Loko Kontent Digital

Loko Kontent Digital ๐Ÿ† Sports | ๐ŸŽฌ Entertainment | ๐Ÿ”ฅ Trending Stories
Habari za michezo, burudani na matukio mapya kila siku. Follow upate kontent kali zaidi!

Twiga stars timu ya taifa ya Tanzania kwa kina dada imepokea kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Burkina Faso k...
31/07/2026

Twiga stars timu ya taifa ya Tanzania kwa kina dada imepokea kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Burkina Faso kwenye mchezo wake wapili wa hatuwa ya makundi wafcon 2026

Matokeo hayo yanaifanya Twiga stars kuendelea kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi B akiwa na alama tatu alizozipata kwenye mchezo wake wa kwanza ambao alimfunga Afrika Kusini

Mpaka sasa Twiga stars amebakiza mchezo mmoja wa kutamatisha hatuwa ya makundi ambao atacheza dhidi ya Ivory coast agust 4 saa tano usiku, mchezo huwo utaamuwa hatma ya Twiga stars kukata tiketi ya kusogea hatuwa ya mtoano ama kurudi nyumbani

Hadi sasa kwenye msimamo ivory coast ndie kinara akiwa na alama zake nne, Tanzania nafasi ya pili na alama mbili, Burkina Faso nafasi ya tatu akiwa na tatu huku Afrika Kusini wakiwa mkiani na alama moja

Mechi za mwisho kundi B
Tanzania vs Ivory coast
Afrika Kusini vs Burkina Faso

Nani kusogea hatuwa inayofuata?

Tanzania Football Federation Haji Manara ClifordMario Ndimbo next game iwe hii tunavuka

31/07/2026

Twiga stars kuwavaa Burkina Faso leo hii julai 31 majira ya saa 5 kamili usiku kwenye mwendelezo wa michuano ya wafcon 2026 nchini Morocco

Twiga stars wanaingia kwenye mchezo huo baada ya kupata ushindi wa bao mbili kwa moja kwenye mchezo wao wa kwanza waliocheza dhidi ya Afrika Kusini

Huku Burkina Faso wakiingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita kwa kichapo cha bao nne kwa moja dhidi ya Ivory coast

Mchezo huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa kila timu huku Twiga stars ikiwa inashika nafasi ya pili na Burkina Faso ikiwa mkiani kwenye msimamo wa kundi B

Timu ya taifa ya Tanzania wanawake Twiga stars imefanikiwa kupata ushindi katika mchezo wake wa kwanza wa hatuwa ya maku...
27/07/2026

Timu ya taifa ya Tanzania wanawake Twiga stars imefanikiwa kupata ushindi katika mchezo wake wa kwanza wa hatuwa ya makundi Kwenye michuano ya WAFCON2026 dhidi ya Afrika Kusini banyana banyana

Twiga stars wamepata ushindi kwa kuichapa banyana banyana mabao mawili kwa moja, na kuandika historia ya kupata alama tatu kwenye michuano hiyo kwa mara ya kwanza toka walipoanza kushiriki mwaka 2010

Baada ya ushindi huo Twiga stars watashuka tena dimbani julai 31 kuvaana na Burkina Faso kuusaka ushindi wao wapili utakao wawezesha kutinga hatuwa ya mtoano kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo

Afrika Kusini 1 - 2 Tanzania
FT : Wafcon 2026

tfftanzania Tanzania Football Federation Baraza la Michezo la Taifa CAF

Shirikisho la soka CAF limetangaza tarehe ya kufanyika kwa draw ya ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho barani Afrika...
27/07/2026

Shirikisho la soka CAF limetangaza tarehe ya kufanyika kwa draw ya ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho barani Afrika hatuwa ya awali kuwa ni August 6 Cairo nchini Misri

Hatuwa hiyo ya awali ya ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho zinataraji kufanyika mwezi Septemba kuanzia tarehe 4 hadi 6 kwenye mzunguko wa kwanza

