23/11/2025
Simba SC imepoteza mmechi yake ya kwanza 1–0 mbele ya mashabiki wao Benjamin Mkapa dhidi ya Petro de Luanda matokeo yanayoacha maswali mazito kwenye mwelekeo wa timu katika Klabu Bingwa Afrika.
Licha ya kuonekana kwa kiasi fulani kutawala mpira kwa vipindi, Simba walikosa pe*******on pass za maana, vertical runs na decisive passes kwenye eneo la hatari. Petro walicheza kwa nidhamu, wakisubiri kosa moja na Simba wakalitoa.
Kuelekea mechi nyingine za kundi D vipo vitu kadhaa ambavyo wanabidi Simba waboreshe:
🛑 Increase Verticality(Cheza kwa Kasi ya Kusogea Mbele) Simba walicheza kwa upana lakini bila kutengeneza hatari ya moja kwa moja golini. Wanahitaji vertical passes (pasi za kupenya katikati), third-man runs (mbio za mchezaji wa tatu kupokea pasi ya kushtukiza), na transitions zenye speed ya kuumiza.
🛑 Final Third Efficiency(Umakini wa Maamuzi Katika Eneo la Hatari) Tatizo si kufika, bali kufanya uamuzi. Simba wanahitaji ubunifu (creativity), killer instinct (ukali wa kumalizia), na maamuzi sahihi wanapokaribia goli.Nafasi walizokosa Ellie Mpanzu na Morice Abraham zilihitaji maamuzi makini kwenye eneo la mpinzani ili kupata mabao
🛑 Compact Defensive Shape(Ulinzi Kuwa Karibu na Kufanya Kazi K**a Unit Moja)
Bao la Petro lilitokana na pengo dogo la mpangilio. Simba wanahitaji kuwa compact (kukaa karibu), kutambua hatari mapema, na mawasiliano mazuri kati ya mabeki na kiungo wa ulinzi (namba 6).Baada ya Mligo kuangushwa na mwamuzi kupeta kuna namna eneo la Mligo lilikosa mtu wa kufanya covering kwa haraka ambapo zikapigwa pasi 6 na wachezaji wa Petro De Luanda zilizozaa bao laiti k**a wangefanya coverage ya space mapema basi huenda wangedhibiti mashambulizi
🛑 Tempo & Pressing Identity ( Kasi ya Mchezo na Presha ya Juu Kurudi Katika DNA ya Simba) Simba walipunguza pressing leo. Wanapaswa kurudi kwenye high pressing (presha ya kuwakaba wapinzani juu), kuwanyang’anya mpira mapema na kushambulia kwa flow ya kasi.
🛑 Game Management(Kutawala Dakika Muhimu) Katika mechi za CAF, kutuliza mpira, kubadilisha tempo, na kutumia akili kwenye maeneo ya hatari ni muhimu kuliko kukimbia na kutumia nguvu kila dakika.
Nafasi bado ipo wakiamua kubadilika wanaweza kuwa tishio.