DIRA YA LEO

DIRA YA LEO Politics | Social | Economics | Sports | Entertainment; Accurate news at the right time.

Kwamba vitambulisho vya taifa 2,027,103 vilivyozalishwa na kufikishwa katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ...
18/09/2026

Kwamba vitambulisho vya taifa 2,027,103 vilivyozalishwa na kufikishwa katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) havijachukuliwa na wananchi, ni habari mbaya na inadhoofisha kazi nzuri ya serikali ya utambuzi wa watu wake.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi idadi hiyo ni sehemu ya vitambulisho vilivyozalishwa baada ya wananchi kukamilisha usajili.

Katambi amesema hadi sasa watu 27,520,835 wamesajiliwa, wakati 23,515,667 wakiwa na namba za utambulisho na vitambulisho 21,526,635 vikiwa vimezalishwa.

Tumesikitishwa na idadi hii ya watu 2,027,103 ambao hawajachukua vitambulisho vyao kutokana na ukweli kuwa kitambulisho cha NIDA ni muhimu. Tunasema hivyo kwa sababu ya umuhimu wa utambulisho katika masuala ya ulinzi na usalama.

Matumizi ya vitambulisho yanaweza kusaidia kutambua watu waliopo katika maeneo mbalimbali na hivyo kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao.

Vitambulisho pia ni muhimu katika kutambua mtu anaposafiri na hata anapofika katika sehemu za malazi ili kurahisisha utambuzi wao na kusaidia mamlaka pale zinapohitaji kufuatilia matukio ya kiusalama.

Vitambulisho kikiwamo cha NIDA vimesaidia kutambuana, kuzuia uhalifu na ni moja ya hati zinazosaidia kuboresha masuala mengi ya kitaifa kwa kuzingatia idadi ya watu na hasa wenye utambuzi k**a huo.

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeanza kutumia technolojia ya kisasa kutoa matibabu ya kibingwa ya ...
17/09/2026

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeanza kutumia technolojia ya kisasa kutoa matibabu ya kibingwa ya upasuaji wa ubongo kwa wagonjwa wa kiharusi inayongeza ufanisi wa matibabu Kwa wagonjwa.

Mkurugenzi wa Upasuaji wa Ubongo MOI Dkt. Lemeri Mchome amesema leo Septemba 17, 2026 kuwa technolojia hiyo ni ya kwanza kutumika nchini na kwamba inakwenda kuleta mapinduzi katika matibabu ya kiharusi.

"Tunatoboa tundu ndogo kichwani na tunapitisha kifaa maalum chenye kamera, Ile kamera inakwenda kutuonyesha eneo ambalo damu imevilia na kutuwezesha kuitoa bila kuathiri sehemu nyingine" amesema Dkt. Lemeri

"Hii ndiyo teknolojia ya kisasa zaidi duniani na sisi k**a taasisi hatuko nyuma, wagonjwa wa kiharusi hawana sababu ya kukimbilia nje ya nchi Kwa matibabu, huduma hiyo inapatikana MOI...kwasasa tunapokea wagonjwa watatu hadi watano Kwa siku, teknolojia hii inakuwa msaada wa matibabu bora" ameongeza

Naye Daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo MOI, Dkt. John Mtei ambaye ameshiriki katika upasuaji wa kwanza kwa kutumia kifaa hicho amesema technolojia hiyo inaacha alama katika mapinduzi ya tiba ya Kiharusi nchini.

"Ufanisi wa matibabu ndiyo nyenzo muhimu katika matumizi ya technolojia hii, mgonjwa anafanyiwa upasuaji na kuondolewa tatizo lake kwa uhakika" amesema Dkt. Mtei

Taasisi ya MOI imeendelea kujikita katika kuleta afua mbalimbali hapa nchini za kuipunguzia Serikali mzigo wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa rufaa za gharama kubwa na pia kuendelea kuwa kituo cha weledi cha matibabu ya Mifupa na mfumo wa fahamu barani Afrika.

