
04/09/2025
Mwamba anaondoka taratibu kwenye ramani ya media zenye credibility.
Huyu kijana alihamasisha vijana wengi waamini kufanikiwa kunawezekana, na wengi wakafika mbali kwa kuamini mfano wa Millard Ayo, aliyefanikisha zaidi upande wa digital media.
Kwa sasa amekuwa k**a Zuwena kwa Mondi, sio yule tena. Simlaumu kabisa homeboy.
Ukitaka credibility kwa public na ukakosana na stakeholders wenye nguvu, unaweza kutolewa kabisa kwenye system.
Katika nchi nyingi za ulimwengu wa tatu survival inahitaji balance.
Watu watakupa sifa, lakini wakisha kukatisha supply chain yao, wanaendelea na shughuli zao.
Kila uamuzi unaoenda tofauti na stakeholder mkubwa wa industry unahitaji assessment ya risk kwa kiwango cha mtu binafsi.
Kuwa trusted media is possible, lakini gharama yake ni kupoteza investment ya miaka mingi.
Swali ni je, kuna mtu atakayekubali kupoteza kile alichokijenga kwa miaka mingi? Jibu ni hapana.
Hakuna mtu mwenye akili ya biashara atakubali hasara ya moja kwa moja kwa sababu ya public perception.
Hakuna media house inayoweza kufanya kazi nje ya regulatory framework. Zote ziko ndani ya mfumo wa sheria za nchi.
Media ikichagua content ya ku-publish au ku-suppress, hiyo ni survival strategy na pia ni biashara.
Ikiwa uamuzi wa ku-publish unahatarisha sustainability ya kampuni, kuepuka ni chaguo la lazima.