JUVE MEDIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali itaendelea kuthamin...
10/08/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali itaendelea kuthamini mchango wa Taasisi za Dini ambazo kwa namna ya pekee zimekuwa zikishiriki katika kutoa mchango kwenye sekta za Afya na Elimu hapa nchini.

Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya wa Uru Seminari, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema – Tabata Kimanga Jijini Dar es Salaam. Amesema kwa miaka mingi na kwa asilimia kubwa Taasisi za dini zimechangia katika utoaji wa huduma za elimu na afya, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi hizo ili kufanikiwa zaidi katika kulijenga Taifa.

Makamu wa Rais amesema Malezi yanayotolewa katika Taasisi za elimu za dini ikiwemo Shule ya Uru Seminari ambayo husisitiza Sala, Kazi na Masomo yanapaswa kutiliwa mkazo katika malezi ya vijana wa sasa. Amesema vijana watakavyoweza kumjua Mungu, kufanya kazi kwa bidii pamoja na kupata elimu wataweza kulijenga vema Taifa kupitia ujuzi na hivyo kuepusha tabia za kupata kipato kupitia njia zisizo sahihi.

Makamu wa Rais amewashukuru, walimu, walezi na wanafunzi waliopata elimu Uru Seminari kwa ushirikiano na malezi mazuri ambayo yalifundisha kumtumikia Mungu pamoja na Wanadamu.

Amewasihi Wanajumuiya ya Uru Seminari kuendeleza umoja na kuhakikisha unakuwa wenye tija kwa Taifa, pamoja na kuendelea kuiombea nchi na Viongozi wake.

Ibada ya Misa Takatifu ya Wanajumuiya wa Uru Seminari, imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, Mhashamu Joseph Mlola.

Akitoa mahubiri kwa Wanajumuiya wa Uru Seminari , Askofu Mlola amewasihi kukumbuka wito muhimu walionao wa kupeleka tunu njema ya Maisha ya kiimani kuishi kwa kumpendeza Mungu pamoja na wanadamu. Amesema ni muhimu kuwa mstari wa mbele kupeleka matumaini, ukweli, amani na haki.

Uru Seminari ni Shule inayomilikiwa na Shirika la Mitume wa Yesu chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Moshi Mkoani Kilimanjaro.

MATUKIO KATIKA PICHA: ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU YA MAHAFALI YA DARASA LA VII NA UTOLEWAJI WA SAKRAMENT YA KIPAIMARA BRO...
09/08/2026

MATUKIO KATIKA PICHA:
ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU YA MAHAFALI YA DARASA LA VII NA UTOLEWAJI WA SAKRAMENT YA KIPAIMARA BROTHER MARTIN PRE & PRIMARY SCHOOL .

MISA IMEADHIMISHWA JUMAMOSI 8/8/2026 KATIKA VIWANJA VYA BROTHER MARTIN PRE & PRIMARY SCHOOL NA KUADHIMISHWA NA PADRE JOHN GRESON (VICAR WA WATAWA) AMBAPO PIA AMETOA SAKRAMENT YA KIPAIMARA KWA VIJANA 63 WA SHULE HIYO

MATUKIO KATIKA PICHA - MOSHI▪︎ Matukio mbalimbali wakati wa Kubariki na kuzindua Nyumba ya  Maaskofu kabla ya Masifu ya ...
04/08/2026

MATUKIO KATIKA PICHA - MOSHI
▪︎ Matukio mbalimbali wakati wa Kubariki na kuzindua Nyumba ya Maaskofu kabla ya Masifu ya Jioni kueleka Kilele cha Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu, wa Askofu Ludovick Minde ALCP/OSS Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi.
▪︎ Uzinduzi huo umefanyika katika Makazi ya Askofu na umehudhuriwa na Wahashamu Maaskofu, Mapadre, Watawa, Viongozi wa Serikali ya Mtaa, Waamini walei pamoja na wageni waalikwa.

MATUKIO KATIKA PICHA - MOSHI▪︎ Mhashamu Isaac Amani Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha akizindua rasmi Nyumba ya  ...
04/08/2026

MATUKIO KATIKA PICHA - MOSHI
▪︎ Mhashamu Isaac Amani Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha akizindua rasmi Nyumba ya Maaskofu eneo la Shanti Town, Jimbo Katoliki Moshi.
▪︎ Uzinduzi huo umefanyika katika Makazi ya Askofu na umehudhuriwa na Wahashamu Maaskofu, Mapadre, Watawa, Viongozi wa Serikali, Waamini walei pamoja na wageni waalikwa.

MATUKIO KATIKA PICHA.ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU YA JUBILEI YA 25 YA PAROKIA YA MT GASPAR MAKOLE JIMBO KUU KATOLIKI DODOM...
03/08/2026

MATUKIO KATIKA PICHA.
ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU YA JUBILEI YA 25 YA PAROKIA YA MT GASPAR MAKOLE JIMBO KUU KATOLIKI DODOMA.
MISA ILIYOADHIMISHWA NA ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU KATOLIKI LA DODOMA ASKOFU BEATUS KINYAIYA KATIKA PAROKIA YA MAKOLE.

MATUKIO KATIKA PICHA .ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU JUBILEI YA MAPADRE 7 WA JIMBO KUU KATOLIKI LA DODOMA AMBAO MWAKA HUU 20...
03/08/2026

MATUKIO KATIKA PICHA .
ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU JUBILEI YA MAPADRE 7 WA JIMBO KUU KATOLIKI LA DODOMA AMBAO MWAKA HUU 2026 WAMETIMIA MIAKA 25 YA UPADRE.
MISA IMEADHIMISHWA NA ASKOFU MSAIDIZI WA JIMBO KUU KATOLIKI LA DODOMA ASKOFU WILBROAD . H. KIBOZI KATIKA PAROKIA YA MT GEMMA GALGAN NKUHUNGU

HABARI PICHA .MISA TAKATIFU YA NADHIRI ZA DAIMA PADRE EMMANUEL MUTAMBO SJ , (SHIRIKA LA JESUIT FATHER) PAROKO WA PAROKI ...
03/08/2026

HABARI PICHA .
MISA TAKATIFU YA NADHIRI ZA DAIMA PADRE EMMANUEL MUTAMBO SJ , (SHIRIKA LA JESUIT FATHER) PAROKO WA PAROKI YA K/NDEGE NA DEKANO WA DEKANIA YA MY GEMMA GALGAN JIMBO KUU KATOLIKI DODOMA

HABARI PICHA .PICHA ZA WANACHAMA WA SHIRIKA LA MT ANNA PAROKIA YA MT PETRO MTUME SWASWA JIMBO KUU KATOLIKI LA DODOMA .HI...
26/07/2026

HABARI PICHA .
PICHA ZA WANACHAMA WA SHIRIKA LA MT ANNA PAROKIA YA MT PETRO MTUME SWASWA JIMBO KUU KATOLIKI LA DODOMA .
HII NI BAADA YA ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU YA KUPOKELEWA KWA WANACHAMA WAPYA WA SHIRIKA LA MT ANNA ,IBADA ILIYOFANYIKA KATIKA PAROKIA YA MT PETRO MTUME SWASWA NA KUADHIMISHWA NA PADRE SILJO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameungana na Familia, Waumini, Viong...
23/07/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameungana na Familia, Waumini, Viongozi na Wananchi mbalimbali katika Misa Takatifu ya kumbukumbu ya miaka sita tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamin William Mkapa, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Immaculate, Upanga Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 23 Julai 2026.

Address

IPAGALA
Dodoma
41217

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when JUVE MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share