CF Media

CF Media Your trusted source for | Sports | Business | Politics | Entertainment | Youtube, tiktok, Instagram

29/09/2026

...

29/09/2026

Kajala amefunguka kuhusu uhusiano wake na Harmonize, akisema kurudi kwake hakukutokana na kukosa sehemu ya kwenda au mtu wa kumpenda. Amesema sababu kubwa ni kwamba akiwa na Harmonize anajisikia kuwa comfortable na amani.

29/09/2026

Zaiylissa amefunguka kuhusu suala la uke mwenza, akisisitiza kuwa hajawahi kuwa mke mwenza na hana mpango wa kuingia kwenye aina hiyo ya ndoa. Amesema ndoa aliyonayo kwa sasa ndiyo ndoa yake ya kwanza na mume wake, huku akieleza wazi kuwa hawezi na hatakuja kuwa tayari kuwa mke mwenza.

29/09/2026

Hali katika Stendi ya Mabasi ya Magufuli jijini Dar es Salaam imeathiriwa na mgomo wa madereva wa mabasi yanayofanya safari za mikoani.

Madereva hao wameamua kusitisha huduma wakipinga mfumo mpya unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani, unaowezesha kukatwa pointi kwenye leseni zao za udereva wanapobainika kufanya makosa ya barabarani.

Kuna baadhi ya couple ambazo unapoziona kwenye picha, huwezi kuona uzuri wa muonekano pekee, bali pia unaona ukaribu, he...
29/09/2026

Kuna baadhi ya couple ambazo unapoziona kwenye picha, huwezi kuona uzuri wa muonekano pekee, bali pia unaona ukaribu, heshima na furaha wanayooneshana. Tanzania kuna couple ya Ricardo Momo na mkewe ambayo imeendelea kuvutia watu kutokana na namna wanavyoonekana kuwa karibu na kufurahia kuwa pamoja.

Jina “Thunai Min Al-Jannah” kwa lugha ya Kiarabu humaanisha “wawili kutoka peponi”, kauli ambayo imekuwa ikitumika kuelezea taswira ya Ricardo Momo na mkewe kutokana na namna wanavyoonekana kwenye picha zao. Wawili hao wameendelea kuonesha mshik**ano na heshima katika safari yao ya pamoja.

Kwa mtazamo wa mashabiki wao, Ricardo Momo na mkewe ni miongoni mwa couple zinazovutia Tanzania, huku picha zao zikionesha ukaribu na furaha wanayoshirikiana. Je, unawaona k**a couple yenye muonekano wa “made in heaven” Tanzania?

29/09/2026

Mtalii aliyekuwa ndani ya gari amekutana na wakati wa kushtua baada ya chui kusogea karibu na dirisha la gari. Wakati mtalii huyo akijaribu kufunga kioo, chui aliingiza mkono wake ndani kupitia dirishani na kumfanya mtalii huyo asite kuendelea kufunga kioo.

Tukio hilo limevutia hisia kwenye mitandao ya kijamii, likionyesha namna wanyama pori wanavyoweza kusogea karibu na magari wakati wa safari za kutazama wanyamapori.

29/09/2026

Tukio la kushtua limetokea jioni ya Septemba 26, 2026 katika Lingnan Impression Park, Guangzhou nchini China, baada ya msanii wa k**e kuanguka kutoka juu wakati akiendelea na onyesho la “Chang’e Flying to the Moon”.

Msanii huyo alikuwa akifanya sarakasi akiwa juu ya kifaa cha duara kilichoning’inizwa hewani, lakini ghafla alianguka kutoka urefu wa zaidi ya mita 10, hali iliyowafanya watazamaji kupiga kelele kwa hofu. Baada ya tukio hilo, alikimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Mamlaka zilisema msanii huyo alipata jeraha la kuvunjika sehemu ya chini ya mguu, lakini hali yake ilikuwa imara na hakukuwa na hatari ya moja kwa moja kwa maisha yake. Sehemu ya onyesho hilo la sarakasi za angani imesimamishwa kwa muda huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.

29/09/2026

Watoto kutoka Uganda wanaounda kikundi cha Triplets Ghetto Kids wamepata nafasi ya kuonekana kwenye jukwaa la kimataifa baada ya kufanya onyesho pamoja na mwanamuziki wa kimataifa, Shakira, mjini Madrid nchini Hispania.

Kikundi hicho kilialikwa kushiriki katika onyesho la Shakira lililofanyika mwishoni mwa wiki, ambapo watoto hao walipanda jukwaani na msanii huyo na kuonyesha uwezo wao wa kucheza sambamba na wimbo “Dai Dai”.

Ushiriki wao unakuja baada ya Shakira kutoa ahadi ya kufanya kazi pamoja na watoto hao, kufuatia kuvutiwa na kipaji chao walipokutana wakati wa michuano ya Kombe la Dunia 2026.

29/09/2026

Tukio la kushangaza lilitokea mwaka 2013 nchini Bulgaria wakati mwanasiasa Ahmed Dogan alipokuwa akihutubia mkutano wa chama chake cha MRF. Akiwa jukwaani, Oktay Enimehmedov alipanda na kumwelekezea Dogan bastola iliyokuwa ikionekana k**a yenye risasi, lakini bastola hiyo iligoma kupiga.

Enimehmedov alidhibitiwa mara moja na watu waliokuwa karibu na jukwaa. Uchunguzi wa baadaye ulibaini kuwa bastola hiyo ilikuwa ya gesi na ilikuwa imejazwa risasi zisizoweza kufyatua. Enimehmedov alik**atwa na baadaye kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka mitatu gerezani.

Address

Mandela Road, Ubungo
Dar Es Salaam
2555

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when CF Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share