09/09/2025
Happy birthday to Me.
Namshukuru Mwenyezi Mungu Kwa kunifikisha leo hii, siku muhimu sana katika maisha yangu. Ndio, ni siku yangu ya kuzaliwa nikiwa na Miaka kibao. Hakika ni Miaka MINGI yenye furaha na maumivu mengi.
Kuna wakati nilifurahi sana, na kuna wakati nililia Tena Kwa maumivu makali yenye kuumiza na kukatisha tamaa kutoka Kwa wanadamu na tena watu wa karibu. Kuna wakati nilikata tamaa kitokana na nyakati ngumu nilizopitia lakini Mwenyezi Mungu kamwe hakuniacha, nilisimama nikafuta machozi na kusonga mbele.
Leo ikiwa ni siku yangu ya kuzaliwa na nikiwa na Miaka MINGI niseme nini ewe Mola wangu zaidi ya kukushukuru Kwa umri huu na hii pumzi ya Bure kabisa, Asante sana, hakika nimekuwa tena nimekuwa haswa. Asante Mungu, Asante Kwa mzazi wangu, Asante Kwa familia yangu na Asante Kwa marafiki wote ambao wamekuwa NAMI nyakati zote za shida na Raha.
Leo ni furaha Kwa kusherehekea siku hii muhimu lakini pia Kwa kusherehekea ushindi wa mitihani yote niliyopitia ambayo pamoja na maumivu makubwa pale nilipoanguka nililia, nikasimama na kufuta machozi na kusema maisha lazima yasonge mbele.
Yapo mengi ya kujifunza na hata pale nilipokosea nimejifunza, wale walioniumiza nimewasamehe japo sintowasahau sababu kovu la donda huacha alama. Maisha lazima yasonge mbele.
Mie leo ni mshindi tena mshindi na mwanamke shujaa asiyekata tamaa. Hata wewe ni mshindi na yote unayopitia Sasa yataisha. Happy birthday Binti wa Saleh, mjukuu wa Mzee Athumani Kiroyan, kutoka katika ukoo wa Mollel, Moivo na Kiroyan.
Tuungane pamoja kusherehekea ushindi huu.