Patrick Keha

Patrick Keha Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Patrick Keha, Digital creator, Dar es Salaam.

Nasaidia Watu Kutatua Migogoro Na Changamoto Zote Kwenye Mahusiano|Uchumba na Ndoa| Na Kuwaelimisha Namna Ya Kujenga Mahusiano Imara|Ya Kudumu Na Yenye Furaha |Kwa Huduma Ya Ushauri Wasiliana Nami Kupitia WhatsApp Gusa Namba👇

wa.me/255655653744

Au Anakwambia "Sawa ni vizuri" 😂Umewahi kukutana nayo hii?Tupe story kidogo
17/09/2026

Au Anakwambia "Sawa ni vizuri" 😂

Umewahi kukutana nayo hii?
Tupe story kidogo

Aliyempa Speed Kubwa Duma Ndiye Aliyemnyima Kobe Mbio..Na Ndiye Anayewapa Wote Uwezo Wa Kupambana Na Kupata Riziki Kila ...
17/09/2026

Aliyempa Speed Kubwa Duma Ndiye Aliyemnyima Kobe Mbio..

Na Ndiye Anayewapa Wote Uwezo Wa Kupambana Na Kupata Riziki Kila Mmoja Kwa Nafasi Na Uwezo Wake..

"Mungu Akikupa Kirema Hawezi Kunyima Mwendo". Ni Jinai Kutamani Uwe K**a Fulani Badala Ya Kushukuru Na Kufurahia Uspecial Ambao Mungu Amekuumba Nao.

Twiga Kamwe Hawezi Kuswa Swala K**a Ambavyo Swala Hawezi Kuwa Simba.

Hakuna Aliyeumbwa kwa Bahati Mbaya, Maisha Ni Safari Sio Mashindano.

Kuwahi Au Kuchelewa Kupata Ni Sehemu Ya Safari Ya Maisha, Hupaswi Kukata Tamaa KwaSababu Tu Uliyoyahitaji Yamechelewa Kutimia. Kwa Kuwa Hatujafika Mwisho Wa Safari Basi Amini Bado Unayo Nafasi.

Kikomo Pekee Kinachotosha Kukupa Uhakika Wa Kutotimiza Ndoto Yako, Ni —Kaburi.
K**a Uko Nje Ya Kaburi, Amini Hakuna Kisichowezekana.
Kilichoonekana K**a Ndoto, Kilikuja Kuwa Uhalisia 2009, Barack Obama Kuwa Rais Wa Kwanza MuAfrica Taifa La Marekan.

K**a Ilivyokuwa Kwa Nelson Mandela Miaka 27 Gerezan, Na Bado Akatoka Na Kuwa Rais Wa Africa Kusin. Sasa Kwanini Wewe Unazikatia Tamaa Ndoto Zako, Sababu Ya Changamoto Ndogo Unazopitia?—Amka Ndoto Bado Inakungoja, Usiikatie Tamaa.

Usiyakatie Tamaa Maisha Yako—Ndoto Inaweza Kuwa Uhalisia, Bado Unaweza Kushinda Na Kusimama Tena.

Kinachohitajika Sio Ukubwa Wa Mbio, Ni Nguvu Ya Kukimbia Hadi Mwisho.

Goliath Alikuwa Na Umbo Kubwa + Uzoefu Mkubwa Kuliko Daudi, Ila Daudi Alishinda Vita💪.

Hakuna Kukata Tamaa, Pambana Mpaka Mwisho✊

Naitwa Patrick Keha

WhatsApp 0655 653 744

Haaa😂
16/09/2026

Haaa😂

Mkuu mimi ninachangamoto hii.Nilishawahi kuwa kwenye mahusiano na mtoto wa k**e ambaye nilimpenda sana na yeye alinipend...
14/09/2026

Mkuu mimi ninachangamoto hii.Nilishawahi kuwa kwenye mahusiano na mtoto wa k**e ambaye nilimpenda sana na yeye alinipenda kweli na tuliishi kwenye mahusiano since 2022-2025 lakini ilifika wakati nilipitia changamoto katika safari yangu ya elimu ambayoilipelekea mimi kusimamisha masomo lakini sikumwambia na hakuwa akifahamu hili kwasababu tulikuwa tukiishi sehemu tofauti lakini baada ya muda nilirejea masomoni kwaajili ya kuendelea na masomo ambapo ulikuwa muda ambao ningetakiwa nimalize Masomo na yeye alitegemea nimalizie kwani hakuwa akijua yote yaliyonikuta. Mwalimu mimi nafsi ikawa inaniuma nashindwa kumwambia ukweli mpaka ikafikia wakati nikajikuta nimekuwa kimya coz najisikia vibaya kutokumweka wazi na mwisho nikaamua kuwa kimya lakini aliumia na alihangaika sana kuhakikisha ananipata lakini mimi nilinyamaza ni mwaka sasa umepita najikuta nashtuka na namkumbuka sana Mwalimu nifanyeje Mwalimu wangu na kiukweli bado nampenda sana.