Na mzunguko wa pili wa hatuwa hiyo ya awali ukitarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 11 hadi 13 mwezi Septemba 2026

Katika michuano hiyo ya CAF ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho Tanzania imetoa wawakilishi wanne ambao ni Young Africans na Simba wanaokwenda kushiriki ligi ya mabingwa huku Azam fc na Singida black stars kwenye michuano ya kombe la shirikisho

Ikumbukwe msimu uliopita wawakilishi wote wanne wa Tanzania walifanikiwa kufika hatuwa ya makundi na kushindwa kusogea hatuwa inayofuata

TotalEnergies CAFCL & CAFCC ๐Ÿ† Azam Football Club SINGIDA BS Young Africans Sports Club Simba Sports Club tffboard๐Ÿ”ต Tanzania Football Federation

Source Africa Soccer Zone ๐ŸŸขโšช

Ni muda mwingine tena kwa taifa la Tanzania kuandika rekodi kwenye michuano ya kimataifa kwa ngazi ya Afrika, na mara hi...
25/07/2026

Ni muda mwingine tena kwa taifa la Tanzania kuandika rekodi kwenye michuano ya kimataifa kwa ngazi ya Afrika, na mara hii ni kina dada twiga stars kushuka dimbani saa 2 kamili usiku kuwakabili "banyana banyana" Afrika Kusini huko nchini Morocco

Ndani ya mwaka 2026 Tanzania tumeshuhudia vijana wa U17 Serengeti boys wakicheza fainali ya afcon ya vijana ambayo haikutarajiwa kwa vijana hao baada ya kuwa wanakwama hatuwa ya makundi mara kwa mara

Mbali na vijana hao pia Tanzania kupitia Taifa stars iliandika rekodi kwenye michuano ya Afcon 2025 iliyotamatika 2026 Januari nchini Morocco na Taifa Stars kwa mara ya kwanza kucheza hatuwa ya mtoano 16 ya michuano ya Afcon

mafanikio ya Serengeti boys na Taifa stars kwenye michuano hiyo ya kimataifa yamepatikana nchini Morocco na sasa ni twiga stars ambao wako Morocco kuipeperusha bendera ya Tanzania

Ikumbukwe "banyana banyana" Afrika Kusini wanaingia kwenye michuano hiyo wakiwa na medali za ubingwa wa Wafcon na kuwa taifa la tatu kati ya mataifa matatu yaliyowahi kutwaa taji hilo

Na mara ya mwisho kwenye michuano ya wafcon iliyopita twiga stars na banyana banyana walikutana hatuwa ya makundi na mchezo kutamatika kwa sare ya bao moja kwa moja

Tanzania Football Federation
Baraza la Michezo la Taifa
ClifordMario Ndimbo

Mahak**a ya usuluhishi wa michezo CAS imepanga October nane kuwa siku ya kusikiliza rufaa ya Senegal dhidi ya uwamuzi wa...
25/07/2026

Mahak**a ya usuluhishi wa michezo CAS imepanga October nane kuwa siku ya kusikiliza rufaa ya Senegal dhidi ya uwamuzi wa kupokwa ubingwa wa mataifa ya Afrika AFCON 2025 iliyofanyika nchini Morocco

Senegal walikata rufaa baada ya shirikisho la soka Afrika CAF kubatilisha ubingwa wao na kuwatangaza Morocco kuwa mabingwa wa mashindano hayo ya AFCON 2025 yaliyomalizika mwezi Januari mwaka huu

Mchezo huwo wa fainali ulimalizika kwa Senegal kuwa bingwa baada ya kushinda bao moja kwa sifuri katika muda wa nyongeza baada ya 90 za kawaida kuisha bila mshindi

CAF baada ya kupitia kanuni za mashindano walibatilisha ushindi wa Senegal kufuatia tukio la wachezaji wa Senegal kutoka uwanjani wakati wa mchezo kwa takribani dakika 17 baada ya mzozo mkubwa uliozuka wakati mchezo ukiendelea kufuatia tukio la Morocco kupewa mkwaju wa penati

