28/10/2025
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imekamilisha kikao chake cha Oktoba 27, 2025 na kutoa maamuzi muhimu kuhusu matukio mbalimbali ya Ligi Kuu na Championship.
Ligi Kuu ya NBC:
Fountain Gate FC 1-0 Dodoma Jiji: Mwamuzi Shomari Lawi ameondolewa kuendesha mechi mizunguko 5 kwa kushindwa kutafsiri sheria za mpira vizuri. Mchezaji Lamela Maneno amefungiwa mchezo 1 kwa kadi za njano.
Dodoma Jiji vs Pamba Jiji: Pamba Jiji imepewa ushindi wa 1-0 baada ya Dodoma Jiji kushindwa kuandaa mchezo kikamilifu. Shabiki Dinani Malugu amefungiwa miezi 6 kwa kutoa lugha ya kashfa dhidi ya TFF.
Faini kwa Klabu:
Mtibwa Sugar: Sh. 20,000,000 kwa kucheza michezo 4 bila kocha mkuu mwenye ujuzi.
TRA United: Sh. 15,000,000 kwa kucheza michezo 3 bila kocha mkuu mwenye ujuzi.
Ligi ya Championship ya NBC:
Kagera Sugar FC 2-1 Barberian FC: Klabu imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 kwa kuchelewa kuwasilisha uwanjani.
African Sports SC 1-0 B19 FC: Daktari wa klabu, Mohamed Lukuwa, amefungiwa michezo 3 na alipe Sh. 500,000 kwa kumpiga mchezaji wa B19, Ramadhani Omary.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inasisitiza umuhimu wa kufuata sheria na taratibu za mashindano ili kuhakikisha Ligi inakuwa shindano safi na huru.