Mofa Digital Studios

Mofa Digital Studios MOFA DIGITAL BACKUP PAGE 🇹🇿🇰🇪🇺🇬🇧🇮🇨🇩🇷🇼 inakusogezea habari na matukio mbali mbali kutokea kila kona ya dunia 🗺️

Taarifa kutoka kambini mwa timu ya taifa ya Brazil zinaeleza kuwa mshambuliaji nyota Neymar anatarajiwa kurejea mazoezin...
06/06/2026

Taarifa kutoka kambini mwa timu ya taifa ya Brazil zinaeleza kuwa mshambuliaji nyota Neymar anatarajiwa kurejea mazoezini wiki ijayo.

Kocha mkuu wa Brazil, Carlo Ancelotti, anasubiri matokeo ya vipimo vya mwisho pamoja na uchungu*i wa afya wa Neymar utakaofanyika Jumatatu, kabla ya kutoa uamu*i kuhusu kujiunga kwake na mazoezi ya kikosi kizima wiki ijayo.

Brazil wataanza kampeni yao ya kuwania taji la Kombe la Dunia kwa mchezo dhidi ya Morocco national football team utakaopigwa mjini New Jersey Juni 13.

Msanii wa mu*iki wa bongo fleva Dogo Rema ameweka wazi kuwa kwasasa anapitia kipindi kigumu sana kiasi kwamba hata akiom...
06/06/2026

Msanii wa mu*iki wa bongo fleva Dogo Rema ameweka wazi kuwa kwasasa anapitia kipindi kigumu sana kiasi kwamba hata akiombwa msaada na wazazi wake nyumbani anakuwa hamna kitu cha kusaidia.

''Mama akinipigia simu unakuta na kuwa sina hata mia tano ambayo hata zamani unakuta nikipata elfu kumi elfu ishirini hata hamsini nilikuwa namtumia hata mjomba kuna siku alinipigia akaniambia sasa unaishije maisha k**a hayo''Amesema - Dogo Rema Kupitia Wasafi FM

Siri aliyosema Florentino Perez kuhusu kumsajili mchezaji kwa €150m imefichuka, Perez anamtaka Olise ndani ya Real Madri...
06/06/2026

Siri aliyosema Florentino Perez kuhusu kumsajili mchezaji kwa €150m imefichuka, Perez anamtaka Olise ndani ya Real Madrid.

Baada ya taarifa hizo, Rais wa Bayern Munich Uli Hoeneß amejibu kuhusu jambo hilo.

"Hatuna nafasi ya kumuuza Olise, hauzwi hata kwa €200m"

Perez kichwa kinamuwaka Moto 😁😁

Maofisa wa Marekani na ubalozi wa Iran wamethibitisha kupokea visa za wachezaji, makocha, wakufunzi na baadhi ya wafanya...
06/06/2026

Maofisa wa Marekani na ubalozi wa Iran wamethibitisha kupokea visa za wachezaji, makocha, wakufunzi na baadhi ya wafanyakazi wa timu ya taifa ya Iran kwa ajili ya Kombe la Dunia la 2026,

Visa ambazo hazijatoka ni za Wasimamizi kadhaa, watendaji wakuu na Katibu Mkuu na rais wa Shirikisho la Soka la Iran, Pia timu ya taifa ya Iran haita weka kambi au makazi yao Arizona nchini Marekani ila watalala Tijuana, Mexico na watakuwa wakisafiri kwenda Marekani kwaajili ya mechi zao tu

Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni: "Sio mimi naamua Argentina, maamu*i yote yanapitia kwa Leo Messi"
06/06/2026

Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni: "Sio mimi naamua Argentina, maamu*i yote yanapitia kwa Leo Messi"

Mchezaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Ureno, Bruno Fernandes, amefunguka kwenye podikasti ya The Diary of a ...
01/06/2026

Mchezaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Ureno, Bruno Fernandes, amefunguka kwenye podikasti ya The Diary of a CEO kuhusu maisha yake ya soka na misingi ya malezi katika familia yake.

Bruno ameeleza kuwa mama yake alikuwa mfanyakazi wa usafi kwenye nyumba za watu, na alikuwa hapendi kabisa kuona akidharauliwa au kutumikishwa vibaya kutokana na udogo wa kazi hiyo. Jambo hilo limemfanya amheshimu sana mfanyakazi wake wa ndani wa sasa, kiasi kwamba haruhusu kabisa watoto wake wamtume au kumnyooshea vidole.

Badala yake, anawafunza watoto wake kufanya mambo yao wenyewe, akiamini kuwa sio heshima kwa mtoto kumtumikisha mtu mzima, na k**a kuna jambo lolote haliko sawa, yeye mwenyewe ndiye anayemweleza..

