Peter Digital

Peter Digital Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Peter Digital, Digital creator, Dar es Salaam.

🎬 Peter Digital | Professional Content Creator
📲 Reels | AI Videos | Creative Visuals
✨ Content za Kiswahili zenye ubora wa kisasa
🚀 Tunabadilisha mawazo kuwa simulizi zinazovutia
📩 Kwa kazi na mawasiliano: Inbox
💡 Modern • Creative • Impactful

18/09/2026

Mwanaume anataka gharama zote za nyumba zigawanywe 50/50, lakini mkewe akimwambia amsaidie kazi za nyumbani au kuhudumia familia, anaruka na kusema yeye ni "Mume wa Kiafrika mwenye heshima zake"! 🤦🏽‍♂️
​Swali kwa wanandoa na wanaotarajia kuingia kwenye ndoa:
​1️⃣ Je, ni haki mume kudai 50/50 ya fedha lakini akakataa 50/50 ya majukumu ya nyumbani?
2️⃣ Hivi hapa binti wa watu ana mume au yuko na chenga?!
​Usipite bila kuacha maoni yako hapa chini, na share video hii iwafikie na wengine! 👇🏽
​🎬 Tazama mchezo huu wa 3D kutoka Peter Digital.

15/09/2026

Alimfunga kijana wa watu miaka 4 jela bila hatia kisa tu gari lake kuharibika... Lakini leo hii, utajiri na maisha ya Mama Tajiri yapo mikononi mwa kijana huyo huyo! 😱🔥
​Je, ungekuwa wewe ni Baraka...
🟢 1: Unamsaidie na kumsamehe?
🔴 2: Unamkaushie ili ajifunze adabu?
​Acha maoni yako hapa chini na SHARE video hii na wengine! 👇🎬

14/09/2026

Unapomdharaulisha mtu aliyeanguka leo, unamwandalia njia ya kuwa shujaa kesho! 💔🔥 Neema alimfukuza na kumtapeli mumewe kwa dharau, lakini hakujua gurudumu la maisha linavyozunguka...
​Ungefanya nini ungekuwa kwenye nafasi ya Juma siku alipopata mafanikio? Ungemsamehe au ungemuacha? 👇 Dondosha comment yako hapo chini! 👇

12/09/2026

Je, tamaa ya maisha ya muda mfupi inaweza kukufanya umkana mama aliyekubeba miezi tisa tumboni?
​Katika mwendelezo wa igizo hili la kusisimua, Neema anakumbana na ukweli mchungu wa maisha. Baada ya kumfukuza mama yake mzazi getini kwa ukatili ili kuficha asili yake ya umaskini mbele ya mumewe Daniel, leo hii malipo yameanza papo hapo.
​Kwa kushawishiwa na rafiki zake wa karibu, Neema alikataa kitita cha Shilingi Milioni 50 kutoka kwa Daniel na kuamua kwenda mahak**ani. Matokeo yake? Ameshindwa kesi vibaya, na wale mashoga zake waliokuwa wanamfaidi fedha zake wamemtupa nje bila huruma!
​Sasa hivi Neema yuko mtaani peke yake, huku Daniel akibaki na maamuzi magumu mikononi mwake...

​K**a ungekuwa Daniel, ungempa Neema hiyo Milioni 50 aanzishe maisha au ungemkaushia dunia izidi kumfundisha adabu?
​Je, kuna nafasi ya kusamehewa kwa mtoto aliyewaasi wazazi wake kisa shinikizo la marafiki?
​Tafadhali dondosha maoni yako hapo chini—tunasoma kila comment! 👇
​📌 TAZAMA VIDEO KAMILI | LIKE | SHARE | FOLLOW PAGE YETU KWA MUPATILIZO WA SERIES HII

🔥 MASHABIKI WA PETER DIGITAL, NIAMBIE! 🔥Kati ya series zote tulizoanza, ni ipi bado unaikumbuka na unataka tuirudishe he...
12/09/2026

