilia: “Watoto wangu wamechoka kwa njaa kwa siku kadhaa, na hatujapata habari yoyote kuhusu mume wangu Muhammad. Aliniacha na wasia kuwa tukihitaji kitu nikupigie, na akasema wewe ni ndugu yake… nami najua hana ndugu.”
Akamjibu akiwa na hasira na kukerwa: “kata simu mama”
Lakini kabla hajakata simu, ghafla sauti ya maneno ya mwanaume yakaingia yenye ukali wa kutaka kujua jambo zaidi:
“Subiri mama! Umesema Muhammad? Muhammad yupi?”
Akasema kwa majonzi: “Mume wangu, Muhammad bin …” (akamtaja kwa jina kamili).
Kimya kikarefuka upande wa pili, kisha sauti ikabadilika ghafla, ikawa yenye hofu na mshtuko: Yule mwanaume akasema...
“Wewe ni mke wa Muhammad?! Subiri hapo, usiweke mbali simu!”
Moyo wa mama ulishikwa na mshangao.
Dakika chache baadaye, mlango wa nyumba yake ukagongwa kwa nguvu. Alipofungua, akakuta kundi la watu wakishikilia mifuko ya chakula, nguo na pesa. Nyuma yao akiwa amesimama yule mwanaume aliyepokea simu.
Yule mwanaume akamwendea mama yule huku machozi yakimtiririka: akisema
“Samahani dada yangu… Muhammad si ndugu yangu wa damu, bali ni ndugu yangu katika dini na ktk mema. Yeye kila mwezi alikuwa akinipatia kiasi cha pesa, akiniusia akisema kwamba: ‘Iwapo siku moja sitakuwepo, na familia yangu ikihitaji msaada, basi wewe ndiye ndugu niliyewaachia familia yangu.’”
Mwanamke akabaki kustaajabu, machozi yakitiririka.
Mwanaume akaendelea:
“Nilidhani amekusahau… kumbe alikuwa anakuamini na akaniachia dhamana. Nimekosea kwa sauti yangu mbaya niliyokujibu nayo, lakini kuanzia leo mimi ndiye ndugu yenu, na nyumba yenu haitakosa riziki.”
Watoto wakakimbia wakishika mikono ya wale waliobeba chakula, wakicheka huku machozi ya mama yao yakibubujika kwa furaha.
✨ Funzo:
Wema wa kweli ni kuacha nyuma amana na msaada kwa familia, si kwa maneno tu bali kwa vitendo. Muhammad alijua thamani ya ndugu wa kweli, hata k**a si wa damu.
✍️Kujiandaa na maisha – Mume alitambua kuwa maisha yanaweza kubadilika ghafla, akawaacha mke na watoto wake na wasia wa msaada. Hii ni funzo kwetu tuwe na mipango ya kuwalinda wategemezi wetu.
✍️Undugu wa Kiislamu – Hata k**a si ndugu wa damu, undugu wa imani na wema una thamani kubwa. Muhammad alimchagua mtu wa amana na kumwita ndugu.
👉Msaada kwa wakati wa dhiki – Wema wa kweli huonekana wakati wa shida. Ndugu huyo alipobadilika na kuwasaidia familia, alidhihirisha thamani ya undugu wa Kiislamu.
🫵Kutokudharau maombi ya wenye shida – Mwanzo aliongea kwa kero, lakini alipofahamu ukweli alibadilika. Funzo ni tusidharau kilio cha mhitaji, huenda ndani yake kuna uokovu wetu.
🤝Kuwajibika kwa familia – Kila mtu anapaswa kuwaza mustakabali wa familia yake hata endapo atapatwa na kifo au matatizo.
💫Mali bora ni mali inayotumika kwa wema Muhammad hakuridhika kufaidika peke yake, bali alitumia riziki yake kuandaa msaada kwa familia yake.
Endelea kufuatilia ukurasa wangu
Hakikisha umebofya jina la Sufian Mzimbiri ili uweze kuni follow na kujifunza mengi zaidi.