Swahili Prime Ent

Swahili Prime Ent Swahili Prime Ent.
> Habari | Michezo | Burudani | Maisha.
> Kila kitu unachohitaji kujua kipo hapa. �
>Ingia hapa kwa habari zaidi �
swahiliprime.blogspot.com

SABABU 8 KWANINI WANAWAKE WANAIGIZA SAUTI ZA CHUMBANI WAKIWA NA WEWE!Udhaifu wako mkubwa k**a mwanaume ni kudhani kuwa a...
08/06/2026

SABABU 8 KWANINI WANAWAKE WANAIGIZA SAUTI ZA CHUMBANI WAKIWA NA WEWE!

Udhaifu wako mkubwa k**a mwanaume ni kudhani kuwa akipiga zile sauti za mahaba chumbani, basi unafanya mambo kwa usahihi.

Ukweli ni kwamba wanawake wanaigiza kufika kileleni mara nyingi zaidi ya unavyofikiria. Usipoelewa, utaendelea kutembea mjini kwa maridadi na maringo ya uongo wakati mwanamke wako anajiondoa kimya kimya kwenye mahusiano.

1. ANAPOTEKA EGO YAKO (Kulinda Hadhi Yako)
Wanawake wanajua kuwa wanaume wanatupia uanaume wao kwenye uwezo wa kitandani. Badala ya kuumiza hisia zako, anaamua kucheza muvi.
Anapiga sauti ili usihisi k**a umefeli. Unadhani wewe ni Simba wa Nyika, kumbe yeye ni muigizaji tu wa filamu!

2. AMECHOKA NA KUKINAI.
Mwanamke anaigiza pale anapogundua kuwa tendo hilo halina mabadiliko na halitakuwa bora tena.
Akili yake ikishachoka, anajifanya amemaliza ili tu mmalize.

3. KUEPUKA MIGOGORO NA MALUMBANO.
Baadhi ya wanaume wanakuwa wakorofi na wenye kujihami wakirekebishwa. Badala ya kukabili hasira au unyonge wako, anaona bora aigize kuridhika. Anachagua amani ya uongo kuliko ukweli wa dhati.

4. UNAWAHI SANA KUMALIZA.
Wanaume wengi wanataka miitikio ya waigizaji wa picha za ngono wakati injini zao ni za pikipiki zinawaka na kuzima haraka. Unamaliza kabla yeye hata hajachochea moto. Anaigiza kumaliza kwa sababu wewe ushamaliza zamani.

5. HUMZINGATII (Husikilizi)
Anakupa ishara lakini unajifanya kipofu. Anasogeza mwili wake, lakini wewe unaendelea na mtindo ule ule wa kukariri. Anaongoza mkono wako, lakini wewe unarudi kwenye mifumo yako. Mwanamke anaigiza pale anapogundua hujali lugha ya mwili wake.

6. KUTOKUWEPO WA HISIA (Emotional Disconnection)
Mwanamke akishajiondoa kihisia kwako, mwili wake unafata. Atakupa muonekano wa nje (Performance), lakini hautapata kilele cha dhati cha hisia zake. Yupo hapo kimwili, lakini kiakili ameshahama kitambo.

7. HAJAWAHI KUFIKA KILELENI NA WEWE
Kuna wanawake hawajawahi kabisa kufika kileleni wakiwa na wanaume wanafahamu hisia hiyo wakiwa peke yao tu. Wanaigiza kwa sababu hawakuamini k**a una uwezo wa kuwafikisha hapo.

8. ANATAKA USIKU UISHE, SIO UENDELEE.
Baadhi ya wanaume wanageuza tendo k**a mbio za nyika zisizo na dira wala marudio. Mwanamke anaamua kuweka mstari wa mwisho wa uongo ili tu akimbie mateso hayo yasiyoisha.

Wanaume, acheni kufanya makosa ya kudhani kelele chumbani ni burudani! Mwanamke anapoigiza kufika kileleni, huo sio mchezo usio na madhara hiyo ni Talaka ya Kimya Kimya Inayotambaa kwa Kasi ya Konokono. Siku akiacha kuwa mkweli kwako kitandani, ndio siku anayoanza kuwa mkweli kwake mwenyewe nje ya nyumba. Na hapo ndipo wanaume wengi wanapopoteza wanawake bila kuelewa wamekosea wapi.

