Chiswagala Stories

Chiswagala Stories > *“Karibu kwenye ulimwengu wa vitabu na stories– Dini, Uzalendo,mahusiano,fantasy, maisha halisi na kila kitu kati yake.

Kalamu yangu, sauti ya roho yako. 📚✍🏾 ”*

22/04/2026

𝕄𝕁𝕌𝔼: 𝐌𝐀𝐘𝐀 𝐀𝐍𝐆𝐄𝐋𝐎𝐔Jina kamili: Marguerite Annie JohnsonAlizaliwa: 4 Aprili 1928, St. Louis, Missouri, MarekaniAlifariki:...
24/11/2025

𝕄𝕁𝕌𝔼: 𝐌𝐀𝐘𝐀 𝐀𝐍𝐆𝐄𝐋𝐎𝐔
Jina kamili: Marguerite Annie Johnson
Alizaliwa: 4 Aprili 1928, St. Louis, Missouri, Marekani
Alifariki: 28 Mei 2014, North Carolina, Marekani

Mtoto aliyeteseka lakini hakuvunjika MOYO

Alikulia katikati ya ubaguzi mkali wa Marekani. Utoto wake haukuwa na maridadi: wazazi walitengana, alipelekwa kulelewa na nyanya yake, na akiwa na umri wa miaka 8 alibakwa na rafiki wa familia. Tukio hilo lilimfunga kimya kwa miaka takribani mitano. Ila kimya chake kilileta kitu alikimbilia kusoma vitabu, na hapo ndiko uandishi wake ulipoamka k**a cheche ya moto chini ya majivu.

Mwanamke wa kazi nyingi, asiye na hofu

Alipofikisha miaka ya ujana, alifanya kazi k**a mpishi, mhudumu, dansa, mwimbaji, hata dereva wa treni mwanamke wa kwanza mweusi kufanya kazi hiyo katika San Francisco. Alikuwa jasiri, na hakupenda mteremko mwepesi; kila hatua yake ilikuwa ushahidi kuwa mwanadamu anaweza kuibuka kutoka shimoni na bado akatembea kifua mbele.

Mwandishi aliyegusa dunia

Kitabu chake maarufu I Know Why the Caged Bird Sings (1969) kilimwinua kimataifa. Ni hadithi ya wasifu, ikiongoza msomaji kupitia mateso, ubaguzi, ukimya, na hatimaye ushindi. Hiki kitabu kilifungua milango kwa waandishi wengine Weusi kuandika maisha yao bila kificho.

Mwanaharakati mwenye sauti nzito

Maya Angelou alishirikiana na wapigania haki k**a Martin Luther King Jr. na Malcolm X. Sauti yake ilikuwa k**a ngoma ya kale nzito, ya kukumbusha watu wasipoteze thamani ya utu. Aliamini katika heshima, kazi, na kusimama imara mbele ya dhoruba.

Mshairi wa taifa

Katika kuapishwa kwa Rais Bill Clinton mwaka 1993, alisoma shairi lake maarufu “On the Pulse of Morning.” Dakika chache tu, na taifa lote lilinyamaza likimsikiliza mzizi wa hekima kwenye jukwaa la historia.

Urithi wake

Vitabu zaidi ya 30 (riwaya, mashairi, wasifu)

Tuzo na shahada zaidi ya 50 za heshima

Filamu na michezo aliyotunga na kuelekeza

Mamilioni waliohamasika kuandika, kusimama, na kuamini kuwa maumivu yao si mwisho

Maya Angelou alituacha ujumbe mmoja muhimu:
“You may trod me in the very dirt, but still, like dust, I’ll rise.”

Na kweli, mpaka leo, bado anainuka katika mioyo ya wengi.

KISA ℂℍ𝔸 𝕄𝔸ℙ𝔼ℕℤ𝕀 𝕐𝔸 KELVIN NA 𝕄𝕀ℝ𝕀𝔸𝕄𝕂𝕀𝕃𝕀ℂℍ𝕆ℙ𝔼𝕃𝔼𝕂𝔼𝔸 𝕌𝕄𝔸𝕌𝕋𝕀Kelvin Otieno alikuwa askari aliyefanya kazi katika mji wa Kisu...
27/09/2025

KISA ℂℍ𝔸 𝕄𝔸ℙ𝔼ℕℤ𝕀 𝕐𝔸 KELVIN NA 𝕄𝕀ℝ𝕀𝔸𝕄
𝕂𝕀𝕃𝕀ℂℍ𝕆ℙ𝔼𝕃𝔼𝕂𝔼𝔸 𝕌𝕄𝔸𝕌𝕋𝕀

Kelvin Otieno alikuwa askari aliyefanya kazi katika mji wa Kisumo. Miaka kadhaa nyuma, alimchukua binti mmoja kijijini kwao aliyeitwa Miriam Achieng. Miriam alitoka kwenye familia masikini sana, na Kelvin akaamua kumsaidia kwa kumpeleka mjini ili awe mke wake wa baadaye.

