
06/09/2025
Jeshi la Polisi katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Septemba 6, 2025 limeeleza kuwa wameona picha mjongeo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanamke akimnywesha pombe mtoto mdogo jambo ambalo ni ukatili kwa mtoto na ni kinyume cha sheria za nchi.
Jeshi hilo limetoa wito kwa yeyote anayemfahamu mwanamke huyo asisite kutoa taarifa kwa njia yoyote atakayoona inafaa ambayo ni rahisi kwake au kupitia namba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi 0699 998899.
Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ametoa wito waliorekodi na kusambaza na wanaoijua familia hii watoe ushirikiano kwa kuwataja badala ya kuendelea kuisambaza.