Msiri Wako

Msiri Wako Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Msiri Wako, Digital creator, Dodoma.

Una Mengi Moyoni ❤️ Mwako Na Uwenda Umekosa Mtu Sahihi Wa Kumweleza Hisia Zako.KARIBU "Msiri Wako" Tupo Kwaajili Ya Kukusikiliza,Kukuelewa Na Kukupa Mwongozo Wa Changamoto Yoyote Ile Uliyonayo Kumbuka Kipaumbele Chetu Ni Usiri Kwa Asilimia 💯 Karibu Sana.

Ushauri Pokea Ila Kabla Ya Kuchukua Maamuzi Jipe Muda Wa Kutafakari Kabla Ya Kuchukua Hatua..."Msiri Wako" Leo Nimekuja ...
14/06/2026

Ushauri Pokea Ila Kabla Ya Kuchukua Maamuzi Jipe Muda Wa Kutafakari Kabla Ya Kuchukua Hatua...

"Msiri Wako" Leo Nimekuja Na Kisa Cha MUUZA MAZIWA YA NG'OMBE Ili Ujifunze Namna Ushauri Unavyoweza Kuongeza Tatizo Badala Ya Kutatua Tatizo...

✍️Ni Kweli Tunapitia Changamoto Nyingi Za Maisha Na Pia Tunahitaji Watu Sahihi Wa Kutuliwaza Na Kutushauri Pale Tunapokua Katika Hali Ya Sitofahamu...

✍️Ila Kupitia Hizo Hali Unaweza Jikuta Umepata Ushauri Wenye Kubomoa Baada Ya Kujenga Na Mwishowe Ukajikuta Ushauri Umekua Sehemu Ya Tatizo Kwako...

🤗Ayaa Maneno Yasiwe Mengi Twende Kwenye Kisa Cha MUUZA MAZIWA YA NG'OMBE Ili Upate Kujifunza Kupitia Hiyo Stori...

🐄Kuna Bwana Mmoja Kwa Jina Anaitwa JUMA KISHINGO Ila Mtaani Anajulikana Zaidi Kwa Jina La JUMA MANG'OMBE...

🛖Ni Mfugaji Maarufu Wa NG'OMBE Katika Kijiji Cha Mkasale Kilichopo Wilaya Ya Tunduru Mkoa Wa Ruvuma...

🐄🥛JUMA MANG'OMBE Anajulikana Kijiji Kizima Kwasababu Katika Eneo Hilo Ni Yeye Pekee Anayefuga NG'OMBE Na Kupelekea MAZIWA YA NG'OMBE Yapatikane Nyumbani Kwake Tu...

🥛🐄 Wanakijiji Wengi Walipendezwa Na Ubora Wa Maziwa Yake Na Kupelekea Huitaji Kuwa Mkubwa Kuliko Uzalishaji Yaani Ilifika Hatua Kwenda Kwa Bwana JUMA MANG'OMBE Na Kurudi Na Pesa Yako Ni Jambo La Kawaida...

🧝Siku Moja Majira Ya Saa Moja Usiku Baada Ya Bwana JUMA MANG'OMBE Kumaliza Kazi Ya Kukamua Na Kuwauzia Wateja Wake

•Alijipumzisha Sebuleni Huku Akiwa Anaangalia Taharifa Ya Habari Channel Ten...

🚪 Mara Mlango Ukagongwa Hodiii Hodiii Hodiii Mara Tatu Mfululizo Ilibidi Iwe Hivyo Kwasababu Sauti Ya Runinga(TV) Ilikua Kubwa Kidogo

•Kwahiyo Mgeni Aliamini Inabidi Aite Kwa Nguvu Ili Wapate Kumsikia...

🚪Mzee JUMA MANG'OMBE Akaitia Karibu Fungua Mlango Upo Wazi, Ndipo Akaingia Kijana Mtanashati Anayejulikana Kwa Jina La Side Boy...

🧝Side Boy Aliingia Ndani Na Akakaribishwa Kukaa Kwenye Kochi Ijapokua Bwana JUMA MANG'OMBE Mwenyewe Alikua Amekaa Chini Kwenye Mkeka

•Maana Ndio Kawaida Yake Anapokua Sebuleni Anapendelea Zaidi Kukaa Kwenye Mkeka Na Sio Kwenye Kochi...

🧑‍🎄Side Boy Ni Kijana Anayeishi Jirani Na Bwana JUMA MANG'OMBE Ni Mtoto Wa Mzee Nguchiro Ila Maisha Yake Anayaishi Zaidi Dar es salaam

•Kwahiyo Hapo Kijijini Huwa Anakuja Mara Moja Moja Kusalimia Wazazi Wake Pale Anapopata Nafasi...

🛖Kijiji Kizima Kinamwamini Side Boy Kwasababu Kila Anapokuja Uwa Anakuja Na Story Mbalimbali Zinazohusu Maisha Ya Dar es salam

•Na Pia K**a Unavyojua Kuishi Mjini Ni Shule Kwahiyo Side Boy Anatumia Hiyo Nafasi Ili Aonekane Yeye Ni Mjanja Kuliko Watu Wote Pale Kijijini...

👥 Baada Ya Kuingia Ndani Na Kukaa Mazungumzo Yakaanza K**a Ifuatavyo...

Bwana Juma: Karibu Kijana Wangu

Side Boy: Shikamoo

Bwana Juma: Marahabaa Habari Za Masiku

Side Boy: Nzuri Mzee Wangu Vipi Wewe Na Familia Yako Kwa Ujumla

Bwana Juma: Tunamshukuru MWENYEZI MUNGU Bado Anaendelea Kutupa Pumzi Zake Vipi Wewe Na Familia Pia

Side Boy: Salama Wazee Nimewakuta Wako Salama Salimini

Bwana Juma: Ayaah Karibu Sana

Side Boy: Asante, Sasa Mzee Wangu Nimekuja Hapa Kwako Ninajambo Nataka Nikushauri

•Maana Tangu Nipo Mdogo Nakuona Upo Unapambana Na Ufugaji Wako Hadi Leo Hii Umetengeneza Jina Kijiji Kizima Kinakujua...

