20/08/2026
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Deni Mjini, Kombo Mohammed Maturu, ameitaka Chadema kutoa majibu kuhusu tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, akisisitiza kuwa chama kinapaswa kuzingatia misingi ya uwazi na uwajibikaji.
Kombo amesema tayari alishawahi kutoa ushauri kwa chama kuhusu suala hilo, lakini hadi sasa hakuna majibu ya kuridhisha yaliyotolewa, hali ambayo amesema inazidi kuibua maswali miongoni mwa wanachama. Ameitaka Kamati Kuu ya chama kukutana na kutoa majibu rasmi kuhusu tuhuma hizo.
Aidha, amesema kikao cha wenyeviti wa mikoa kilichofanyika hivi karibuni hakikufikia idadi iliyotarajiwa ya viongozi 30, kwani walihudhuria wenyeviti 15 pekee. Kwa mujibu wake, baadhi ya viongozi walishindwa kushiriki kutokana na kutoridhishwa na namna tuhuma zinazomkabili Heche zinavyoshughulikiwa.
Kombo amesisitiza kuwa CHADEMA ni taasisi na si mali ya mtu mmoja, hivyo viongozi wanapaswa kuwaj