
03/07/2025
MSAGASUMU AFARIKI KWA AJALI DODOMA
Mchezaji wa zamani wa soka Tanzania SELEMANİ MSAGASUMU amefariki kwa ajali usiku wa kuamkia leo tarehe 3 Julai 2025. Msagasumu alikuwa anaendesha pikipiki ambayo iligongana na gari na kupelekea umauti wake papo hapo, Dereva wa gari anashikiliwa na Polisi ilihali mwili wa marehemu ukiwa hospitali ya Mkoa. Katika uhai wake Msagasumu amewahi kuzichezea timu kadhaa ikiwemo CDA ya Dodoma (Watoto wa Nyumbani) lakini alikuwemo kwenye timu ya Taifa ya vijana U20 (Ngorongoro Heroes) mwaka 1999 .
SISI NI WA ALLAH NA HAKIKA KWAKE NI MAREJEO YETU.
Pumzika Sele mpaka wakati mwingine!