02/10/2025
⚠️ ASILI YA FITNA ZINAZOZUKA KATIKA DINI
Amesema Muhammad bin Ali Ash-Shawkānī رحمه الله katika tarjama ya Ali bin Qāsim Hanish
Miongoni mwa maneno yake mazuri niliyoyasikia kutoka kwake ni haya:
Watu wako katika ngazi tatu:
❶ Ngazi ya juu kabisa ni: wanazuoni wakubwa.
Hawa ndio wanaojua haki na batili, Hata wakikhitalifiana ikhitilafu yao haileti fitna, kwa sababu wanatambua yaliyomo kwa kila mmoja wao.
❷ Ngazi ya chini: watu wa kawaida walioko juu ya maumbile ya asili aliyoumbiwa mwanadamu.
Hawana ugumu wa kuukubali ukweli, Wao humfuata anaye waongoza, akiwa katika haki nao huwa k**a yeye, na akiwa katika batili nao pia huwa mfano wake.
❸ Ngazi ya katikati: hawa ndio chimbuko la shari na asili ya fitna zote zinazozuka katika dini.
Ni wale ambao hawaja jishughulisha na elimu kiasi cha kufikia daraja ya ngazi ya kwanza, na hawajaiacha hadi wahesabiwe miongoni mwa watu wa ngazi ya pili, Hawa, wanapomuona mmoja wa watu wa ngazi ya juu akisema jambo ambalo wao hawalifahamu, na ambalo linapingana na itikadi zao walizodumbukia humo kwa sababu ya mapungufu yao, humrushia mishale ya lawama na kumsingizia kila kauli mbaya, Kisha huwaharibu watu wa maumbile sahihi katika ngazi ya chini, wakawazuilia kuukubali ukweli kwa hila na upotoshaji wa batili, Hapo ndipo fitna za kidini husimama na kuenea!
📚 البدر الطالع (1/473
Tarjama
Abuū Uthaymeēn - Ālly Īkapū
https://t.me/sawtsalaf1
•┈┈•◈◉❒✒❒◉◈•┈┈•