13/10/2025
Nguzo za ibada ya Umrah (أركان العمرة) ni mambo muhimu ambayo yakikosekana Umrah haikamiliki. Kuna nguzo kuu nne:
🕋 Ihram (الإحرام)
Ni kuingia katika hali ya ibada kwa nia maalum ya kutekeleza Umrah.
Hapa mtu hutoa nia ya Umrah akiwa katika moja ya miqat (eneo la mipaka ya kuhirimia).
"Labbaika ‘Umratan” – Ee Mola, nimeitikia kufanya Umrah.
🔄 Tawaf (الطواف)
Ni kuzunguka Kaaba mara saba ukiwa katika hali ya ibada, kuanzia kwenye Hajar al-Aswad (Jiwe Jeusi).
Unazunguka ukiweka Kaaba upande wa kushoto.
Tawaf ni alama ya kuonyesha utiifu na upendo kwa Mwenyezi Mungu.
🏃♂️ Sa’i baina ya Safa na Marwa (السعي بين الصفا والمروة)
Ni kutembea au kukimbia kidogo kati ya vilima viwili vya Safa na Marwa mara saba.
Hii ni kumbukumbu ya safari ya Hajar (mke wa Nabii Ibrahim) alipokuwa akitafuta maji kwa mwanawe Ismail.
✂️ Kukata au kunyoa nywele (الحلق أو التقصير)
Ni ishara ya kukamilika kwa ibada ya Umrah.
Wanaume hunyoa au hukata nywele, wanawake hukata kipande kidogo cha nywele zao (kidogo kutoka kila upande).
=========================================
Karibu IBN BATUTA TOURS LTD kwa safari za Ibada ya Hijja na Umrah Makkah na Madina. Wasiliana nasi 0752 950 350