Kelvin alimhudumia Miriam kwa moyo wote. Alimlipia karo kuanzia chuo cha kati mpaka Chuo Kikuu, alimnunulia mahitaji yote ya maisha, na hata alikuwa akituma pesa kwa mama mzazi wa Miriam k**a msaada wa familia.

Baada ya Miriam kuhitimu masomo yake ya shahada, ghafla alimwambia Kelvin kuwa hana tena mpango wa kuendelea naye. Kwa sauti ya dharau, alimwambia:
"Kelvin, nimechoka kuwa nawe. Wewe huna hadhi wala maisha mazuri ya baadaye. Nimepata mtu mwingine mwenye nafasi kubwa sana jijini Nairobi. Huwezi kuwa mpenzi wangu tena."

Kauli hiyo ilimuumiza Kelvin sana. Kwa majonzi makubwa, aliamua kwenda kwa mama yake Miriam kijijini kuomba msaada wa kumshawishi binti yao akubali kufunga ndoa naye. Lakini mama alimjibu kwa upole kuwa binti yake ni mtu mzima na ana uhuru wa kuchagua mume wake mwenyewe.

Kelvin hakuishia hapo, alikwenda pia kumwambia dada yake Miriam, lakini naye akamkataa kwa maneno ya kuumiza: "Wewe ni askari wa kawaida tu, Miriam sasa ana kiwango kingine. Tafuta mwanamke wa daraja lako."

Moyo wa Kelvin ukajaa hasira na maumivu yasiyoelezeka. Alirudi nyumbani akiwa amekata tamaa. Baadaye alimwita Miriam nyumbani kwake akidai kuwa wanapaswa kuzungumza ili kumaliza tofauti zao. Miriam alikubali kwenda bila wasiwasi mkubwa.

Lakini alipofika, hakukutana na maneno ya maelewano bali na giza la kifo. Kelvin alikuwa amejihami na bunduki, na kwa hasira kali ambazo hakuwa ameweza kudhibiti, alimshambulia Miriam kwa risasi nyingi. Alikufa papo hapo, na ndoto za maisha yake zikakatishwa.
Je wewe unasimama na nani? Kelvin au Miriam
𝙵𝚘𝚕𝚕𝚘𝚠 Chiswagala Stories

𝐇𝐚𝐝𝐢𝐭𝐡𝐢 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐖𝐄𝐋𝐈: 𝐀𝐧𝐭𝐨𝐧𝐢 𝐧𝐚 𝐜𝐥𝐞𝐨𝐩𝐚𝐭𝐫𝐚Wakati wa karne ya kwanza kabla ya Kristo, dunia ya kale ilishuhudia moj...
26/09/2025

𝐇𝐚𝐝𝐢𝐭𝐡𝐢 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐖𝐄𝐋𝐈: 𝐀𝐧𝐭𝐨𝐧𝐢 𝐧𝐚 𝐜𝐥𝐞𝐨𝐩𝐚𝐭𝐫𝐚

Wakati wa karne ya kwanza kabla ya Kristo, dunia ya kale ilishuhudia moja ya mapenzi yaliyotikisa historia. Hii ni hadithi ya Mark Antoni, jenerali maarufu wa Warumi, na Malkia Cleopatra VII wa Misri.

Cleopatra alikuwa mwanamke mwenye akili ya juu, urembo na mvuto usio wa kawaida. Alijua lugha nyingi na alitawala Misri kwa ujanja wa kisiasa. Antoni, akiwa shujaa na rafiki wa karibu wa Julius Caesar, alitambuliana naye baada ya kifo cha Caesar. Walipokutana, haikuchukua muda mrefu mapenzi yao kuchanua.

Walipendana kwa nguvu kiasi kwamba walikuwa tayari kuiacha dunia yote kwa ajili yao wenyewe. Cleopatra alimpenda Antoni kwa moyo wake wote, na Antoni akajikuta akiacha heshima na mamlaka ya Roma kwa ajili ya malkia huyu. Waliishi maisha ya kifahari, wakipanga karamu kubwa, safari kwenye mto Nile, na mipango ya kutawala dunia kwa pamoja.

Lakini mapenzi yao pia yakaleta vita. Warumi wengi walimwona Antoni k**a msaliti kwa sababu ya mapenzi yake ya wazi kwa Cleopatra. Mwisho wa yote, walikabiliana na majeshi ya Octavian (baadaye Kaisari Augustus) katika Vita vya Actium. Waliposhindwa, wakaamua wasiendelee kuishi wakiwa wametenganishwa na wakiwa wameanguka. Antoni alijichoma kwa upanga, na Cleopatra, akihisi dunia haina maana bila mpenzi wake, akachagua kujiua kwa kuiruhusu nyoka aina ya cobra amng’ate.

