
28/04/2025
Nageuka kuangalia njia niliyopitia January hadi leo naona nyayo za watu wawili waliotembea pamoja.
Nashangaa! nyayo nyingine ni za nani?
, Mungu aliahidi atakuwa nami kila niendako. Zaburi.145:18-19
Lakin nagundua maeneo flani kuna nyayo za mtu mmoja tu.
, Bwana mbona sehemu nyingine uliniacha peke yangu?
Anajibu, mwanangu nyayo za mtu mmoja unazoziona ni nyayo zangu, maana sehemu hizo zilikuwa ngumu sana kwako, kwani njia ilielekea mlimani na kushukia mtoni.
, hivyo nilikubeba mgongoni
Isaya. 43:1-2
Napiga magoti kumshukuru MUNGU, Zaburi. 103:1-4
MUNGU awe nawe katika safari ya maisha yako, akubebe katika magumu yote unayopitia,
Mungu abariki umalize vema mwaka huu.
AMEN.