Ushauri wa Biashara.

Ushauri wa Biashara. Badilisha Fikira badilisha Maisha

10/03/2026

MITAZAMO 5 YA KIMASKINI UNAYOPASWA KUACHANA NAYO MARA MOJA

Kuna watu wanafanya kazi kwa bidii miaka mingi, lakini maisha yao ya kifedha hayapigi hatua kubwa. Mara nyingi tatizo sio ukosefu wa bidii ni mtazamo kuhusu pesa na utajiri.

Hii hapa ni mitazamo ambayo imewazuia watu wengi kupiga hatua kuelekea utajiri.

1. KUAMINI KUWA KUFANYA KAZI SANA PEKE YAKE NDIO NJIA YA UTAJIRI

Watu wengi wanafanya kazi sana lakini bado hawaongezi utajiri. Sababu ni kwamba utajiri haujengwi na kazi pekee, unajengwa na uwekezaji na umiliki wa mali.

Usitegemee kipato tu. Anza kujenga uwekezaji na assets zinazoweza kukuongezea pesa.

2. KUAMINI KUWA KIPATO KIKUBWA NDIO UTAJIRI

Watu wengi wana kipato kikubwa lakini bado hawana utulivu wa kifedha. Utajiri haupimwi kwa kipato, unapimwa kwa mali na uwekezaji unaomiliki.

Jenga tabia ya kuhifadhi na kuwekeza sehemu ya kipato chako.

3. KUAMINI UWEKEZAJI NI WA WATU WENYE PESA NYINGI

Watu wengi husubiri mpaka wawe na pesa nyingi ndipo waanze kuwekeza. Ukweli ni kwamba watu wengi huwa matajiri kwa sababu walianza kuwekeza mapema.

Anza kuwekeza hata kwa kiasi kidogo. Consistency ndiyo siri.

4. KUTUMIA PESA KUONYESHA MAFANIKIO

Watu wengi hutumia pesa kununua vitu vya kuonyesha status kabla hawajajenga msingi wa kifedha. Mara nyingi vitu hivyo hupoteza thamani badala ya kuongeza utajiri.

Tanguliza kujenga mali na uwekezaji kabla ya kuongeza maisha ya anasa.

5. KUAMINI KUWA MUDA BADO UPO

Watu wengi huahirisha kuanza kujenga utajiri wakiamini wataanza baadaye. Lakini katika fedha muda ndiyo nguvu kubwa ya uwekezaji.

Anza mapema iwezekanavyo. Kidogo kinachoanza leo kinaweza kuwa kikubwa sana miaka ijayo.

Watu wengi hubadilisha kazi zao lakini hawabadilishi mitazamo yao kuhusu pesa.
Lakini ukweli ni huu:

Ukibadilisha mtazamo wako kuhusu fedha, unaanza kubadilisha mwelekeo wa maisha yako ya kifedha. 💰
Nitazamo gani wewe uko nao hapa?

07/03/2026

USIKATE TAMAA: SIRI YA MILANGO INAYOGOMA KUFUNGUKA

​Kuna wakati maisha yanakupeleka kona ambayo hukuitegemea. Unafanya kila kitu kwa usahihi unasali, unafanya kazi kwa bidii, unajitoa kwa watu lakini unapoishia ni kukutana na MLANGO ULIOFUNGWA. Mlango huo hauna hata tundu la kuchungulia. Unagonga, hufunguliwi. Unapiga kelele, hakuna anayeitika. Unapiga teke, mlango hautikisiki.
​Sikiliza kwa makini: Hapo ndipo mchezo unapoanza.

​1. Mlango Uliofungwa ni Kichocheo cha Akili (The IQ Booster)
​Watu dhaifu wakiona mlango umefungwa, wanakaa chini na kuanza kulia. Wanatafuta huruma ya watu. Lakini mashujaa wanajua kuwa mlango uliofungwa ni fumbo la kutatuliwa. K**a mlango haufunguki kwa kugonga, labda unahitaji kusukumwa. K**a haufunguki kwa kusukumwa, labda unahitaji ufunguo maalum. Na k**a ufunguo haupo, labda unapaswa kuuvunja au kutafuta njia nyingine ya kupita.

