nLink TV

nLink TV Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from nLink TV, Media/News Company, Dar es Salaam.

Ili upate habari, burudani, mahojiano ya kipekee na vipindi vinavyogusa maisha ya kila siku – follow kurasa zetu kwa jina la nlinktv:

YouTube 👉 g24tv

Facebook 👉 g24tv

Instagram 👉

TikTok 👉

X (Twitter) 👉

26/10/2025

KAULI YA ASKOFU GWAJIMA KWA TAIFA NA VIONGOZI

26/10/2025

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi, Uwajibikaji na Mahusiano kutoka Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Leila Riyaz Bhanji, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025 na kuendelea kulinda amani ya nchi.

Akizungumza leo Oktoba 26, 2025 katika Kongamano la Wanawake wa Dar es Salaam lililofanyika katika ukumbi wa DYCC Chang’ombe, Bhanji amesema ni wajibu wa kila Mtanzania kuilinda amani na kuepuka kushawishiwa kushiriki maandamano ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa utulivu.

“Tusipokuwa na amani, Tanzania itakuwa tofauti sana. Wanaotuhamasisha kuandamana wapo nje ya nchi na familia zao. Ni muhimu sisi tuliopo humu ndani kuilinda nchi yetu,” alisema Bhanji.

Aidha, ametoa wito kwa vijana kuepuka mihemko, lugha za fedheha dhidi ya viongozi na vitendo vinavyoashiria chuki, akisisitiza kuwa uchaguzi ni tukio la kidemokrasia lisilotakiwa kugeuzwa chanzo cha machafuko.

Kongamano hilo limejadili faida na changamoto za uchaguzi likiongozwa na kaulimbiu isemayo: “Usipomchagua unayemtaka, utachaguliwa usiyemtaka.” Washiriki wametakiwa kuhamasisha wengine kushiriki kupiga kura pamoja na kuomba amani kuelekea uchaguzi mkuu.

26/10/2025

Dar es Salaam, Oktoba 26, 2025 — Jeshi la Polisi Tanzania limeonya vikali watu wote wanaopanga kuvunja sheria au kuhatarisha amani katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, likisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa bila upendeleo, huruma au kusita.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumapili, Msemaji wa Jeshi hilo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, amesema wananchi wamepewa elimu ya kutosha kuhusu wajibu wao wa kudumisha amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi, hivyo hakuna kisingizio kwa yoyote kufanya fujo au uvunjifu wa sheria.

“Tumeendelea kutoa elimu ya uraia na ya kutii sheria kwa muda mrefu kupitia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara na njia nyingine mbalimbali. Hakuna sababu ya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki muhimu,” alisema DCP Misime.

Aidha, amewatoa hofu wananchi wanaotarajia kujitokeza kupiga kura, akibainisha kuwa usalama umeimarishwa kwenye vituo vyote vya kupigia kura nchini, na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi wakitekeleza haki yao ya kikatiba kwa utulivu.

DCP Misime pia ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wageni waliopo na wanaoendelea kuwasili nchini kuwa Tanzania itaendelea kuwa “kisiwa cha amani”, akisema uchaguzi wa mwaka huu utaendeshwa kwa utulivu k**a ilivyoshuhudiwa katika chaguzi zilizopita.

Jeshi la Polisi limehitimisha kwa kusisitiza kuwa halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu, kikundi au taasisi yoyote itakayojaribu kuvuruga mchakato wa uchaguzi au kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza kusikitishwa na chapisho jipya la Amnesty International lenye kichw...
26/10/2025

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza kusikitishwa na chapisho jipya la Amnesty International lenye kichwa “Unopposed, Unchecked, Unjust: ‘Wave of Terror’ Sweeps Tanzania Ahead of 2025 Poll”, ikisema kuwa limejaa madai makubwa yasiyo na uthibitisho.

Kupitia taarifa yake kwa umma, Serikali imesema Tanzania inaendelea kuwa taifa lililo tayari kushirikiana na wadau wa kimataifa katika kuimarisha demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria, lakini imeeleza masikitiko yake kwamba Amnesty International ilichapisha tuhuma hizo bila kulipa Serikali nafasi ya kutosha kujibu kabla ya taarifa hiyo kwenda kwa umma.

“Ni jambo la kusikitisha kuona shirika hili limeamua kutoa taarifa zenye tuhuma nzito bila kuzingatia misingi ya usawa, ukweli na maadili ya mazungumzo ya kimataifa kuhusu haki za binadamu,” imeeleza Serikali katika taarifa hiyo. Aidha, imesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kulinda usalama wa raia wake na kuheshimu misingi ya haki kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

Serikali pia imezitaka taasisi na mashirika ya kimataifa kushirikiana kwa misingi ya ukweli, heshima na majadiliano jumuishi badala ya kuchapisha taarifa zinazoweza kupotosha na kudhoofisha taswira ya taifa.

Dar es Salaam, Ijumaa, Oktoba 24, 2025 — Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kuhusu kimbunga cha kit...
24/10/2025

Dar es Salaam, Ijumaa, Oktoba 24, 2025 — Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kuhusu kimbunga cha kitropiki Chenge, ambacho kinatarajiwa kusababisha mvua kubwa, upepo mkali na mawimbi makubwa ya baharini katika maeneo ya ukanda wa pwani kuanzia tarehe 26 hadi 28 Oktoba.

Kwa mujibu wa taarifa ya TMA iliyotolewa Ijumaa, Oktoba 23, 2025, madhara ya mfumo huo yanatarajiwa kuathiri mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na Tanga, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, ambapo mvua kubwa zinatarajiwa kuambatana na mawimbi yenye urefu wa hadi mita kadhaa na upepo mkali wa baharini.

> “Uchambuzi wa mifumo ya utabiri wa hali ya hewa unaonesha kuwa mfumo huo utaendelea kusogea upande wa magharibi huku nguvu yake ikipungua taratibu unapoelekea mwambao wa Tanzania. Hata hivyo, utaongeza mvua, upepo mkali na mawimbi makubwa katika kipindi cha Oktoba 26 hadi 28,” ilisema TMA.

TMA ilieleza kuwa kufikia Ijumaa asubuhi, dhoruba hiyo ilikuwa katika kaskazini-mashariki mwa Madagascar, takribani kilometa 1,680 kutoka pwani ya Mtwara, ikisogea kuelekea magharibi kupitia Bahari ya Hindi.

Wananchi wa maeneo husika wametakiwa kuchukua tahadhari, hasa wavuvi, waendesha mitumbwi, wasafiri wa baharini na wakazi wa maeneo ya mabondeni yanayopata mafuriko mara kwa mara

  BONYEZA LINK HII KUFATILIA MOJA KWA MOJA KESI INAYO MKABILI MWENYEKI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (  ) LIVE
18/08/2025

BONYEZA LINK HII KUFATILIA MOJA KWA MOJA KESI INAYO MKABILI MWENYEKI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO ( ) LIVE

...........Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii►YOUTUBE: nlink TV►INSTAGRAM: nlink TV►TWITTER: nlink TV►FACEBOOK: nlink TV #...

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when nLink TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share