Sento Flani DiCaprio

Sento Flani DiCaprio SENTOFLANI DICAPRIO
๐Ÿ“ฐ Habari za siasa โ€ข Uchambuzi โ€ข Mijadala ๐Ÿ“ Tanzania ๐Ÿ”” Kwanza kupata taarifa za kisiasa

18/09/2026

VIDEO

*MAKAMU WA RAIS ATOA MAELEKEZO MAHUSUSI KWA MAWAZIRI WATATU KUTATUA MGOGORO WA MPAKA ENEO LA WANANCHI NA MSITU WA KAZIMZUMBWI*

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ametoa siku saba kwa mawaziri wanaohusika na TAMISEMI, Maliasili na Utalii pamoja na Ardhi kufika eneo la pugu na kutatua mgogoro wa muda mrefu unaohusu mipaka ya kiutawala na mpaka wa Msitu wa Kazimzumbwi, ambao umekuwa ukiwaathiri wananchi wa Pugu na maeneo ya jirani.

Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo leo, Septemba 18, 2026, alipofanya ziara katika Dampo la Pugu linalotumika kukusanya taka za Mkoa wa Dar es Salaam ili kujionea hali halisi ya eneo hilo na kusikiliza kero za wananchi wanaoishi maeneo ya jirani.

17/09/2026

*TRC YAANZA HATUA ZA UJENZI WA RELI ZA MIJINI (MONORAIL) DSM, YASEMA SEKTA BINAFSI KUTEKELEZA MRADI HUO*

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limefanya kikao cha kwanza na mshauri mwelezi kampuni ya SYSTRA kutoka Ufaransa, inayotarajiwa kufanya upembuzi yakinifu (Feasibility Study) ya mradi wa reli za mjini (Monorail) Jijini Dar Es Salaam, ambapo limesema, sekta binfasi ndiyo itakayotekeleza mradi huo.

Kikao hicho kilichofanyika Septemba 17, 2026 Jijini Dar Es Salaam, ni kiashiria cha kuanza matayarisho ya mradi huo unaolenga kuboresha usafiri wa umma na kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo la biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya wasilisho la kampuni ya SYSTRA kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Mhandisi Machibya Shiwa, amesema, sekta binafsi imepewa takribani 70% katika utekelezaji wa dira 2025, hivyo hii ni fursa kwa sekta hiyo kutekeleza mradi huo.

โ€œNatoa wito kwa sekta binafsi kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo kufutia nafasi kubwa waliyonayo ya kuongeza uwekezaji nchini, kufuatia Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kisheria,, kisera na kitaasisi ili kuvutia uwekezaji wa ndani nan je ya nchiโ€™โ€™, ameongezea Mha. Shiwa.

Mradi huo wa ujenzi wa reli moja, unalenga kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya usafiri linalotokana na ukuaji wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo kufikia 2030 inatarajiwa kuwa na Idadi ya watu wapatao milioni kumi (10).

โ€œKuanza kwa mchakato huu ni hatua muhimu katika maandalizi ya kujenga mfumo wa kisasa wa usafiri wa Mijini. Upembuzi yakinifu utatupatia msingi wa kitaalamu wa kubaini namna bora ya kutekeleza mradi kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi na ukuaji wa jiji la Dar es Salaam.โ€ Maefafanua zaidi Mha. Machibya Shiwa.

Reli hiyo inatarajiwa kupunguza muda na gharama za safari pamoja na msongamano wa magari na kuwawezesha wananchi kufika kwa urahisi kwenye maeneo ya kazi, biashara na huduma.

Kwa mujibu wa Mhandisi Shiwa, kiuchumi, mradi huo utaongeza ufanisi wa biashara, kufungua fursa za ajira na uwekezaji na kuongeza thamani ya maeneo yanayohudumiwa na reli na kupunguza hasara zinazotokana na muda unaopotea katika foleni.

*MAKAMU WA RAIS MHE. NDEJEMBI AENDELEZA DIPLOMASIA YA TANZANIA โ€“ VIENNA* Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzan...
16/09/2026

*MAKAMU WA RAIS MHE. NDEJEMBI AENDELEZA DIPLOMASIA YA TANZANIA โ€“ VIENNA*

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya mikutano miwili ya pande mbili (bilateral meetings) pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 70 wa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA) Jijini Vienna, Austria, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tanzania kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.

Katika mkutano wake na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Bw. Rafael Mariano Grossi, mazungumzo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano katika matumizi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia kwa madhumuni ya amani na maendeleo, hususan matibabu ya saratani, kilimo na usalama wa chakula, lishe, maendeleo ya wataalamu pamoja na maandalizi ya Tanzania kuelekea matumizi ya nishati ya nyuklia k**a nyongeza ya vyanzo vya uzalishaji umeme nchini siku zijazo.