Follow page hii Ulimwengu wa Habari

"Kupoteza studio kwa moto si jambo dogo. Ni maumivu makubwa kuona matokeo ya jasho, muda na ndoto ulizojenga kwa miaka y...
01/06/2026

"Kupoteza studio kwa moto si jambo dogo. Ni maumivu makubwa kuona matokeo ya jasho, muda na ndoto ulizojenga kwa miaka yakikumbwa na janga k**a hili. Wanasema mwanaume analia mara chache, hivyo ukimuona mwanaume analia ujue ameumizwa kwa kiwango ambacho maneno hayawezi kueleza.

Kwa niaba yangu, ningependa kutoa wito kwa umoja wa wasanii, marafiki na wadau mbalimbali tuungane katika kipindi hiki kigumu. Kila mmoja kwa nafasi yake atoe mchango wowote unaowezekana k**a ishara ya upendo, mshik**ano na kusimama pamoja na mwenzetu. Leo ni Barnaba, kesho inaweza kuwa yeyote kati yetu.

Pole sana ndugu yangu. Tunaamini Mungu atakupa nguvu ya kusimama tena na kujenga upya kwa mafanikio makubwa zaidi" Amesema Msanii Rammy Galis

Follow hii Page Ulimwengu wa Habari

Mke wa Nipsey Hussle, Lauren London, amefichua hivi karibuni kwamba hajakuwa kwenye mahusiano yoyote tangu mume wake ali...
31/05/2026

Mke wa Nipsey Hussle, Lauren London, amefichua hivi karibuni kwamba hajakuwa kwenye mahusiano yoyote tangu mume wake alipoaga dunia, k**a njia ya kumuenzi na kumheshimu kwa kuwa mume na baba bora sana alipokuwa hai.

Pia ameweka wazi kwamba hana nia ya kuolewa au kuwa kwenye mahusiano na mtu mwingine yeyote kwa sababu anataka kubaki mwaminifu kwa mume wake milele.

Je, huu ni kiwango cha juu kabisa cha uaminifu, au ni kiki 🗣️?

Follow page hii Ulimwengu wa Habari

HAWA SITA WAHUSISHWA NA YANGA MSIMU UJAO! ​Mabingwa wa kihistoria, Dar es Salaam Young Africans (Yanga SC), wamepanga ku...
31/05/2026

HAWA SITA WAHUSISHWA NA YANGA MSIMU UJAO!

​Mabingwa wa kihistoria, Dar es Salaam Young Africans (Yanga SC), wamepanga kufanya mapindu*i makubwa na mabadiliko ya kimkakati kwenye kikosi chao kuelekea msimu ujao. Safari hii, viongozi wamekuja na msimamo mzito unaolenga mafanikio makubwa zaidi kimataifa! 🎯

​Uongozi umeweka wazi kuwa hakuna nafasi kwa mchezaji asiye na uzoefu wa michuano mikubwa ya CAF. Safari hii hakuna huruma, kwani wamegundua kuwa huruma ya nyuma ndiyo iliyowaponza. Kutokana na msimamo huo, Yanga wamedhamiria kuwang'oa vigogo hawa sita wanaohusishwa nao msimu ujao.

​AZIZ KI ~ Kiungo Mshambuliaji 🧠⚡
​LAMINE JARJOU ~ Winga wa Kushoto 💨
​IDD NADO ~ Winga wa Kulia 💫
​NASRI KOMBO ~ Beki wa kati 🛡️
​IBRA BANCE ~ Kiungo mkabaji ⚙️
​SULEYMANE FOFANA ~ Mshambuliaji wa kati ⚽🔥

​Mabadiliko haya yanakuja baada ya tathmini ya kina ya wapi kikosi kinahitaji kuongezewa nguvu ili kutawala soka la Afrika.

​Mnasemaje WanaNchi? Kati ya hawa sita, ni nani unayeona anastahili kuvaa u*i wa kijani na njano msimu ujao, na ni nani anayekidhi vigezo vya kuifikisha Yanga nusu fainali au fainali ya CAF? Angusha comment yako hapa chini! 👇🔰

Follow page hii Ulimwengu wa Habari

Klabu ya PSG imetwaa ubingwa wa Michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya kwa ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Arsenal katika ...
30/05/2026

Klabu ya PSG imetwaa ubingwa wa Michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya kwa ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Arsenal katika Mchezo wa fainali uliochezwa Budapest nchini Hungary, Mara baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1

Ubingwa huu unakuwa wa pili mfululizo kwa PSG Mara baada ya msimu uliopita kutwaa mbele ya Inter Milan

FT: PSG 1-1 Arsenal (AET: 4-3)

Follow page hii Ulimwengu wa Habari

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mofa Digital Studios posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share