Follow Swahili Prime Ent

IRAN YAFUNGA RASMI MLANGO WA BAHARI WA HORMUZ KWA 100%!Shirika la Habari la Serikali ya Iran (Fars News) limetangaza ras...
08/06/2026

IRAN YAFUNGA RASMI MLANGO WA BAHARI WA HORMUZ KWA 100%!

Shirika la Habari la Serikali ya Iran (Fars News) limetangaza rasmi kufungwa kikamilifu kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz, ikiwa ni jibu la dharura katika vita vinavyoendelea kati yake na Israel.

Video zilizorushwa na vyombo vya habari vya Tehran zinaonyesha boti za mwendokasi na vikosi vya majini vya Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC) vikiwa vimetapakaa kwenye chakepoint hiyo ya kimkakati ili kusimamia amri hiyo ya mzingiro bila msamaha kwa nchi yoyote.

Mlango huu wa bahari unabeba takriban asilimia 20 ya mafuta yote ya dunia na Gesi Asilia ya Kimiminika (LNG). Hatua hii imesababisha safari za meli za mafuta kupungua kwa kiwango kikubwa, na kupelekea bei ya nishati kupaa kwa kasi.

Iran inajua kuwa haina uwezo wa kushindana angani na ndege za Israel za F-35 Stealth Jets. Kwa hiyo, badala ya kupigana vita ambavyo vitawagharimu kijeshi, wameamua kuhamishia mapambano kwenye uchumi wa dunia. Kwa kufunga Mlango wa Hormuz, Iran inamnyonga kiuchumi kila dereva aliyepo Marekani, Ulaya, na Asia kupitia bei ya mafuta, na kumlazimisha Donald Trump kuingilia kati na kuifunga breki Israel kwa nguvu.

Hapa sasa ndipo tunaweza kushuhudia mapigano ya ana kwa ana ya majini. Kwa sababu Kikosi cha tano cha Jeshi la Majini la Marekani (US 5th Fleet) kilichopo Bahrain hakitakubali Mlango wa Hormuz ufungwe kwa sababu sheria za kimataifa zinasema ni njia huru ya maji. Kitendo cha boti za IRGC kusimama hapo kinatengeneza mazingira ya dharura ambapo manowari za Marekani zinaweza kuanza kufyatua risasi ili kufungua njia hiyo kwa nguvu.

Follow Swahili Prime Ent

K**anda Mkuu wa IRGC wa Iran, Ahmad Vahidi, Anaripotiwa KUUAWA kwenye Mashambulizi ya Ndege za F-35 za Israel! Ripoti za...
08/06/2026

K**anda Mkuu wa IRGC wa Iran, Ahmad Vahidi, Anaripotiwa KUUAWA kwenye Mashambulizi ya Ndege za F-35 za Israel!

Ripoti za awali kutoka kwenye mitandao ya habari ya Kiarabu zinasema kuwa, K**anda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC), Ahmad Vahidi, ameuawa usiku wa kuamkia leo katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel jijini Tehran.

Vahidi si askari wa kawaida wa mipakani. Alikuwa K**anda wa zamani wa kikosi cha siri cha Quds Force, kabla ya Soleimani, alikuwa Waziri wa Ulinzi wa Iran, na ni mmoja wa washauri wakuu wa karibu wa Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei. Yeye ndiye ubongo unaoratibu usambazaji wa makombora kwa vikundi vyote vya proxi (k**a Hezbollah na Houthi).

Utawala wa Iran unaongozwa na itikadi ya kisasi. Kuuawa kwa K**anda wa ngazi hii kunalazimisha jeshi la IRGC kujibu mapigo kwa kutumia silaha zao za mwisho kabisa bila kuogopa matokeo yake. Hii inaweza kuifanya Iran irushe mamia ya makombora kwa mara moja kuelekea miji ya Tel Aviv na Haifa, jambo ambalo litalipua rasmi Vita Kuu ya Dunia ya Ukanda huo, na kuharibu kabisa mpango wa amani wa Donald Trump.

Taarifa hizi bado zinasubiri uthibitisho rasmi kutoka serikali ya Iran, lakini tayari zimeshasababisha taharuki kubwa na sherehe kwa upande wa Israel.