​Maisha hayakupi milango iliyofungwa ili kukurudisha nyuma, yanakupa ili kukufanya uwe na akili zaidi. Unapokutana na kizuizi, akili yako inalazimika kufanya kazi kwa asilimia 100 zaidi ya ilivyokuwa awali.

​2. Je, Unagonga kwa Namna Gani? (The Art of War)
​Watu wengi wanakata tamaa kwa sababu wanagonga mlango kwa "vidole." Maisha hayatambui vidole; maisha yanatambua ngumi na mabega! Kugonga tena kunamaanisha kurudi ukiwa na nguvu mpya. K**a uliomba kazi ukiwa na CV ya kawaida, rudi ukiwa na ujuzi mpya. K**a biashara ilikataa, rudi ukiwa na mbinu mpya ya masoko. Maisha yanapenda watu wasiokubali kirahisi neno "Hapana." Siri ni hii: Mara nyingi mlango hufunguliwa kwa yule anayegonga kwa sauti ya juu zaidi na kwa muda mrefu zaidi. Usiwe mtu wa kujaribu mara moja kisha unarudi nyuma ukijificha kwenye kivuli cha huzuni.

​3. Usisherehekee Kwenye Ukuta, Tafuta Mlango Mwingine!
​Kuna watu wana "Mapenzi ya Kijinga" na mlango mmoja uliogoma. Wanakaa mbele ya mlango ule ule kwa miaka kumi, wanalia, wanalalamika, na kulaumu dunia. Huo siyo uvumilivu, huo ni ujinga.

​Ukiona mlango wa mbele una walinzi na kufuli saba, geuka utazame pembeni. Labda kuna dirisha liko wazi. Labda kuna tundu la paa. Labda kuna ukuta ambao ni dhaifu unaweza kuubomoa. Maisha ni mapana sana. Usiruhusu mlango mmoja uliogoma kukupa tafsiri kuwa wewe ni "failure." Kushindwa kupita mlango mmoja hakumaanishi safari imeishia hapo kunamaanisha unatakiwa kubadili gia na kutafuta uelekeo mpya.

​4. Moto wa Ndani: Usikubali Kuzimika
​Kukata tamaa ni sawa na kuzima injini ya gari katikati ya barabara ya mwendo kasi. Utasababisha ajali ya ndoto zako! Milango inayogoma kufunguka ipo hapo ili kuchuja wale "wasio na nia ya dhati." Ni kizuizi cha asili (Natural Filter) kinachotenganisha washindi na watazamaji.

​Ukiona mlango unagoma, washa moto ndani yako. Pata hasira chanya. Hasira ya kusema: "Huu mlango hauwezi kunizuia mimi kufikia hatima yangu!" Moto huo ndio utakaokupa nguvu ya kutafuta njia nyingine au kutengeneza mlango wako mwenyewe.

​ WEWE NI MFUA VYUMA, SIYO MLALAMISHI
​Leo, simama mbele ya kioo. Jitazame. Wewe siyo mwathirika wa milango iliyofungwa. Wewe ni mshindi ambaye bado hajapata upenyo wake.

​K**a umekataliwa, hiyo ni Direction (Uelekeo), siyo Rejection (Kukataliwa). K**a umekwama, hiyo ni Pause (Mapumziko), siyo Stop (Mwisho). Nenda kagonge tena. Nenda katafute njia nyingine. Na ikibidi, vuka ukuta! Dunia haina zawadi kwa wanaokata tamaa, ina taji kwa ajili ya wale wanaopigana mpaka milango yote ifunguke!

ZINGATIA:...👇👇👇
01/03/2026

ZINGATIA:...👇👇👇

23/08/2025
23/08/2025

Unahitaji watu ili UFANIKIWE

23/08/2025

Stay positive

Zingatia....
23/08/2025

Zingatia....

03/08/2025

Kuwa mwaminifu kwako mwenyewe na kuwa na ujasiri wa kushinda hofu yako

03/08/2025

One of the most beneficial and valuable gifts we can give to ourselves in this life:
is allowing ourselves to be surprised! It is okay if life surprises you. Its a good thing!

Address

Area D
Dodoma Outlying

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ushauri wa Biashara. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ushauri wa Biashara.:

Share