Rais wa Cameroon, Paul Biya, ameondoka tena nchini humo kuelekea Ulaya, wiki chache tu baada ya kurejea nyumbani kea zia...
16/09/2026

Rais wa Cameroon, Paul Biya, ameondoka tena nchini humo kuelekea Ulaya, wiki chache tu baada ya kurejea nyumbani kea ziara.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 93 alirejea nchini humo mnamo Agosti 20 baada ya kukaa Ulaya kwa siku 73.

Kuondoka kwake hivi karibuni kunakuja baada ya kukaa kwa muda mfupi tu nchini Cameroon.

Kutokuwepo kwa Biya nchini kwa muda mrefu kumevutia hisia za wengi, hasa baada ya kukaa kwake nje ya nchi kwa siku 73 mapema mwaka huu

“Mimi nashangaa, mtu ambaye amewahi kuwa Rais wa Kenya, unaacha kiti cha urais, badala ya kwenda kuwa kiongozi mstaafu m...
16/09/2026

“Mimi nashangaa, mtu ambaye amewahi kuwa Rais wa Kenya, unaacha kiti cha urais, badala ya kwenda kuwa kiongozi mstaafu mwenye hekima, unaenda kuwa kiongozi wa uasi, kiongozi wa upinzani. Mpaka sasa mahak**a inamwambia aondoke […] K**a Uhuru Kenyatta hakunishinda akiwa Rais, atanishinda wakati huu kweli?” - William Ruto, Rais wa Kenya

16/09/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Tanzania imepiga hatua katika mapambano dhidi ya saratani, kufuatia uwekezaji wa Serikali katika kinga, uchunguzi na matibabu, huku ikilenga kuongeza huduma hizo na kujijenga kuwa kitovu cha utaalamu na mafunzo ya tiba ya saratani kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Makamu wa Rais, amesema hayo wakati akihutubia Jukwaa la Kisayansi la Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA Scientific Forum) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, linalofanyika Vienna nchini Austria.

Amesema chini ya uongozi wenye maono na dhamira thabiti ya kisiasa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, sekta ya afya imeendelea kuwa kipaumbele cha kitaifa, jambo linalodhihirishwa na maendeleo yaliyopatikana katika nyanja za kinga, utambuzi na matibabu ya saratani kuanzia ngazi ya msingi hadi ngazi ya juu ya huduma za afya.

Makamu wa Rais, ametaja hatua mbalimbali za mafanikio zilizofikiwa na Tanzania, k**a kuongezeka kwa utoaji wa chanjo ya dozi moja dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa wasichana wenye umri wa miaka tisa hadi 14, kutoka asilimia 58 mwaka 2018 hadi asilimia 98 mwaka 2026, kuongezeka kwa vituo vinavyotoa tiba ya saratani kwa mionzi (radiotherapy) kutoka vitatu mwaka 2020 hadi sita mwaka 2026, hatua iliyoongeza upatikanaji wa huduma hiyo kutoka asilimia 14 hadi asilimia 26 na kunufaisha wagonjwa wapatao 6,500.

Amesema Serikali imelenga kufikisha vituo tisa vya huduma jumuishi za saratani katika kanda sita za kimkakati Tanzania Bara na Zanzibar ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kusogeza huduma za kibingwa karibu zaidi na wananchi. Hatua hiyo inaenda sambamba na uwekezaji mkubwa katika teknolojia za kisasa za uchunguzi na matibabu.

Aidha, Makamu wa Rais amesema, Tanzania imeanza kutumia mashine ya PET-Scan inayounganishwa na cyclotron, kifaa maalumu kinachowezesha uzalishaji wa isotopu za mionzi zinazotumika katika uchunguzi wa kisasa, na kuwa miongoni mwa nchi 10 za kwanza barani Afrika kutoa huduma hiyo.

