25/04/2025
*Mwaliko wa Mazungumzo ya Uratibu wa Sanaa na Laura Gamba hapa KokoTEN Studio*
KokoTEN Studio inapenda kuwaalika wasanii, wakurugenzi wa sanaa, na wadau wa sekta ya ubunifu kushiriki katika mazungumzo ya kiuratibu na *Laura Gamba*, Mkurugenzi Mkuu wa Creative Lounge Trust kutoka Zimbabwe.
Laura ni mtaalamu wa sanaa mwenye uzoefu mkubwa katika kuratibu, kutafiti, na usimamizi wa sanaa. Ameongoza miradi mbalimbali ya sanaa inayolenga masuala ya kijamii na mazingira, ikiwa ni pamoja na maonyesho ya "Art and Ecology" yaliyofanyika Harare, Zimbabwe, ambayo yalilenga kuhamasisha uelewa wa mazingira kupitia sanaa.
*Taarifa za Tukio:*
- *Tarehe:* Jumamosi, Aprili 26, 2025
- *Muda:* Saa 10 Jioni
- *Mahali:* KokoTEN Studio, Dar es Salaam
Katika mazungumzo haya, Laura atatupatia uzoefu wake katika kuratibu sanaa, kazi anazofanya nchini Zimbabwe, na fursa zinazoweza kuwasaidia wasanii wa Kitanzania kupitia ushirikiano wa kimataifa. Ziara yake nchini Tanzania ni sehemu ya mradi wa ukuratibu aliouanzisha baada ya kushiriki katika Tamasha la Sanaa la Glasgow mwaka 2024, kwa msaada wa British Council.
Tukio hili ni fursa adhimu kwa wasanii na wadau wa sanaa kujifunza na kubadilishana mawazo kuhusu ukuratibu wa sanaa na ushirikiano wa kimataifa.
______________________
*Join Us for a Curatorial Talk with Laura Gamba at KokoTEN Studio*
Dear Art lovers,
We are delighted to invite you to an insightful curatorial talk by *Laura Gamba*, Principal Director of Creative Lounge Trust in Zimbabwe. Laura is a distinguished curator, researcher, and arts manager, known for her extensive work in contemporary African art. Her visit to Dar es Salaam is part of a curatorial project initiated after her participation in the Glasgow Art Festival in 2024, supported by the British Council.
*Event Details:*
- *Date:* Saturday, April 26, 2025
- *Time:* 4pm to 6pm
- *Venue:* KokoTEN Studio, Dar es Salaam
During the talk, Laura will share her experiences and the impactful work she is doing in Zimbabwe. She will also discuss opportunities for Tanzanian artists to engage in collaborative projects and cultural exchanges.
studio