Kupotea kwa Ahmad Vahidi kunaacha pengo kubwa sana katika safu ya amri ya kijeshi na ulinzi wa anga wa nchi ya Iran katikati ya dhoruba hili la kivita.

Follow Swahili Prime Ent

HALI NI MBAYA MASHARIKI YA KATI: Mvutano unazidi kupaa kwa kasi ya hatari baada ya mataifa mawili kuanza kupigana yenyew...
08/06/2026

HALI NI MBAYA MASHARIKI YA KATI: Mvutano unazidi kupaa kwa kasi ya hatari baada ya mataifa mawili kuanza kupigana yenyewe kwa yenyewe ndani ya ardhi zao!

Utawala wa Iran ulirusha makombora makubwa ya masafa marefu yakilenga maeneo ya kaskazini mwa nchi ya Israel.

Punde baada ya mashambulizi hayo, ndege za kivita za Israel zilipenya anga la Iran na kuangusha mabomu mazito yaliyosababisha milipuko mikubwa katika miji ya Tehran ambao ni mji mkuu wa nchi na kitovu cha amri ya kijeshi.
Tabriz ambalo ni jiji kuu la Kaskazini-Magharibi mwa Iran lenye viwanda vikubwa vya ulinzi.
Isfahan ambao ni kitovu kikuu cha utafiti wa teknolojia ya Nyuklia na maghala ya makombora ya chini ya ardhi.

Mabadilishano haya ya dharura ya vipigo vya kijeshi yanatokea huku Rais wa Marekani, Donald Trump, akiwa katikati ya juhudi kubwa za kusukuma makubaliano ya amani na Iran. Hatua hii ya Israel inaiweka diplomasia ya Marekani chini ya shinikizo kubwa na hatari ya kufeli.

Mji wa Tabriz upo karibu na mpaka wa Kaskazini. Kupiga hapa maana yake Israel imesafisha mifumo ya rada za Kaskazini ili ndege zao ziweze kuingia na kutoka bila kuzuiliwa.

Netanyahu ametumia muda huu huu ambao Iran ilirusha makombora k**a sababu halali ya kupiga Iran, ili kuhakikisha anaharibu kabisa uwezekano wa Trump kukaa meza moja na viongozi wa Iran kusaini mkataba wa amani ambao Israel inauona k**a tishio.

Follow Swahili Prime Ent

ISRAELI YAASI AMRI YA TRUMP, YAENDELEA KUPIGA MABOMU JIJI LA TEHRAN KWA NDEGE ZA F-35!Licha ya Rais wa Marekani, Donald ...
08/06/2026

ISRAELI YAASI AMRI YA TRUMP, YAENDELEA KUPIGA MABOMU JIJI LA TEHRAN KWA NDEGE ZA F-35!

Licha ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kutoa amri na shinikizo kubwa kuitaka Israel ikubali makubaliano mapya kati ya Iran na Marekani, Serikali ya Israel imeasi msimamo huo na kuendelea kushambulia kwa mabomu jiji la Tehran kwa kutumia ndege za kivita za F-15, F-35, na makombora ya Marekani.

Mashambulizi haya yanafanyika kwa maamuzi ya upande mmoja ya Israel, hatua inayotishia kupasua kabisa uhusiano wa kihistoria kati ya Washington na Tel Aviv.

Netanyahu anaonyesha kuwa hayuko tayari kusitisha vita hadi miundombinu yote ya nyuklia na kijeshi ya Iran isambaratishwe, huku Trump akitaka diplomasia ichukue mkondo wake ili kulinda uchumi na bei ya mafuta duniani.

Israel inajua kuwa makubaliano yoyote ya amani yatakayosainiwa kati ya Trump na viongozi wa Tehran yataipa Iran nafasi ya kuendelea kuratibu mradi wake wa nyuklia chini ya meza bila kupigwa. Netanyahu anaamini hii ndio nafasi yake ya mwisho ya kihistoria kutumia ndege za F-35 kupenya na kuharibu maghala ya siri ya Tehran kabla Marekani haijamfunga mikono kisheria.

Ndege za F-35 na F-15, pamoja na makombora yanayotumika kupiga Tehran, zote zimetengenezwa na Marekani na zilitolewa k**a msaada wa kijeshi. Israel kuzitumia silaha hizi kwa dharura dhidi ya maagizo ya White House ni dhihirisho la wazi kuwa Tel Aviv imeweka maslahi yake ya usalama mbele kuliko urafiki wake na Washington.