Aidha, Makamu wa Rais amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Vienna (UNOV) na Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Dkt. Monica Juma. Mazungumzo yaliyolenga kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na UNODC katika juhudi za kudhibiti dawa za kulevya.

Makamu wa Rais, Mhe. Ndejembi, yuko Jijini Vienna, Austria, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano Mkuu wa 70 wa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA), unaowakutanisha Viongozi na Wawakilishi wa Nchi wanachama kujadili masuala mbalimbali yanayohusu matumizi salama na ya amani ya sayansi na teknolojia ya nyuklia.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
16 Septemba 2026
Vienna - Austria

15/09/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Jukwaa la Kisayansi la Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA Scientific Forum) linalofanyika Vienna nchini Austria leo tarehe 15 Septemba 2026.

*TANZANIA YAPIGA HATUA MATIBABU YA SARATANI, SASA YALENGA KUWA KITOVU CHA TIBA AFRIKA*Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muung...
15/09/2026

*TANZANIA YAPIGA HATUA MATIBABU YA SARATANI, SASA YALENGA KUWA KITOVU CHA TIBA AFRIKA*

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kinga, uchunguzi na matibabu ya saratani kutokana na uwekezaji unaofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akihutubia Jukwaa la Kisayansi la IAEA mjini Vienna, Austria, amesema Tanzania inalenga kuwa kitovu cha utaalamu na mafunzo ya tiba ya saratani kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni ongezeko la chanjo ya HPV kwa wasichana wenye miaka 9โ€“14 kutoka asilimia 58 mwaka 2018 hadi asilimia 98 mwaka 2026, huku vituo vya tiba ya saratani kwa mionzi vikiongezeka kutoka vitatu mwaka 2020 hadi sita mwaka 2026. Serikali pia imeongeza teknolojia za kisasa za uchunguzi na matibabu, ikiwemo PET-Scan, MRI, LINAC, CT Scan na mammography, na inalenga kuwa na vituo tisa vya huduma jumuishi za saratani katika kanda sita za kimkakati Tanzania Bara na Zanzibar ifikapo 2030.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa IAEA na washirika wa kimataifa kuendelea kuiunga mkono Tanzania kupitia mpango wa Rays of Hope, pamoja na kuiteua Taasisi ya Saratani Ocean Road kuwa Kituo cha Umahiri cha Saratani kwa ajili ya mafunzo na kujenga uwezo wa wataalamu wa Afrika. Hatua hiyo inalenga kuimarisha nafasi ya Tanzania k**a kitovu cha huduma, utaalamu na teknolojia za kisasa za tiba ya saratani katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Tanzania imetumia mkutano huo kueleza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na IAEA katika matumizi mengine ya teknolojia ya nyuklia, ikiwemo kilimo na maandalizi ya muda mrefu ya programu ya nishati ya nyuklia.

Kwa Tanzania, mkutano huo unatoa fursa ya kuunganisha hatua ambazo tayari zimepigwa na mahitaji ya awamu inayofuata ya kuongeza vituo vya saratani, kujenga wataalamu, kupata teknolojia zaidi na kuimarisha ushirikiano wa kisayansi na kifedha.

Jukwaa hilo la siku mbili linafanyika chini ya kaulimbiu โ€œRays of Hope: Delivering on the Promise of Cancer Care,โ€ likiwakutanisha viongozi, wanasayansi, wataalamu wa afya na wadau wengine kujadili namna ya kupunguza pengo la upatikanaji

MWAMBA HUYU HAPA! ๐Ÿ”ฅUncle CHOLO, Prof. Katuga โ€” mwenyewe ni Mwamba wa Mambo! ๐Ÿ๐Ÿ’ช๐Ÿพ
15/09/2026

MWAMBA HUYU HAPA! ๐Ÿ”ฅ
Uncle CHOLO, Prof. Katuga โ€” mwenyewe ni Mwamba wa Mambo! ๐Ÿ๐Ÿ’ช๐Ÿพ

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akiongoza kikao cha Maandalizi cha Viongozi ...
14/09/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akiongoza kikao cha Maandalizi cha Viongozi na Wataalamu mbalimbali kutoka Tanzania, wanaoshiriki Jukwaa la Kisayansi la Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA Scientific Forum) mara baada ya kuwasili Vienna nchini Austria leo tarehe 14 Septemba 2026.

Makamu wa Rais, anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Jukwaa la Kisayansi la Wakala wa Kimataifa wa Nguvu ya Atomu (IAEA Scientific Forum) litakalofanyika tarehe 15 na 16 Septemba 2026 Vienna nchini Austria. Jukwaa hilo linafanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 70 wa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu ya Atomu (International Atomic Energy Agency - IAEA).

