03/10/2026
Islam Channel imetangaza washindi wa Tuzo za Biashara za mwaka 2026 (Islam Channel Business Awards), zinazotambua mafanikio, ubunifu na mchango wa wafanyabiashara katika jamii ya Waislamu.
Miongoni mwa makampuni yaliyoibuka na ushindi ni DigiLite iliyotwaa tuzo ya biashara changa, ICCO Pizza katika biashara za kifamilia, Mubarak London kwa biashara ndogo, EaseFix katika biashara za ukubwa wa kati na Caprinos Pizza katika biashara kubwa.
Washindi wengine ni ARC Aero Systems katika sekta ya teknolojia, Foodery katika sekta ya chakula na vinywaji, Smoke & Pepper katika biashara za Franchise, Batley Law katika huduma za kitaalamu na Muslim Ski Club katika sekta ya utalii.
Aidha, Tiles DIY ilishinda katika biashara za rejareja, Ibn Sina Sanctuary katika biashara zinazoongozwa na wanawake, Kestrl katika huduma za kifedha, Offa katika sekta ya ardhi na majengo, huku Inspire Capital Sports ikitambuliwa kwa mchango wake kwa jamii.
Katika tuzo maalumu, Qamer Khan na Rashid Khan wa K Furniture na K Lives Foundation walipokea tuzo ya waanzilishi, huku S Mohammad Khalid wa Euro Quality Lamb akitunukiwa tuzo ya mafanikio ya maisha katika biashara.
Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango wa wafanyabiashara, makampuni na wajasiriamali katika kukuza uchumi, kuleta ubunifu na kutoa fursa mbalimbali ndani ya jamii.