Wachezaji wa Senegal walitoka uwanjani na kwenda vyumbani kupinga uwamuzi wa mwamuzi kuwapa Morocco mkwaju wa penati wakishindikizwa na kocha wao Pape Thiaw na baada ya muda unaokadiriwa kuwa dakika 17 wachezaji wa Senegal walirudi uwanjani na Morocco wakapiga penati ambayo Brahimu Diaz alikosa na mchezo ukaendelea

Baada ya tisini kutamatika Senegal wakapata bao katika dakika 30 za nyongeza kupitia kwa mchezaji wao Pape Gueye na kutwaa ubingwa huo kabla haujabatilishwa

Na mnamo tarehe 25 mwezi March, Senegal iliwasilisha rufaa yake katika mahak**a ya usuluhishi wa michezo CAS ikitaka uwamuzi wa CAF kubatilishwa na warejeshewe ubingwa wao

Katika uwamuzi wa CAF baada ya kupitia kanuni za mashindano na kuubatilisha ubingwa wa Senegal, waliwapa Morocco ushindi wa mabao matatu kwa sifuri na kuwatangaza kuwa mabingwa wa AFCON 2025 dhidi ya Senegal

Kwa sasa mahak**a ya usuluhishi wa michezo CAS itasikiliza rufaa hiyo October nane kabla ya kutoa uwamuzi wake wa mwisho kuhusu nani anapaswa kutambulika rasmi k**a bingwa wa AFCON 2025

Swali ni je nani atatambulika k**a bingwa baada ya maamuzi ya CAS kutoka?

Loko Omi Amisa Abdulrahman Yahya Njenge Micky Jnr โœช CAF Football Senegal TFT MOROCCO ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ

Credit BBC News Swahili

Klabu ya Azam fc  imemtambulisha nyota wake mpya raiya wa Ufaransa Donovan Makoma akitokea Birkirkara inayoshiriki ligi ...
22/07/2026

Klabu ya Azam fc imemtambulisha nyota wake mpya raiya wa Ufaransa Donovan Makoma akitokea Birkirkara inayoshiriki ligi kuu ya Malta

Donovan Makoma ana umri wa miaka 27 anacheza eneo la kiungo mkabaji na anasifa ya kucheza k**a mlinzi wa kati anakuja kuongeza nguvu kwenye timu ya azam fc kwa msimu wa 2026/27

Timu bora bidhaa bora

Kupitia ukurasa rasmi wa Afisa habari wa young Africans  ameandika kuwa timu ya Yanga leo  itafunga kuwatangaza wachezaj...
22/07/2026

Kupitia ukurasa rasmi wa Afisa habari wa young Africans ameandika kuwa timu ya Yanga leo itafunga kuwatangaza wachezaji wazawa walio wasajili na hivi karibuni wataanza kuwatambulisha wachezaji wao wapya wakigeni

Hadi kufikia sasa Yanga wameshatambulisha nyota wao wanne wazawa ambao watakwenda kuitumikia yanga kwa msimu wa 2026/27,

nyota hao ni Juma issa Abushiri kutoka fountain gate, Mohammed M***a, Abdulnasir Muhamed sambamba na Hussein Mihambo wote kutoka mashujaa fc

Mbali na hilo yanga tayari imeshatambulisha benchi lake la ufundi litaloongozwa na mtaalamu kutoka Afrika Kusini Manqoba Mngqithi sambamba na wasaidizi wake Simo dladla, Kagisho dikgacoi, Greg etafia sambamba na Vardaan valodia

Je Unahisi ni wachezaji wangapi wakigeni yanga itawatambulisha na huyo Uliemsikia atakuwepo?