🔥 MASHABIKI WA PETER DIGITAL, NIAMBIE! 🔥
Kati ya series zote tulizoanza, ni ipi bado unaikumbuka na unataka tuirudishe hewani? 😱🎬
👇 Andika jina la series unayoitaka kwenye COMMENT.
K**a watu wengi wataichagua, tutaifufua na kuendelea na episode inayofuata! 🔥👀
Peter Digital — hadithi haijaisha! 🎥🔥

05/09/2026

Je, unaweza kumkana mzazi aliyekusomesha kwa shida na tabu, kisa tu kulinda ndoa na utajiri wa uongo?!
​Neema amechukua mabegi ya wazazi wake na kuwatupia nje ya geti kwa ukatili mkubwa... Anaogopa Daniel akiwakuta hapo atagundua ukweli wa umaskini wa familia yao!
​Lakini swali linabaki kwako mwanafomu... 👇
K**a mwanamke anaweza kumkana na kumtupa mama yake mzazi, huyo mume ataaminije k**a yuko salama?!
​💬 Dondosha comment yako hapo chini:
​Daniel ampe adhabu gani akikuta huu ukatili?
​Una ushauri gani kwa binti anayewaonea aibu wazazi wake?
​(Usisahau Kushea na Kutag rafiki yako aone huu udhalimu! 🔔)





03/09/2026

Kuna vitu kwenye maisha unaweza kupoteza ukavipata tena, LAKINI SIO WAZAZI WAKO! 😭💔
​Rehema alijikana asili yake na kuwafukuza wazazi wake nje ya geti kisa tu kulinda ndoa yake na bilionea Daniel. Lakini je, laana ya machozi ya mama na hekima ya fumbo la baba vitaiacha ndoa hii salama?
​JE, UNGEKUWA DANIEL UNGEFANYA NINI BAADA YA KUGUNDUA UKWELI HUU? 💬
​Dondosha comment yako hapo chini, na usiache ku-share video hii iwafikie wote wanaotukana malezi ya wazazi wao!

03/09/2026

Baraka anakula msumari wa moto! Mzee wake amelazwa mahututi kijijini anahitaji matibabu ya haraka, lakini Baraka hana hata shillingi moja—hela zote alizokuwa nazo alimpa Neema ambae kwa sasa anapanga mtego wa kumdhalilisha VIP Club mbele ya umati! 💔😭
​Hivi wewe ungekuwa kwenye nafasi ya Baraka, ungefanya nini?
👉 Ungetoa pikipiki yako dhamana kuokoa maisha ya baba?
👉 Au ungeenda VIP Club kumfuata Neema upate hela zako?
​Dondosha maoni yako hapa chini! 👇👇

13/08/2026

Alionekana maskini, dhaifu na asiye na thamani… lakini siri yake inaanza kufichuka! 😳💔
Zawadi anaendelea kumsaidia Daniel kwa moyo wa kweli, huku Tessy akiamini kuwa pesa ndiyo kila kitu. Lakini Daniel ana siri ambayo inaweza kubadilisha kila kitu… 👀🔥
Je, Zawadi atajuta kumwamini Daniel? Na Tessy atagundua nini?
👇 Tazama EP 3 mpaka mwisho na usikose EP 4!

12/08/2026

Matajiri wengi huanzia kwenye msoto, lakini ni wanawake au watu wachache sana wenye moyo wa kukubali kukaa kwenye matope ya mchakato.
​Wengi leo wanakimbilia waliofanikiwa tayari na kusahau kuwa kila aliyepo juu, kuna mtu alishika mkono wake akiwa chini kabisa. Utu haupimwi kwa kile ulichonacho mkononi leo, unapimwa kwa akili na nia yako ya kesho! 💯🔥
​Tazama Episode hii ya 2 kisha niambie ukweli kutoka moyoni mwako:
👇 Je, wewe uko upande gani? Upande wa KUTAFUTA PAMOJA kuanzia kwenye msoto, au wa KUSUBIRI ALIYEFANIKIWA TAYARI?
​Dondosha comment yako hapo chini! 👇💬

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Peter Digital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share