“Kati ya mwaka 2021 na 2026, idadi ya mashine za MRI imeongezeka kutoka saba hadi 28, LINAC kutoka mbili hadi nane, CT Scan kutoka 12 hadi 97, mammography kutoka nne hadi 20, huku mashine za x-ray za kidigitali zikiongezeka kutoka 147 hadi 770”, alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA), Nchi Wanachama na washirika wa kimataifa kuendelea kuunga mkono uimarishaji wa huduma jumuishi za saratani nchini Tanzania, ikiwemo kufadhili miradi ya kitabibu iliyoainishwa katika mpango maalumu ulioandaliwa na Tanzania kwa kushirikiana na IAEA kupitia kauli mbiu ya Rays of Hope (Mionzi ya Matumaini).

Utekelezaji wa miradi hiyo unatarajiwa kuongeza huduma za uchunguzi, utambuzi na matibabu katika maeneo mbalimbali nchini na hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wanaolazimika kusafiri umbali mrefu au kufika katika hospitali, saratani ikiwa katika hatua za mwisho.

Katika hatua inayolenga kuipa Tanzania nafasi kubwa zaidi kikanda, Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA) kuiteua Taasisi ya Saratani Ocean Road kuwa Kituo cha Umahiri cha Saratani, ili kusaidia mafunzo na kujenga uwezo wa wataalamu kutoka nchi nyingine, hususan zile za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Jukwaa hilo limefunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Rafael Mariano Grossi, huku likiweka msisitizo katika kuendeleza mpango wa Rays of Hope, ambao Tanzania tayari inanufaika nao katika kujenga uwezo wa huduma za saratani.

Tanzania imetumia mkutano huo kueleza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na IAEA katika matumizi mengine ya teknolojia ya nyuklia, ikiwemo kilimo na maandalizi ya muda mrefu ya programu ya nishati ya nyuklia.

Kwa Tanzania, mkutano huo unatoa fursa ya kuunganisha hatua ambazo tayari zimepigwa na mahitaji ya awamu inayofuata ya kuongeza vituo vya saratani, kujenga wataalamu, kupata teknolojia zaidi na kuimarisha ushirikiano wa kisayansi na kifedha.

Jukwaa hilo la siku mbili linafanyika chini ya kaulimbiu “Rays of Hope: Delivering on the Promise of Cancer Care,” likiwakutanisha viongozi, wanasayansi, wataalamu wa afya na wadau wengine kujadili namna ya kupunguza pengo la upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu ya saratani duniani.

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeendesha mafunzo ya upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu madogo ...
14/09/2026

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeendesha mafunzo ya upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu madogo kwa kushirikiana na wataalam kutoka Uingereza ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa kutoa huduma bora za kibingwa na bobezi wakati wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 yanayotarajiwa kufanyika Tanzania, Kenya na Uganda.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo madaktari kufanya upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu madogo kwa ufanisi zaidi.

Dkt. Mpoki amesema ushirikiano baina ya MOI na taasisi ya St. Roch Society ya Uingereza utawezesha kuimarisha utoaji wa tiba ya mifupa na majeraha kwa wanamichezo kuelekeza mashinadnao ya AFCON 2027, pamoja na wananchi wa kawaida.

Kwa upande wake, Daktari bingwa wa upasuaji wa Magoti kutoka St. Roch Society ya Uingereza Dkt. Nic Bowman, ameushukuru uongozi wa MOI kwa mapokezi mazuri na ukarimu, akieleza kuwa ushirikiano kati ya taasisi hizo umeendelea kuimarika.

Mafunzo hayo yamewakutanisha wataalam wa afya kutoka Tanzania, Ghana, Sudan Kusini, Kenya na Uganda, yakilenga kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi katika teknolojia za kisasa za upasuaji wa magoti.

Mbunge wa jimbo la Segerea Mhe. Agnesta Lambert Kaiza (CHAUMA) amefika nyumbani kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa T...
11/09/2026

Mbunge wa jimbo la Segerea Mhe. Agnesta Lambert Kaiza (CHAUMA) amefika nyumbani kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mara nyingine kumfariji na kumpa pole kwa kuondokewa na mme wake mpendwa.

Pamoja na salaam binafsi, Mhe. Mbunge Agnesta amewasilisha salamu za rambirambi kutoka kwa wananchi wa jimbo la Segerea.