Toka kuanza kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 1930 nchini Uruguay michuano hiyo hadi kufikia sasa mwaka 2026  tayari ...
20/07/2026

Toka kuanza kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 1930 nchini Uruguay michuano hiyo hadi kufikia sasa mwaka 2026 tayari imeshafanyika mara 23 huku mataifa nane pekee ulimwenguni ndio yamewahi kushinda taji hilo kutoka katika mabara mawili tu

Kuanzia mwaka 1930 hadi mwaka 2026 ambako ndio makala ya 23 ya michuano hiyo mikubwa ya soka dunia ilipofanyika nchini Mexico, Canada sambamba na USA haya ndio mataifa yaliyo wahi kubeba taji hilo la kombe la dunia

๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ท Brazil โ€” 5 ๐Ÿ†
๐Ÿ‡ฉ๐Ÿ‡ช Germany โ€” 4 ๐Ÿ†
๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡น Italy โ€” 4 ๐Ÿ†
๐Ÿ‡ฆ๐Ÿ‡ท Argentina โ€” 3 ๐Ÿ†
๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡พ Uruguay โ€” 2 ๐Ÿ†
๐Ÿ‡ซ๐Ÿ‡ท France โ€” 2 ๐Ÿ†
๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ธ Spain โ€” 2 ๐Ÿ†
๐Ÿด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟ England โ€” 1 ๐Ÿ†

Kulingana na mtiririko huwo wa mabingwa ambao wamewahi kushinda taji la kombe la dunia bara la Amerika kusini limetoa mataifa matatu huku bara la Ulaya likitoa mataifa matano ambayo yameonja radha ya kuwa mabingwa wa kombe la dunia

Bara la Amerika kusini ambako wanatoka Brazil, Argentina sambamba na Uruguay wao kwa ujumla wameshinda taji hilo mara 10 ambako Brazil ameshinda mara tano, Argentina akishinda mara tatu huku Uruguay akishinda mara mbili

Kwa upande wa bara la ulaya wao wametoa washindi wa tano ambao ni Germany, Italy, France, Spain pamoja na England ambao wamewahi kushinda taji hilo na kwa ujumla bara la ulaya limebeba mataji 13 ya kombe la dunia ambalo Germany na Italy kila mmoja ameshinda mara nne, Spain na France kila mmoja ameshinda mara mbili huku England akishinda mara moja na kufikisha jumla ya mataji 23 yaliyokwenda ulaya

Kwaiyo toka kuanzishwa kwa michuano hiyo, mataifa kutoka ulaya yamekuwa na wakati mzuri wa kushinda kombe hilo kuliko mataifa kutoka mabara mengine huku bara la Afrika,Asia, Amerika kaskazini pamoja na Oceania yakiwa hajawahi kushinda taji hilo

Je Mataifa ya Afrika, Asia, Amerika kaskazini pamoja na Oceania unayaona yanaweza kushinda kombe hilo kwenye makala zijazo za 24 zitakazofanyika 2030 nchini Morocco, Spain pamoja na Ureno?

Timu ya taifa ya Argentina imeshindwa kutetea taji lake la michuano ya kombe la dunia la mwaka 2026 ambalo walilibeba 20...
19/07/2026

Timu ya taifa ya Argentina imeshindwa kutetea taji lake la michuano ya kombe la dunia la mwaka 2026 ambalo walilibeba 2022 nchini Qatar baada ya kupokea kichapo cha bao moja kwa sifuri

Baada ya kichapo hiko Argentina wameshinda kufikia rekodi ambayo iliwekwa na Italia na Brazil kuwahi kubeba taji hilo mara mbili mfululizo

Italia walifanya hivyo mwaka 1934 kisha mwaka 1938 huku Brazil wakifanya hivyo mwaka 1958 sambamba na mwaka 1962 na kuwa ndio mataifa pekee yaliyowahi kubeba taji la kombe la dunia mara mbili mfululizo

Mbali na rekodi hiyo Argentina wameandika rekodi ya kumaliza mchezo wa fainali bila shuti lolote lililolenga lango huku wakipiga mashuti mawili tu kwenye dakika 120

Slide namba mbili takwimu za mchezo wa fainali Argentina vs Hispania

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
0000

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Loko Kontent Digital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share