Mwisho.

K**a una mkasa wowote, au changamoto unahitaji ushauri binafsi

Wasiliana nami kupitia WhatsApp.

0655 653 744

Save then nitumie ujumbe anza kwa kujitambulisha (jina na mahali ulipo).

Mimi ni Patrick Keha

Kuolewa na mtu sahihi ukiwa na miaka 35 ni bora kuliko kuolewa kwa mtu asiye sahihi ukiwa na miaka 20.Presha ya jamii, m...
14/09/2026

Kuolewa na mtu sahihi ukiwa na miaka 35 ni bora kuliko kuolewa kwa mtu asiye sahihi ukiwa na miaka 20.

Presha ya jamii, marafiki, au familia, usiruhusu kamwe vikutoe kwenye utulivu wa kuiamua kesho yako.

Chelewa usipotee, kuliko kuwahi halafu ukapotea.

Unaifahamu hii mbegu?Je, umewahi kula?Ilikuwaje?Wazoefu tupeni uzoefu😂
12/09/2026

Unaifahamu hii mbegu?
Je, umewahi kula?
Ilikuwaje?

Wazoefu tupeni uzoefu😂

DARASA HURU
12/09/2026

DARASA HURU

MAMBO 7 AMBAYO UNAPASWA KUJIFUNZA KUYAKUBALI ILI UWE NA AMANIAmani ya moyo Inaanza pale unapokubali ukweli ambao huwezi ...
11/09/2026

MAMBO 7 AMBAYO UNAPASWA KUJIFUNZA KUYAKUBALI ILI UWE NA AMANI

Amani ya moyo Inaanza pale unapokubali ukweli ambao huwezi kuubadilisha.

Kuna uchovu ambao hausababishwi na ugumu wa kazi.

Unasababishwa na kupigana kila siku na jambo ambalo tayari limeshatokea, mtu ambaye hataki kubadilika, au hali ambayo haiko ndani ya uwezo wako.

Mfano, kutaka kila kitu kiende k**a ulivyopanga. Unataka watu wakuelewe.

Unataka waliokuumiza wajute. Unataka yaliyopita yarudi na yawe tofauti. Lakini maisha hayafanyi kazi hivyo.

Wakati mwingine amani haiji kwa kubadilisha hali yako; inakuja kwa kubadilisha namna unavyoikabili.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo unapaswa kujifunza kuyakubali.

1. KUBALI KWAMBA SIO KILA MTU ATAKUELEWA

Unaweza kuwa na moyo mzuri, lakini bado kuna watu watakuelewa vibaya.

Unaweza kuwa mwaminifu, lakini bado mtu akakuita mwongo.

Unaweza kufanya jambo kwa nia njema, lakini mtu mwingine akaliona kwa namna tofauti.

Usitumie muda mwingi kujaribu kujielezea kwa kila mtu, Kuna watu watakuelewa kwa uzoefu wao, badala ya ukweli wako.

Muhimu ni Fanya yaliyo sahihi, Eleza pale inapohitajika.

Lakini baada ya hapo, ruhusu kila mtu awe na mtazamo wake, Amani inaanza kutawala pale unapogundua kwamba sio jukumu lako kudhibiti kila mtu anavyokufikiria.

2. KUBALI KWAMBA BAADHI YA WATU WATAONDOKA KWENYE MAISHA YAKO

Hili ni gumu.

Unawapenda baadhi ya watu na unatamani wabaki nawewe.

Lakini maisha huwa yanabadilika, Watu wanabadilika. Mahusiano yanabadilika.

Na wakati mwingine mtu ambaye uliamini angekuwa sehemu ya maisha yako kwa muda mrefu anaondoka.

Sasa Usitumie nguvu kubwa kumlazimisha abaki, Mtu akichagua kuondoka mwache aende, huwezi kujenga amani kwa kumlazimisha akae mahali ambapo ameshakuonyesha hataki tena kuwepo.

Mshukuru kwa yale mema mliyoshirikiana, Jifunze kutokana na yaliyotokea.

Kisha endelea.

Namna nyingine ya kumuonyesha mtu unampenda, ni kumruhusu aende mahali anakohisi atapata amani zaidi ya ile anayoipata kwako.

3. KUBALI KWAMBA YALIYOPITA HAYAWEZI KUBADILISHWA

Kuna mambo unayakumbuka na kutamani ungefanya tofauti.

Labda ulifanya uamuzi mbaya, Labda ulimwamini mtu ambaye hakustahili kuaminiwa, Labda ulipoteza nafasi.

Labda ulikaa mahali ulipopaswa kuondoka mapema, Lakini jana haiwezi kurudi ili urekebishe.

Unachoweza kufanya ni kujifunza kutokana na jana ili usiharibu kesho kwa kosa lilelile.