Follow Swahili Prime Ent

HIZI NDIZO HATUA 6 ZA NDOA, NA KWANINI WATU WANAKATA TAMAA KWENYE HATUA YA 3!Ndoa ina hatua sita kuu, lakini jambo la ku...
07/06/2026

HIZI NDIZO HATUA 6 ZA NDOA, NA KWANINI WATU WANAKATA TAMAA KWENYE HATUA YA 3!

Ndoa ina hatua sita kuu, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba wanandoa wengi hukata tamaa na kuachana wakiwa kwenye hatua ya tatu. Angalia rada zako vizuri, wewe upo hatua ya ngapi sasa hivi?

🌸 HATUA YA 1: Kipindi cha Asali (The Honeymoon Stage)
Kila kitu kinaonekana rahisi na chenye furaha.
Unasamehe haraka sana na upendo unakuja wenyewe bila nguvu kwa sababu maisha hayajawaweka kwenye majaribu bado.
Kila mguso una umeme wa mahaba, na unahisi hatimaye umepata kile ulichokuwa unakitafuta maishani.

⚡ HATUA YA 2: Ukweli Halisi (The Reality Stage)
Hapa ndipo unapoanza kuona yale mambo uliyoyafumbia macho wakati wa uchumba.
Unagundua anasafisha vibaya au anaacha soksi kila kona ya nyumba.
Unagundua mwenzako anahitaji kubembelezwa na kuhakikishiwa upendo mara kwa mara kuliko ulivyotarajia.

💔 HATUA YA 3: Kukata Tamaa na Maumivu (The Disappointment Stage)
Hapa ndipo ukuta unapobomoka na wanandoa wengi wanasaliti au kuachana!"
Unagundua kuwa mwenzako si yule mtu uliyemuwazia kichwani mwako.
Unaanza kuwaza kuwa oh, nilioa/niliolewa na mtu sahihi?
Ukweli ni kwamba hukukosea kuchagua mtu, hapana! Ni kwamba hapo ndipo ulipokutana na sura yake halisi baada ya picha za mapozi kuisha.

🛠️ HATUA YA 4: Marekebisho na Kubadilika (The Adjustment Stage)
K**a mkifanikiwa kuvuka na kusurvivel hatua ya tatu, mnaingia hapa.
Hapa mnaacha kujaribu kubadilishana tabia, na badala yake mnaanza kujifunza jinsi ya kuishi na kufanya kazi pamoja mkiwa na madhaifu yenu.
Unajifunza ni vita gani vya kupigana na vipi vya kuviacha vipite kwa usalama.

🤝 HATUA YA 5: Ushirika Imara (The Companionship Stage)
Hapa ndipo ndoa inapokuwa thabiti k**a mwamba na imeshika mizizi.
Yale mashtukizo yote yanakuwa yameisha, na nafasi yake inachukuliwa na kujuana kwa ndani kabisa.
Unakuwa unajua mwenzako anahitaji nini hata kabla hajasema au kuomba. Kamba yenu ya upendo inakuwa ngumu kukatika.

💎 HATUA YA 6: Upendo wa Ndani Usio na Masharti (The Deep Love Stage)
Ni wanandoa wachache sana wenye sifa za kufika hapa! Upendo hapa unakuwa hauna masharti.
Mnaweza kukaa kimya pamoja chumbani bila kuongea neno, lakini mkajisikia mko karibu zaidi kuliko wakati mnaongea.
Mnaweza kugombana lakini mnajua wazi kuwa ugomvi huo hauwezi kubomoa ngome yenu. Mmeishi kwa ubaya na wema na bado mmechagua kubaki. Hatua hii haitolewi k**a zawadi inapambaniwa kwa miaka, kwa machozi, na kwa kumsamehe mmoja msaliti mara elfu saba!

Wewe na mwenza wako kwenye hizi hatua mpaka leo mpo namba ngapi?

Follow Swahili Prime Ent kwa habari zaidi

Ingia hapa kutazama wimbo
07/06/2026

Ingia hapa kutazama wimbo

WRITTEN IN THE ECHOES - A Journey of Two Souls ❤️✨​Welcome back to...