*KIWANDA KIKUBWA CHA KUCHAKATA MCHANGA MZITO WA BAHARINI(HMS) BARANI AFRIKA KUJENGWA PANGANI,TANGA*โ–ช๏ธNi cha Kampuni ya M...
14/09/2026

*KIWANDA KIKUBWA CHA KUCHAKATA MCHANGA MZITO WA BAHARINI(HMS) BARANI AFRIKA KUJENGWA PANGANI,TANGA*

โ–ช๏ธNi cha Kampuni ya Madini ya Shenghe ambacho ujenzi wake umeanza

โ–ช๏ธMadin ya mchanga mzito kutoka nchi mbalimbali Afrika kuchakatwa Pangani,Tanga

โ–ช๏ธWaziri Mavunde apongeza hatua ya kuifanya Tanzania kitovu cha uongezaji thamani madini Afrika

โ–ช๏ธAwataka wawekezaji kukamilisha ujenzi wa kiwanda mapema

โ–ช๏ธRais Samia apongezwa kwa mazingira rafiki ya uwekezaji

Chengdu,China

Kampuni ya Shenghe Resources ya China imeanza ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata madini madini ya mchanga mzito wa baharini (๐™ƒ๐™š๐™–๐™ซ๐™ฎ ๐™ˆ๐™ž๐™ฃ๐™š๐™ง๐™–๐™ก ๐™Ž๐™–๐™ฃ๐™™๐™จ) katika eneo la Tajiri,Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga ambapo kampuni hii inatekeleza mradi mkubwa wa uchimbaji wa madini tembo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Shenghe Ndg. Xie Bing wakati wa ziara ya Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali za uongezaji thamani madini zinazofanywa kampuni hiyo.

Akizungumza katika ziara hiyo Ndg. Bing amesema kwa Bara la Afrika wana miradi ya madini hayo katika nchi za Msumbiji, Afrika ya Kusini na Madagascar lakini wameichagua Tanzania kuwa ndio kitovu cha uchakataji madini hayo barani Afrika na sasa wameanza ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata madini hayo(๐™ˆ๐™ž๐™ฃ๐™š๐™ง๐™–๐™ก ๐™Ž๐™š๐™ฅ๐™–๐™ง๐™–๐™ฉ๐™ž๐™ค๐™ฃ ๐™‹๐™ก๐™–๐™ฃ๐™ฉ) wilayani Pangani,Tanga na kuahidi kukamilisha ndani ya muda mfupi ujao ambapo malighafi kutoka nchi nyingine za Afrika zitaletwa Tanzania kwa ajili ya uchakataji wake na kuongezea thamani.

Aidha,Ndg. Bing ameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mh. Rais Samia S. Hassan kwa mazingira rafiki ya uwekezaji ambayo yamewavutia kuja kuwekeza Tanzania.

Akizungumza katika ziara hiyo,Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amepongeza maamuzi hayo makubwa ya Kampuni ya Shenghe ambayo yanaendana na sera ya Madini na Sheria ya Madini ya takwa la uongezaji thamani madini nchini na kusema hatua hiyo itachochea upatikanaji wa Ajira,Kuongezeka kwa mapato na kukua kwa teknolojia katika eneo la uchakataji madini.

Aidha Waziri Mavunde ameitaka Kampuni ya Shenghe kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa wakati na pia inama

13/09/2026

TRA YAWAITA WENYE SIFA KUOMBA ZABUNI YA ETS, MWISHO SEPTEMBA 15, 2026

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, ametoa wito kwa kampuni zenye sifa na uwezo unaohitajika kujitokeza na kuwasilisha maombi ya Zabuni kwa ajili ya kutoa huduma ya Stempu za Kielektroniki (ETS), zinazowekwa kwenye bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa.

Mfumo huo ni muhimu katika kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa, kudhibiti matumizi ya stempu bandia, kupunguza mianya ya ukwepaji kodi na kusaidia kudhibiti bidhaa zinazozalishwa au kuingizwa nchini kinyume cha taratibu. Hivyo, TRA inawahimiza kampuni zenye sifa kujitokeza na kushiriki katika mchakato huo kabla ya dirisha la maombi kufungwa tarehe 15 Septemba 2026.

Kamishna Mkuu Mwenda ametoa wito huo jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2026, wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaji kwa watumishi wa TRA wenye mahitaji maalum, na kueleza kuwa kampuni zenye sifa zinakaribishwa kuomba Zabuni hiyo kabla dirisha halijafungwa.

Amesema TRA inatarajia kupata waombaji wenye uwezo, watakaowasilisha gharama nafuu na watakaosaidia kuimarisha udhibiti wa matumizi ya Stempu bandia, kupambana na bidhaa za magendo na kudhibiti bidhaa ambazo hazijafuata taratibu zilizowekwa.

13/09/2026

*Mama Samia kafungua Uchumi wa Tanzania kwa kiwango Kikubwa - Mbunge Nape*

Address

Temeke
Dar Es Salaam
N/A

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sento Flani DiCaprio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category