
23/03/2025
Ngoja niweke sawa hoja ili kuepuka mgongano na watu wanaochelewa Sana kuelewa,
japokua nitatumia lugha isioeleweka Kwa wepesi ilikuendelea kudumisha tabaka, lakini isipokua TU Kwa atakae ruhusu kutafakari Kwa kutumia ufahamu yeye atapokea uamsho Moja Kwa Moja.........
nianze na historia kidogo......
kabla ya hiki kinachoitwa "UWEKEZAJI WA KIGENI"
Bara la alkeblan(afrika) lilikuwa likivunwa pasina malipo yoyote kwanzia madini, aridhi, mazao, wanyama, mpaka binadamu..
vyote hivi vilipelekwa UGENINI wanakotoka wanaoitwa WAWEKEZAJI Leo, Ili kuijenga miundombinu ya maeneo yao, (nchi/mabara wanakotokea)
na hivyo kuwafanya wako kuwa na nguvu zaidi katika maeneo tofauti tofauti k**a kiuchimi, kisiasa, kijeshi nakadharika nakadharika Leo......
Kwa ufupi Sana...
baada ya wimbi (miaka kadhaa) la nchi nyingi kujipatia uhuru kutoka Kwa wanyonyaji /watawala wao (wazungu) wale waliokuwa wakichukua Kila kitu walichotaka bure kbisa.....
ndipo kukaboreshwa sela mbalimbali kupitia umoja wa mataifa zenye lengo la kuruhusu MGENI kuwekeza kokote atakako ikiwa atazingatia mashariti 1 2 3..
watakayo kubaliana
Sasa hapa ndipo neno MUWEKEZAJI WA KIGENI linazaliwa pamoja na UKORONI MAMBO LEO.....
kwamba ni Mtu yule yule aliekutumikisha Zamani katika kuvuna asilimali ya aridhi yako bila malipo na mateso sana ili akajenge kwake...
Leo anakuja vile vile lakini Kwa propaganda...
hatumii tuteni(mabavu)
anatumia lugha k**a "technical support"
lakini sio kwamba anakusaidia kinyume chake utamsaidia kuvuna asilimali ya aridhi ya nyumbani kwako mwenyewe na wewe kuachiwa asilimia siyofika nusu ya mlichozalisha.....
Kwa kigezo cha ametoa "MITAMBO NA UJUZI"
mmhh mmh mmh anasahau aliomba tumpokee k**a mtoa msaada,
"wale wafanyakazi wasio na ujuzi aliokuwa akiwak**ata Zamani bure(watumwa)
Leo anakuja vile vile ila kwa mazungumzo wa malipo kiasi kwajina la "anatoa Ajira"
Sasa Mimi Sina tatizo na hako ka utaratibu....
shida yangu ni kwamba
KWANINI HAYA TUNARUHUSU YANAFANYIKA SASA
.......zama ambazo tekonolojia imekuwa, maarifa yameongezeka, Kila Kitu kipo wazi....
kwanini hatubebi majukumu yetu wenyewe tunamuachia mgeni afanye kwaniaba yetu na sisi tupo