Marekani Yaangusha Droni za Iran Angani na Kukaza Mzingiro wa Kiuchumi Baharini!Vikosi vya Jeshi la Marekani vimefanikiw...
07/06/2026

Marekani Yaangusha Droni za Iran Angani na Kukaza Mzingiro wa Kiuchumi Baharini!

Vikosi vya Jeshi la Marekani vimefanikiwa kuzitungua na kuzisambaratisha droni nne za milipuko za Iran zilizorushwa kulenga usafiri wa baharini katika Mlango wa Bahari wa Hormuz, na kujibu mapigo kwa kuharibu rada za adui.

Muda mfupi uliopita, vikosi vya CENTCOM vmetungua droni nne za ushambuliaji za Iran zilizorushwa kuelekea Mlango wa Hormuz zikiwa tisho la wazi kwa usalama wa majini. Baada ya hapo, majeshi ya Marekani yalipiga na kuharibu vituo vya rada vya pwani vya Iran kule Goruk na Kisiwa cha Qeshm ili kuzuia mashambulizi zaidi, ilieleza taarifa ya Marekani.

Marekani imefichua kuwa majaribio ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC) ya kurusha makombora ya masafa marefu kuelekea nchi za Ghuba (Kuwait na Bahrain) yamefeli, baada ya makombora hayo kutunguliwa au kuanguka kabla ya kufikia maeneo ya kambi za Marekani.

CENTCOM imezitaja taarifa za Iran kuwa ni uongo unaolenga kufunika ukweli, na imesisitiza kuwa majeshi ya Marekani yanaendelea kutekeleza amri ya mzingiro wa majini (Blockade), kwa kuzik**ata na kuzizima meli zote zisizotii sheria zinazojaribu kuisaidia Iran.

Follow Swahili Prime Ent

Iran Yazindua Mfumo Mpya wa Tozo ya Crypto kwa Meli Zote Zinazopita Mlango wa Hormuz!Nchi ya Iran imeanza rasmi kupokea ...
07/06/2026

Iran Yazindua Mfumo Mpya wa Tozo ya Crypto kwa Meli Zote Zinazopita Mlango wa Hormuz!

Nchi ya Iran imeanza rasmi kupokea malipo ya kodi na ushuru wa dharura kwa kutumia sarafu za kidijitali za Bitcoin na Crypto, kutoka kwa meli zote za mafuta zinazoendelea kupita na kusafiri katika Mlango wa Bahari wa Hormuz.

Utawala wa Iran umetangaza kuwa, kupitia mkakati huu mpya wa kidijitali, nchi hiyo itakuwa moja ya mataifa yanayomiliki kiasi kikubwa zaidi cha Crypto au Bitcoin duniani ifikapo mwaka 2030.

Marekani imekuwa ikitumia nguvu ya Dola na mfumo wa benki wa kimataifa wa SWIFT kuzipiga marufuku nchi adui zisifanye biashara ya kimataifa. Bitcoin haina mmiliki, haina Central Bank, na shughuli zake zinafanyika kwenye mtandao uliovurugika wa Blockchain ambao hauwezi kufungwa na serikali ya Washington. Iran kupokea malipo ya Crypto kutoka kwa meli za mafuta maana yake wanatengeneza kuta ya Kinga ya Kifedha ambapo wanaweza kuuza na kupokea mabilioni ya pesa bila Marekani kujua au kuweza kuzuia miamala hiyo.

Mlango wa Bahari wa Hormuz ndio barabara kuu inayopitisha takriban 20\%ya mafuta yote yanayotumiwa duniani kila siku. Iran kudai kodi ya Bitcoin ili meli zipite salama maana yake wamegeuza jiografia ya eneo hilo kuwa chanzo cha kuzalisha utajiri wa kidijitali. Kampuni za meli na nchi zinazonunua mafuta (k**a nchi za Asia na Ulaya) zitalazimika kununua Bitcoin kwa fujo ili zilipe ushuru huo na kupata mafuta, jambo ambalo linaenda kupandisha thamani ya Bitcoin sokoni kwa kiwango cha dhoruba!

Hatua hii inalenga kukata nguvu ya sarafu ya Dola ya Marekani k**a silaha ya vikwazo, na kutengeneza mfumo huru wa kifedha uliopo nje ya usimamizi wa Pentagon na nchi za Magharibi.

Follow Swahili Prime Ent

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Swahili Prime Ent posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share