Hivyo walikufa pamoja, lakini jina lao likabaki milele. Waliandika historia k**a wapenzi waliokuwa tayari kupoteza kila kitu – utawala, mali, na hata maisha – kwa ajili ya mapenzi.
Je wewe wa kwako mnapendana au mnaishi tu Bora liende?

𝐅𝐨𝐥𝐥𝐨𝐰 Chiswagala Stories

SEHEMU YA PILI: FUMBO LA MWAKA 2005Kichwa cha mama kiliegemea ukutani. Alionekana kuishiwa nguvu, kana kwamba maisha yot...
17/05/2025

SEHEMU YA PILI: FUMBO LA MWAKA 2005

Kichwa cha mama kiliegemea ukutani. Alionekana kuishiwa nguvu, kana kwamba maisha yote yaliyokuwa ndani yake yalikuwa yamevutwa na pumzi ya mwisho ya siri aliyoficha.
Jessica alikaa karibu naye. "Mama, tafadhali niambie ukweli wote. Ni nani aliyepiga simu? Baba yuko hai?"
Bi. Rukia alikuna uso wake kwa taulo dogo, kisha akasema kwa sauti ya chini:
"Jessica… mwaka 2005, palitokea jambo kubwa sana kwenye familia yetu. Baba yako alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakilindwa na serikali kwa siri. Alishuhudia tukio la kihalifu kubwa. Ili kumlinda, waliigiza kifo chake. Niliapa sitakufunulia mpaka utakapokuwa tayari—lakini sasa, sijui ni kwa nini ametoroka. Au k**a hiyo simu ilikuwa onyo."
Jessica aliinama kichwa, machozi yakimtiririka. Dunia yake yote ilikuwa imebadilika kwa dakika tano tu.
Kisha mama yake aliongeza:
"Na yule aliyepiga simu usiku… si mara ya kwanza. Ni mtu niliyemjua zamani. Aliwahi kuniambia kuwa siku nikisikia jina la Mzee tena, basi nitambue kuwa muda wa ukweli umefika."
Jessica aliinua uso wake, macho yakiangaza. "Hivyo mama… hatuko salama?"
Mama yake alitabasamu kwa huzuni, kisha akasema:
"Hatukuwahi kuwa salama, mwanangu. Tumekuwa tukijificha kwenye kivuli cha uongo kwa miaka 20. Na sasa, kivuli hicho kimeanza kutoweka."

Chiswagala Stories chiswagalastories.blogspot.com
16/05/2025

Chiswagala Stories chiswagalastories.blogspot.com

SEHEMU YA KWANZA: KICHECHEO CHA USIKUJessica alipowasha taa ya sebuleni, macho yake yalikutana na picha ya familia iliyo...
15/05/2025

SEHEMU YA KWANZA: KICHECHEO CHA USIKU

Jessica alipowasha taa ya sebuleni, macho yake yalikutana na picha ya familia iliyokuwa ukutani—picha ya zamani ya baba, mama, yeye na kaka yake. Alikuwa hajawahi kujiuliza kwa undani kwanini hawakuwa na picha mpya za baba. Aliambiwa alifariki, lakini maelezo yalikuwa mepesi mno.

Sasa, baada ya simu ya saa nane usiku, kila kitu kilianza kutikiswa ndani yake.

“Mama!” aliita kwa hofu, “Mama! Simu imeita! Kuna mtu amesema Mzee ametoroka!”

Mama yake, Bi. Rukia, alitoka chumbani akiwa ameshikilia rosari yake. Macho yake yalikuwa mekundu, kana kwamba alikuwa tayari akilia hata kabla ya kuambiwa chochote.

“Umesema nini?” aliuliza kwa sauti iliyobeba hofu na huzuni ya zamani.

“Mama, simu... simu ya mezani… imeita. Mtu mmoja amesema ‘Mwambie mama, Mzee ametoroka’. Halafu akakata simu.”

Mama yake aliketi sakafuni ghafla, akashika kichwa. “Niliapa kamwe hatutafuatwa… Niliapa watoto wangu wasijue ukweli… Mungu wangu!”

Jessica alipigwa na butwaa. “Mama, mzee gani? Baba si alifariki?”

Mama yake alimtazama kwa macho yaliyojaa aibu na maumivu. “Jessica, baba yako hajawahi kufa… na hiyo simu ya usiku ni mwanzo wa mwisho wa siri niliyoficha kwa miaka ishirini.”

SEHEMU INAYOFUATA: “Fumbo la Mwaka 2005” – Mama anaanza kufungua ukurasa wa siri kubwa ya familia yao, na jina la mtu walilofikiri amekufa linarejea kwa nguvu.

Address

Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chiswagala Stories posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share