Mhe mbunge amemuahidi Mhe Rais kuwa wana Segerea wataendelea kumuombea ili apite salama ktk kipindi hiki kigumu.

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ametangaza Septemba 15 ambayo ni siku yake ya kuzaliwa, kuwa siku ya Mapumziko ya ...
11/09/2026

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ametangaza Septemba 15 ambayo ni siku yake ya kuzaliwa, kuwa siku ya Mapumziko ya Kitaifa nchini humo, ikipewa jina la Munhumutapa Day, hatua inayolenga kutambua na kuenzi urithi wa Kihistoria na kitamaduni wa Zimbabwe.

Uamuzi huo umewekwa rasmi Kisheria kupitia Statutory Instrument 148 of 2026, na kufanya Septemba 15 kuwa miongoni mwa siku rasmi za Mapumziko nchini Zimbabwe ambapo kwa mujibu wa uamuzi huo, Munhumutapa Day itaadhimishwa kila mwaka k**a sehemu ya kalenda rasmi ya Sikukuu za taifa.

Jina la Munhumutapa linahusishwa na historia ya dola ya kale ya Mutapa, iliyokuwa na ushawishi mkubwa katika eneo ambalo leo linajulikana k**a Zimbabwe pamoja na sehemu za nchi jirani. Serikali ya Zimbabwe imekuwa ikisisitiza umuhimu wa kuhifadhi historia, utamaduni na urithi wa taifa k**a sehemu ya kuimarisha utambulisho wa Wananchi.

Kwa kutangazwa kwa Munhumutapa Day, Septemba 15 sasa itakuwa siku maalum ya kitaifa kwa Wananchi wa Zimbabwe. Siku hiyo inatarajiwa kupewa umuhimu kupitia shughuli mbalimbali za kitaifa na kitamaduni zitakazolenga kuenzi historia na urithi wa taifa.

Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amewataka raia wa Uturuki wanaoishi nchini humo kuondoka, huku ...
10/09/2026

Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amewataka raia wa Uturuki wanaoishi nchini humo kuondoka, huku akitangaza Maandamano makubwa mbele ya Ubalozi wa Uturuki mjini Kampala, Septemba 18.

Muhoozi, ambaye ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, alisema kupitia mtandao wa X kwamba amekata uhusiano na maslahi ya Uturuki nchini Uganda na kuwataka raia wa Uturuki wafungashe mizigo yao na kuondoka.

Pia amemtaka Mbunge Twala Fadhil kuongoza maandamano hayo, huku akionya kuwa mtu yeyote atakayehusishwa na kuwa wakala wa Uturuki wakati wa maandamano anaweza kuk**atwa.

Mvutano huo unahusishwa kwa kiasi kikubwa na Fred Lumbuye, mkosoaji wa serikali ya Uganda na mwanablogu anayeishi Uturuki.

Muhoozi amekuwa akiitaka serikali ya Uturuki kumrejesha Lumbuye nchini Uganda au kumfukuza.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna tangazo rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda linalothibitisha kwamba serikali imeweka amri rasmi ya kuwafukuza raia wote wa Uturuki.

Hatua hiyo inaweza kuongeza mvutano katika uhusiano kati ya Uganda na Uturuki, ambao unahusisha biashara, uwekezaji, miundombinu na elimu.

“Zile picha za kujiunga na Yanga nilipiga hotelini nikisaini mkataba, Ilinipa shida sana na Rais wa Yanga nadhani mpaka ...
05/09/2026

“Zile picha za kujiunga na Yanga nilipiga hotelini nikisaini mkataba, Ilinipa shida sana na Rais wa Yanga nadhani mpaka sasa kwakuwa nilimwambia sipo tayari kucheza Yanga na nipo tayari kuwarudisha kila kitu chao ili nibaki Simba ila Rais wa Yanga alikataa kabisa akasema kila Mtu ananisubiri ndani ya Yanga, tulivutana sana hakunielewa basi nikaamua kuheshimu Mkataba wangu”

- Clatous Chota Chama, Nyota wa Simba akazungumzia kujiunga na Yanga.

Address

Tabata
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when DIRA YA LEO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share