Usiendelee kujihukumu kwa mtu ambaye ulikuwa kabla hujapata maarifa uliyonayo leo.

Usijichukie kwa sababu ya makosa ambayo yalikufundisha kuwa mtu mwenye hekima zaidi, Kubali yaliyopita, Jifunze. Kisha Endelea.

4. KUBALI KWAMBA HUWEZI KUMBADILISHA KILA MTU

Unaweza kumshauri mtu, Unaweza kumpenda.
Unaweza kumweleza ukweli, Unaweza kumpa nafasi nyingi.

Lakini huwezi kumlazimisha mtu abadilishe tabia ambayo yeye mwenyewe hataki kuibadilisha.

Hili ni jambo ambalo watu wengi huwa wanachelewa kulielewa.

Mwanangu, upendo unaweza kumsaidia mtu kubadilika, lakini huwezi kubadilika kwa niaba yake, Usibebe jukumu ambalo sio lako, Mtu mzima anawajibika kwa maamuzi yake, Wewe wajibika kwa yako. Hapo utapata amani.

5. KUBALI KWAMBA MAISHA HAYATAENDA KILA MARA K**A ULIVYOPANGA.

Unaweza kupanga vizuri na bado mambo yakabadilika.

Unaweza kufanya kazi kwa bidii na mafanikio yakachelewa. Unaweza kuwa na nia nzuri na ukakutana na changamoto.

Hii haimaanishi maisha yamekugomea, Inamaanisha tu kwamba huwezi kudhibiti kila kitu.

Usijiteshe kwa sababu maisha yamechelewa kwenda unavyotaka, Sio kila kitu kitakwenda kwa mpango wako. Lakini bado unaweza kuishi kwa hekima ndani ya hali uliyopewa.

6. KUBALI KWAMBA HUWEZI KUPENDWA NA KILA MTU

Usijaribu kuwa mtu wa kumfurahisha kila mtu, Ukiishi hivyo, utaanza kufanya maamuzi kwa kuogopa watu watasema nini.

Utavaa ili uwafurahishe, Utaishi kwa namna wanayotaka, Utakataa kile unachotaka kwa sababu unaogopa kukataliwa.

Mwisho wake utakuwa na watu wengi wanaokupenda kwa sababu unawafurahisha, lakini wewe mwenyewe utakuwa umeshajipoteza.

Jua thamani yako, Heshimu watu, Fanya yaliyo sahihi. Lakini usiuze amani yako ili ununue kukubalika kwa watu.

7. KUBALI KWAMBA WEWE MWENYEWE BADO UNAKUA.

Usiamini umefika.

Bado una mambo ya kujifunza, Bado unaweza kukosea, Bado unaweza kubadilisha mtazamo, Bado kuna tabia unatakiwa kuziacha.

Na hilo sio udhaifu, Ni sehemu ya kuwa binadamu, Usijilazimishe kuwa mkamilifu ili ujione una thamani. Jifunze kuwa mtu bora kuliko ulivyokuwa jana.

K**a leo umeona kosa ambalo jana hukuliona, hiyo ni hatua, K**a leo umejifunza kusema “hapana” mahali ambapo zamani uliogopa, hiyo ni hatua.

K**a leo umeanza kujiheshimu zaidi, hiyo ni hatua, Maisha hayahitaji uwe mkamilifu; yanahitaji uwe tayari kujifunza na kukua.

Mwisho Kabisa..

Mwanangu, amani ya moyo haimaanishi kwamba maisha hayatakuwa na matatizo.

Inamaanisha umejifunza kutoruhusu kila tatizo likuvuruge.

Kuna mambo utayarekebisha, Kuna mambo utayaacha, Kuna watu utawasamehe, Kuna watu utawaacha waende, Kuna mambo utayapigania.

Na kuna mambo utasema:

“Hili siwezi kulibadilisha, kwa hiyo sitapoteza amani yangu kulipigania.

Huo ni ukomavu.

Kwa sababu kuna wakati ushindi sio kupata unachotaka.

Ushindi ni kufika mahali ambapo jambo lililokuwa linakutesa halina tena uwezo wa kukutawala.

Kubaliana na ukweli, Jifunze, Achilia yasiyokuwa mikononi mwako.

Kisha endelea na maisha yako.

Amani inaanza pale unapokoma kupigana na mambo ambayo huwezi kuyabadilisha.

━━━━━━━━━━━━━━

Mimi naitwa, Patrick Keha.

Mwalimu wa Mahusiano, Uchumba na Ndoa.

Karibu kwenye WhatsApp Status yangu kupata mafunzo ya kila siku BURE kuhusu Mahusiano, Uchumba na Ndoa.

WhatsApp: 0655 653 744

Save namba yangu, kisha nitumie majina yako mawili ili nami niweze kukuhifadhi.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Patrick Keha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share