Abm Radio Dodoma

Abm Radio Dodoma Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Abm Radio Dodoma, Radio Station, Dodoma.

17/08/2026

Muhindi amechachamaa kweli kweli na kile ambacho kinaendelea ndani ya klabu ya

Endelea kutufuatilia ABM RADIO DODOMA

17/08/2026

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa agizo la kukamatwa kwa dereva yeyote atakayepaki lori katika maeneo ya service road bila kufuata utaratibu wa maegesho.

​Chalamila ametoa agizo hilo leo, Agosti 17, 2026, wakati wa ziara yake katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Temeke, ambako amekagua matumizi ya barabara na kubaini malori yakipaki katika maeneo yasiyoruhusiwa.

​Amesema tabia hiyo inasababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara, ikiwemo kuziba njia na kuathiri matumizi sahihi ya miundombinu ya barabara.

​Kutokana na hali hiyo, amewaagiza viongozi pamoja na vyombo vinavyohusika kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa na madereva wanaokiuka utaratibu wa maegesho wanachukuliwa hatua.

​Chalamila amesema hatua hiyo inalenga kurejesha utaratibu katika matumizi ya barabara, pamoja na kuhakikisha miundombinu hiyo inatumika kwa usalama na manufaa ya watumiaji wote.

Endelea kutufuatilia ABM RADIO DODOMA

17/08/2026

Mzazi ashangazwa na T -shirt aliyomnunulia mtoto wake dondosha Comment yako kuhusu hili.👇👇👇

Endelea kutufuatilia ABM RADIO DODOMA

17/08/2026

Miami nchini Marekani alishuhudiwa roboti wa kusambaza bidhaa wa kampuni ya Prime akijirushia kwenye maji baada ya kufanya safari nyingi za kupeleka bidhaa sehemu alipoagizwa.

Mashuhuda waliochukua na kuchapisha video hiyo wanasema walimuona akielekea moja kwa moja hadi ukingoni na kudondokea kwenye maji wakiwa wana uhakika kuwa hajapoteza muelekeo (GPS malfunction) bali alifanya makusudi.



Endelea kutufuatilia ABM RADIO DODOMA

17/08/2026

Upande wa Jamhuri umefunga ushahidi wao kwa Shahidi wa 18 katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

​Akizungumza leo Agosti 17, 2026 Mahakamani, Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga amesema msimamo huo umefikiwa baada ya Jamhuri kufanya tathmini ya kina ya ushahidi na hoja zote zilizowasilishwa katika kesi hiyo.

​Hata hivyo, Katuga ameomba Mahakama iruhusu Jamhuri kuwasilisha hoja za ziada kueleza sababu zinazowafanya waone Lissu ana kesi ya kujibu, ombi ambalo Lissu amepinga akieleza kuwa sheria tayari inaweka utaratibu unaopaswa kufuatwa katika hatua hiyo.
​Iwapo Mahakama itaamua kuwa Lissu ana kesi ya kujibu, atapewa nafasi ya kuanza kujitetea kwa kuwasilisha ushahidi na Mashahidi wake na endapo Mahakama itaamua kuwa hana kesi ya kujibu, kesi hiyo itafikia mwisho.

​Kesi hiyo inaendelea mbele ya jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru.

Endelea kutufuatilia ABM RADIO DODOMA

17/08/2026

Neno kutoka kwa Mtumishi wa Mungu Mtume Boniphace Mwamposa wa madhabahu ya Mwamposa Boniface Godwin Usiogope amini tuh.

Endelea kutufuatilia ABM RADIO DODOMA

17/08/2026

Haya vuka ilijaribu au kikulambe 😂😂😂🤣🙌
ABM RADIO DODOMA

16/08/2026

K**a huwaga unaambiwa mamtu mamtu ndo huyu sasa.😂😂😂😂

Endelea kutufuatilia ABM RADIO DODOMA

16/08/2026

Mchome kiongozi mwandamizi wa chama cha democrasia na maendeleo chadema.

Endelra kutufuatilia ABM RADIO DODOMA 91.2

16/08/2026

Mtoto mwenye umri wa miezi minne ametelekezwa katika Kituo kidogo cha magari ya abiria yanayosafiri kutoka Babati kuelekea Wilaya ya Hanang', Mkoa wa Manyara.

​Mtoto huyo anadaiwa kutelekezwa na abiria mmoja aliyesema anatokea Arusha kuelekea Mwanza, baada ya kumkabidhi kwa mjasiriamali, Glory Lazaro aliyekuwa akifanya biashara ya kuuza bidhaa mbalimbali katika kituo hicho.

​Kwa mujibu wa Glory, tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni, Agosti 15, 2026 ambapo abiria huyo alimkabidhi Mtoto akidai kuwa angerejea, lakini aliendelea na safari na hakurudi tena.

​Glory amesema tukio hilo limemweka katika mazingira magumu kutokana na kwamba tayari ana Watoto watano anaowahudumia na hana uwezo wa kifedha wa kumlea Mtoto huyo peke yake.

​Kutokana na hali hiyo, ameiomba Serikali, mamlaka husika pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia ili Mtoto huyo apate malezi, ulinzi na huduma stahiki.

Endelea kutufuatilia ABM RADIO DODOMA

Address

Dodoma
41203

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Abm Radio Dodoma posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category