01/04/2025
NYIEEE! HUKU KUMECHANGAMKA ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Kabla sijasema mengi,watoto wa buku bee chukueni chandimu mkacheze nje,wakulu tuna jambo letu.
La, k**a hamko tayari kupitwa na uhondo, KARIBUni mjumuike nasi wakulu USIKU HUU muonje vyenye tulifaidi.
Jamani eee,kumetokea mjadala wa moto ๐ฅ๐ฅ๐ฅndani ya nafsi yangu hadi nikaamua mgogoro huu wa nafsi niulete kwenu.
Kati ya KARIBU ya Seif Shaaban akiwashirikisha Berry Black na Mr Blue,na USIKU HUU ya Mfalme Daudi,hapa simzungumzii Young Dee,namzungumzia Daz Mwalimu a.k.a Daz Baba akiwashirikisha Sajo na Mr Blue,unadhani IPI KALI???
Binafsi nilishajaribu kuziweka katika mzani ngoma hizi mbili nikashindwa kutoa hukumu!
Ukiisikiliza Karibu utaona ndiyo kali zaidi; baadaye ukiisikiliza Usiku Huu utaona ndiyo kali zaidi ๐ค
Halafu sasa,zote zina kauchawi f'lani hivi: ukianza kuisikiliza Usiku Huu utatamani kuirudia mara alfu lela u lela;vivyo hivyo ukianza kuisikiliza Karibu utatamani kuirudia mara alfu lela u lela!
Halafu sasa,zote "zimevamiwa" na mtoto wa mtaa,Nyani Zee Babylon enzi hizo akiwa tozi tozi kweli ๐
Binafsi,nazipenda zote ila katika Usiku Huu napenda zaidi vasi ya Daz Baba pamoja na kiitikio:
Nataka niwe na wewe hapo sista duu/
Unapendeza peke yako usiku Huu/
Na mavazi yako yananiweka roho juu/
Kasi ya kucheza toka chini mpaka juu/.
Halafu katika Karibu, Tonya ni balaa, Blue ni balaa lakini humu Berry Black aliua sana.Huwa nafikiri blaza Seif hata angemuuzia Berry Black ngoma hii iwe yake (Berry Black ft Tonya & Blue) .Napenda zaidi kiitikio na vasi ya Berry Black :
Kamata mchuchu wako njoo turuke k**a vipi k**a hujui n'takufunza kucheza/
Ukiweza k**ata machupa ya 'wine' pombe kali punguza kumeza/
Nicheki nilivyo bling bling nilivyo ching ching n'shapagawa k**a kawa napoteza/
'Stage' k**a kawa nawameza/
Wachumba nawafunza kucheza/
Ukiweza/
Chombeza/
Mcheki Marco Chali alivyo-chill ndani ya 'club' yuko na ka-chixx kake katuliii...
Ka-chixx kana 'good shape' kana 'nice lips every song ' kana-swing hakachokiii/
We' niite Berry Black 'real' /
Uki-feel real ndani ya 'club' niki-clap soo kwa 'chart'-iii/
'Welcome move your body like a snake'/
'Slow shawty style in mini-skirt'/
Skiza 'rhymes, you and me galie'/
Oya wee,hawa jamaa walikuwa na unyamwezi mwingi sana na huo nd'o UKWELI๐๐ซก
Hapo nimejaribu kutafuta mistari ya Berry Black pekee ili niunde 'lyrics' lakini nina uhakika nitakuwa nimechapia sana๐๐๐
Haya hebu ngoja nijaribu kufuatishia kiitikio Tonya anapoimba :
Come njoo tu-dance/
Sweet boo/
Sweet bang with me kariiibu(kariiiiii)
Hii nadhani nimeiotea๐๐๐
Oya,narudia,Bongo Fleva ya kizazi cha kina Tonya Blue Joseline Mb Dog nk. ilikuwa na unyamwezi mwingi sana (na si kwamba nawadharau wasanii wa sasa,hasha)! Kuna ngoma za Tonya hadi leo huwa naambulia kubahatisha tu maneno kadhaa๐Pengine labda kwa sababu mimi ni Bush Star ila kwakweli hawa jamaa walikuwa matozi haswa,si uvaaji tu mpaka matumizi ya lughaโฅ๏ธ
Sasa kwa mfano, kwenye 'bridge' ya ngoma ya Mb Dog iliyoitwa Tip Top,pale mwanadada Keisha unaweza kuniambia aliimba nini? Mimi nilikuwa najiimbia tu mradi liende:
Dantoromero,say Tip Top East African soldiers x2๐
Au kile kiitikio cha Ishk Candeni ya Mb Dog:
Ishk Candeni iiiii/
Ishk sholahaaaiii/
Egiyuvamidooo ishkiiiii/
Mhnaaaaaa๐
Bora liende mradi tu na-enjoy utamu wa melody.
MIMI NADHANI KUNA UMUHIMU WA WASANII HAWA (ALHAMDULILLAHI BADO WAPO) WAANDIKE 'LYRICS' ZA NYIMBO ZAO ILI VIZAZI VIJAVYO VIJE VIFAIDI UTAJIRI HUU WA MIZIZI YA BONGO FLEVA.
Turudi kwenye sokosoko letu la leo: kati ya KARIBU ya Seif Shaaban akiwashirikisha Sajo na Mr Blue na USIKU HUU ya Mfalme Daudi a.k.a Daz Mwalimu kura yako inadondokea wapi? Mimi niko juu ya fensi sijui pa kudondokea kwa kweli,wewe je?
Naitwa Fujo Masta.
April 1,2025,
Dodoma Tanzania.