
06/08/2025
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai, ame fariki dunia leo Agosti 6, 2025 akiwa anapatiwa matibabu hospitalini baada ya kuugua ghafla.
Marehemu Ndugai alizaliwa Januari 22, 1960 na alihudumu k**a Spika wa Bunge kuanzia Novemba 17, 2015 hadi alipojiuzulu Januari 6, 2022. Baada ya kujiuzulu, aliendelea kuwa Mbunge wa Kongwa, nafasi aliyohudumu akitimikia hadi mauti ilipomkuta.
Mwaka huu, Ndugai alishiriki katika kura za maoni za ubunge na kuibuka mshindi kwa kupata kura 5,690, akiendeleza kutetea nafasi yake ya ubunge kwa kipindi kingine.