Bwana Juma: Ni Kweli Kabisa Ufugaji Wa NG'OMBE Ndio Unaniendeshea Maisha Yangu Ndio Maana Siwezi Kuacha Eeh Nakusikiliza Kijana Wangu...

Side Boy: K**a Unavyojua Mimi Maisha Yangu Yapo Dar es salam Kuna Mambo Mengi Nimejifunza Kupitia Kuisha Huko Mjini

•Sasa Nimeona Haitakua Vyema Niwe Na Jambo Lenye Kukufahaa Halafu Nikae Kimya Nimeona Bora Nije Nikuambie Mzee Wangu...

Bwana Juma: Karibu Kijana Wangu Nakusikiliza

Side Boy: Nimeona Unauza Maziwa Ila Kuna Idadi Kubwa Ya Watu Wanakosa Maziwa Je Huoni K**a Kuna Pesa Unaipoteza Kwa Kushindwa Kuwahudumia Na Hao Wateja Wanaorudi Kila Siku...???

Bwana Juma: Ni Kweli Kabisa Kijana Wangu Ila K**a Unavyojua Siwezi Hudumia Watu Wote Kwasababu Maziwa Ninayozalisha Ni Machache Ukilinganisha Na Idadi Ya Wanaohitaji.

Side Boy: Ndio Maana Nimekuja Hapa Nataka Nikupe Mbinu Ya Namna Ya Kuuza Kwa Wateja Wote Bila Kuruhusu Mtu Ata Mmoja Kurudi Na Pesa Yake Nyumbani...

Bwana Juma: Aisee Nitakushukuru Sana Kijana Wangu Hii Ndio Faida Ya Vijana Kutembea Mnakua Na Mawazo Mapya Kuliko Sisi Tunaokaa Sehemu Moja Akili Zetu Zinakua Zimeganda...

👥😂🤣 Kikapita kicheko Cha Wote 😂😂👥

Side Boy: Ipo Hivi Unachotakiwa Kufanya Ni Wewe Kuongeza Maji Kwenye Maziwa Kwasababu Ata Huko Mjini Watu Wanafanya Hivyo Na Wanauza

•Ila Nakushangaa Wewe Umekomaa Na Kuuza Maziwa K**a Yalivyo Ndio Maana Yanakua Machache Na Kwa Mtindo Huo Ata Ufuge NG'OMBE Wengi Kiasi Gani Hautaweza Kuhudumia Watu Wote...

Bwana Juma: Kimya K**a Sekunde 5 Hivi Kisha Akajibu Ni Kweli Eeh Naweza Ongeza Maji Na Nikaongeza Kuhudumia Watu Wengi Zaidi...!!!

Side Boy: Ndio Mzee Wangu We Fanya Hivyo Utakuja kunipa Ushuhuda Na Utakuja Kunishukuru Kwa Wazo Langu Nililokupa...

Basi Mazungumzo Yanakaendelea Na Story Zingine Za Pale Mtaani Hadi Side Boy Alipoaga Kwenda Nyumbani Kwao...

💦 🐄🥛Bwana JUMA MANG'OMBE Siku Iliyofata Bila Kukawia Akaanza Kuchanganya Maziwa Na Maji K**a Alivyoshauriwa Na Side Boy...

💸💰 💸 Mzunguko Wa Pesa Ukaongezeka Wateja Wakaongezeka Mpaka Bwana JUMA MANG'OMBE Akajihisi Alikua Wapi Siku Zote Kufanya Huo Mchezo...

📱 Alimpigia Simu Side Boy Kumshukuru Ndani Ya Muda Mfupi Ushauri Wake Umefanya Kazi Kuliko Alivyotarajia...

🚨🛑🚨 Ghafla Kadri Siku Zinavyozidi Kwenda Wateja Wakaanza Kupungua Kwa Kasi Ya 5G Mara Maziwa Yakaanza Kubakia Yaani Hauzi Yote K**a Mwanzo...

🥲🥲 Biashara Ikawa Ngumu Wateja Hawapo Tena Bwana JUMA MANG'OMBE Hali Yake Ya Kifedha Ikaanza Kudolola Ndipo Anakuja Kuambiwa Watu Hawana Imani Na Yeye Tena Kwasababu Anaweka Maziwa Maji...

💔💔Akaacha Kuweka Maji Ila Wateja Bado Hakuna, Ikamlazimu Kutembea Nyumba Hadi Nyumba Kuwaambiwa Sahivi Maziwa Yake Ni Safi Haweki Tena Maji Ila Ikawa Bado Hawamuamini...

🐄🧝Mwisho Ikabidi Aanze Kutembea Na Ng'ombe Zake Kupita Kuwakamulia Watu Majumbani Ili Kuwaaminisha Maziwa Ni Safi...

❤️ FUNZO ❤️
Sio Kila Ushauri Unatakiwa Kuufata Kuna Ushauri Mwingine Unaweza Ukaonekana Mzuri Kwako Ila Baada Ya Muda Unakuja Kugundua Ilikua Ni Shimo La Kuangamia Kwako...

JE.. UMEJIFUNZA NINI KUPITIA HIKI KISA...???

🙏Naomba Share Huu Ujumbe Ili Uwafikie Watu Wengi Zaidi...

"MSIRI WAKO" TUPO KWAAJILI YAKO

Address

Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Msiri Wako posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share